Elections 2010 Viongozi wa serikali wanafanya hili kwa utashi wao au ni sehemu ya uongozi?

faithful

JF-Expert Member
Aug 10, 2010
378
33
Wadau tafadhali naomba nielimishwe!kwenye uchaguzi mwaka huu nimeona mengi mapya ambayo hayakuwepo miaka ya nyuma.....mfano utakuta baadhi ya viongozi wakubwa wa wilaya na mikoa wanawapokea vema wagombea mbalimbali wa uraisi bila ubaguzi wa vyama vyao na wengine wanahudhuria mikutano yao na kukaa hightable....wengine hadi wanapewa nafasi za kusalimia wananchi jukwaani....na wapo wanaowakaribisha wagombea hawa maofisini huku wakiwa na sare zao....JE NI SEHEMU YAO YA KAZI AU NI ITASHI WAO TU?..JE VIONGOZI HAWA WANATENDA LILILO SAHIHI KUSHIRIKI KWENYE KAMPENI KWA NJIA HII?
 
Faith, unamaanisha jinsi vile CCM wanavyokodisha malori kubeba wahudhuria mikutano na kuwavika watoto wa shule magwanda ya chama??!
30xfz9x.jpg

Hapo kwenye blue, Ndg. Kinana ameshasema ni kwamba "wanajipendekeza" wao wenyewe:
Jana, Kinana alilazimika kuwakana viongozi wa serikali wanaoshiriki mapokezi ya Mama Salma, kwa madai kuwa ziara zake (Salma) ni za kichama.
Alisema viongozi wa serikali wanaojiunga katika misafara ya Mama Salma mikoani, wakitumia magari ya serikali `wanajipendekeza' wenyewe na kwamba chama hakiwatumi kufanya hivyo.
Kutoka Nipashe.
 
Hili la kuwatumia watoto wa shule( wenyewe wanawaita chipukizi) linakera zaidi. Ni kinyume kabisa na KATIBA ya JMT ambayo inaeleza wazi UMRI wa mtu kushiriki SIASA kwa maana ya kupiga kura kuchagua au kuchaguliwa. Asasi za kijamii kama LHRC wanafaa kuliangalia hili kwa kuwa sio jambo jema mtu kuzaliwa na kukua akiwa tayari ni mwanachama wa chama cha siasa kama yalivyo masuala ya DINI, KABILA.
 
Back
Top Bottom