Viongozi wa DINI waikosoa sheria ya madini

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
VIONGOZI wa dini waliotembelea maeneo ya migodi ya dhahabu ya North Mara na Geita mkoani Mwanza, wameikosoa sheria mpya ya madini wakieleza kuwa licha ya kutamka wazi kuwa wananchi wanaohamishwa maeneo ya migodi walipwe fidia, ina kasoro ya kutotaja kiasi kinachotakiwa kutolewa katika fidia hiyo.

Viongozi hao kutoka madhehebu ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata) na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), katika tamko lao jana, wameitaka Serikali kuhakikisha inawalipa fidia waathirika wote wa matukio hayo.

Akisoma tamko la pamoja baada ya ziara yao ya siku nne, Askofu Paul Ruzoka wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora alisema wamejionea ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Askofu huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa TEC alisema mambo mengine yaliyojitokeza katika ziara hiyo ni uharibifu wa mazingira na wananchi kupoteza ardhi yao.
 
Tumelalamika vya kutosha! Tumeshauri vya kutosha! Tumelaumu sana! sasa ni wakati muafaka wa kuchukua hatua.
Tuhakikishe 2015 CCM byebye.
 
Tumelalamika vya kutosha! Tumeshauri vya kutosha! Tumelaumu sana! sasa ni wakati muafaka wa kuchukua hatua.
Tuhakikishe 2015 CCM byebye.

Hapo mtabadili chupa tu mvinyo ni ule ule. Kikubwa ni waTz mbadilike na kuwa wazalendo kwa taifa lenu.
 
Back
Top Bottom