Viongozi Wa Makanisa Tanzania, Je Wake Wenza Siyo Ufisadi?

FDR.Jr

JF-Expert Member
Jun 17, 2008
1,359
353
awali Ya Yote Ninatangulia Kuwaombea Msamaha Wote Ambao Wako Mbele Ya Haki Ya Mwenyezi Mungu, Naamini Kuwa Tupo Wakristo Wengi Tunaohukumu Wenzetu Kwa Sababu Za Imani Yetu,ndio Maana Namlilia Mungu Awape Raha Wale Wote Waliotutangulia Ikiwa Ni Pamoja Na Wale Wote Ambao Waliishi Ktk Jamii Yetu Wakiwa Ni Wakristo Lakini Walishindwa Kuishi Kwa Maadili Hayo Ya Ukristo Ktk Ndoa. Mungu Wetu Ni Mwingi Wa Rehema Na Msamehevu Asiye Na Mfano. Sasa Ninawaomba Wakuu Humu Ndani Jf Mtafakari Mienendo Ya Wakuu Wa Makanisa Hapa Tanzania Ktk Kuwahudumia Waamini Wao, Utoto Wangu Ktk Ukristo Uliniaminisha Kuwa Hairuhusiwi Kwa Mkatoliki Au Mlutheri Kuwa Na Wake Wawili Na Akakubaliwa Kuwa Mshiriki Wa Kila Siku Kanisani, Hilo Halikuwa Na Nafasi Hususani Walutheri Maana Wao Walikuwa Wanakutenga Na Kanisa Kabisa Na Siku Unaporejea Ilikupasa Usamehewe Na Washarika Wote Ambao Watakupokea Baada Ya Kukiri Kwako Hadharani. Siku Hizi Naona Mambo Yanabadilika Kila Kukicha, Mfano Licha Ya Sokoine Kuwa Na Wake Wawili Alizikwa Kwa Msingi Wa Ukatoliki Tena The Cardinal Rugambwa Na Bishop Denis Waliongoza Mazishi Yale Huku Wakisaidiwa Na Masheikh Na Viongozi Wa Madhehebu Mengine, Juzi Mzee Bhoke Naye Kapelekwa Church Lutheran Kwa Misa Ya Mazishi Huku Wanahabari Wakitutangazia Kuwa Marehemu Mzee Wetu Alikuwa Na Wake Wengi Tu, Na Nina Mashaka Kuwa Hata Mtaalamu Chacha Zakayo Wangwe Kuwa Naye Atapewa Holly Mass, Wakuu Binafsi Nakubaliana Na Holly Mass Kwa Deceased Wote Ila Kinachonitatiza Ni Utaratibu Wa Kubagua Aina Za Waumini Wetu Ktk Final Holly Mass! Ninapenda Wakuu Tuwachallenge Hawa Viongozi Wa Dini Ktk Vita Dhidi Mmomonyoko Wa Maadili.mungu Awabariki Wote Watakaochangia Mada Hii Kwa Nia Kujenga Jamii Iliyo Bora Ya Sasa Na Ijayo,amen
 
umesema vizuri sana, kuna haja ya kutobagua waamini sababu ya status zao katika jamii, wote tunahesabiwa sawa sawa mbele za haki, ktk mazingira mengine kama kweli marehemu alikuwa na wake wengi ndio hatuwezi kujua dk ya mwisho ya uhai wake ali confess vipi kwa padre na hatuna ruhusa ya kuwa judgemental lakini tunapoona kuna mazingira ya kutokuwa na haki yatupasa kuhoji, je kanisa lipo kwaajili ya kila mmoja au?
 
Back
Top Bottom