Viongozi wa serikali chini ya ulinzi mauaji ya M/kti Arumeru.

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Akizungumzia tamko la CCM lililotolewa na Nape kukanusha tuhuma za kuhusika na mauaji, Mnyika amesema, Nape anaficha ukweli juu ya kuhusika kwa baadhi ya viongozi wake na mauaji hayo.

“Kama angetafakari kabla ya kusema angejua kuwa mpaka sasa viongozi wa serikali wanaotokana na CCM wako chini ya ulinzi wa polisi kuhusiana na mauaji ya Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Usa River. Lakini pia viongozi na wanachama wa CCM wametajwa kwa majina kuhusika katika tukio la wabunge wa CHADEMA kukatwa mapanga huko Mwanza. Na mpaka sasa wako chini ya uchunguzi wa Jeshi la Polisi Mwanza,” alisema Mnyika.

CHANZO: Tanzania Daima
 
Wana ccm kolimba,malima,rutihinda,amina chifupa,imran kombe,balali nana kawaua?sembuse akanushe wana chadema
 
Kumwambia nape afikirie ni sawa na kuomba samaki aruke angani; hana akili ya kufikiria na zaidi mtu mwenye uwezo wa kufikiria hawezi kuwa mwanachama wa ccm, sitanii. Kwani unaakili unashindwa kuona wizi, dhuruma, na ualfi wa CCM hadi uwe mwanachama kwa leo hii????

Naililia nchi yangu tajiri yenye watu na serikali masikini; heri watanzania tungezaliwa ng'ombe au samaki mataifa mengine wakatufanya kitoweo.
 
Sera na silaha ya CHADEMA ya 'MABADILIKO BILA FUJO' sasa imegeuka bomu linalokichana chana Chama Cha Mapinduzi ambao wao hivi sasa wanasomeka mbele ya umma kama CCM - Chama Cha Mauaji na fujo za kila aina.

Hakika doa hilo la CCM kukumbatia fujo na hulka ya kuua viongozi wa vyama vya upinzani na wanachama wa kawaida huenda ikachangia kupunguza imani zaidi kwa chama hicho kikongwe nchini.
 
Nape nikama bendera inayo fuata upepo hana lolote alijualo yeye kazi yake ni kuropoka tu! Nina wasiwasi halmashauri ya kichwa chake haifanyikazi vizuri!!
 
Wana ccm kolimba,malima,rutihinda,amina chifupa,imran kombe,balali nana kawaua?sembuse akanushe wana chadema
Umemsahau na yule waziri ambaye mawaziri na maafisa wa polisi walikuwa wanabishana juu ya chanzo cha ugonjwa wake, Ni nani aliyempa sumu? Ulikuwa ni upepo tu lakini kwa sasa umepoa.
 
Umemsahau na yule waziri ambaye mawaziri na maafisa wa polisi walikuwa wanabishana juu ya chanzo cha ugonjwa wake, Ni nani aliyempa sumu? Ulikuwa ni upepo tu lakini kwa sasa umepoa.

Wakampa uwaziri kamili ili amalize mzizi wa fitna
 
Mm siwezi kumlaumu Nape kwani yupo kazini kwake bila kuropoka hawezi kula wala watoto wake hawataenda chooni hivyo basi Nape ropoka ropoka tu Ndungu yangu ila sasa tizama na umma unataka nn na inatengemea nn kutoka kwako siyo unashadadia tuu tena kwa nadharia ya ushadidi pulizi kwani wenzako kwa sasa wapo na nadharia ya zalishi geuzi
 
Umemsahau na yule waziri ambaye mawaziri na maafisa wa polisi walikuwa wanabishana juu ya chanzo cha ugonjwa wake, Ni nani aliyempa sumu? Ulikuwa ni upepo tu lakini kwa sasa umepoa.

huyu waliyempa wizari ya uchukuzi?! Kuna mwingine hana wizara maalumu, naye anaumwa, na kanyoa nywele pia!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom