viongozi wa madaktari Dodoma na Ifakara washikiliwa na polisi

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
wakuu kuna habari kwamba viongozi wa madaktari katika hospitali za Dodoma na Ifakara wameitwa kwa OCD.bado wapo kwenye mahojiano.kama serikali ina madaktari wa jeshi kwa nini serikali inashurutisha madaktari kufanya kazi??
 
kuwashurutisha haitawezekana. ngoja wawadunge insulin na potassium.
 
Kwa umoja wenu mtashinda,na hata hao waliowakamata ni umoja wenu tu ndio utawatoa huko na hata kupatikana kwa baill ni kwa umoja wenu tu na kikubwa mawasiliano yanatakiwa yaimarike,hakuna kulala mpaka kieleweke.
 
Hata wakiwakamata hakuna kurudi nyuma hapa, tena ndio wanazidisha hasira...........:tongue:
 
MM kama pinda angeniomba ushauri, ningemwambia kwanza kabisa awaombe msamaha kwa kuwadharau

pili awe tayari kujadiliano nao pasipo masharti yoyote yale

tatu majadiliano yafanyike kwa ushahidi sio porojo kama za wenzake wanazofanya
 
wakuu kuna habari kwamba viongozi wa madaktari katika hospitali za Dodoma na Ifakara wameitwa kwa OCD.bado wapo kwenye mahojiano.kama serikali ina madaktari wa jeshi kwa nini serikali inashurutisha madaktari kufanya kazi??

kama serikali ilikuwa tayari kuwalipa wabunge posho ya shilingi laki mbili(200,000) kwa kuketi kitako katika eneo lao la kazi, je inashindwa nn kuwalipa madaktari? utaona hapa ndipo serikali inashindwa kutoa majibu ambayo madaktari wataielewa kuwa haina pesa, sio kweli pesa zipo ila kuna matumizi mabaya ya fedha za umma unaofanywa na wachache ambao wengi wao sio wawajibikaji

kuwakamata viongozi wa mgono sio suluhisho bali kukaa kitako ikijumuisha kuwalipa na posho na kuja na suluhu ambayo inatekeleza kwa pande zote

mm naona hata kama daktari angelipwa 3 mn sioni tatizo kwani kama mbunge ambaye hajaenda shule analipwa mshahara wa zaidi ya milioni 2 ukichanganya na marupurupu inafikia karibu milion 7, je kwanini madaktari wasidai kulipwa 3.5 milioni?

niwaachie wengine wachangie
 
pinda utatangatanga sana mwaka huu...yaani wewe ni kama tikiti maji tu
 
Back
Top Bottom