Elections 2010 Viongozi wa dini na wale vingozi wastaafu wanamaanisha nini?

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Nimejaribu kufuatilia kwa undani kwa viongozi wastaafu na viongozi wale wa dini wakiwaamasisha wananchi kutochagua chama bali tuchague kiongozi mwenye sifa safi kama vile tusichague Mafisadi na wale wapenda rushwa! Tunaambiwa tuchague kiongozi atakayeletea wananchi wake maendeleo sasa hapa nataka kujua kiongozi huyo ambaye wanayemtaka achaguliwe ni nani kati ya hawa wagombea wetu! Ni nani msafi hapa anayetakiwa? Lakini naona watanzania wameshamjua wanayemtaka hata nikirejea maneno ya akiongozi mstaafu aliyewahi kuwa waziri mkuu kwenye utawala wa baba wa taifa anavuta Fegi kwa sana sijui yuko wapi tokea kampeni zianze! Nanukuu kauli yake kwa Serikali ya awamu ya nne alisema - WATANZANIA NI WATU WAPOLE SANA LAKINI MSIWAZARAU! IKO SIKU ITAFIKA WATASEMA BASII!! TUMEAMUA!! mwisho wa kunumnukuu, na kweli wakati ndio huu! natumaini watanzania wanamjua nani SAFI na nani Fisadi! wanajanvi hembu angalieni hii hoja kazi kwako hiyo Tarehe 31 Oct!!!
 
kiongozi mwadilifu ni JK, anapiga vita ufisadi kwa nguvu zote si kesi zipo mahakamani subiri majibu!
 
Kesi gani tena na ameshasema wale mafisadi walisingiziwa? kweli ni kiongozi muadilifu aliyeamua kutengua kesi iloko mahakamani na kusema wale washtakiwa walisingiziwa!! asante sana Henge jibu lako safi sana!
 
hey friend,i respect your views ila inachosha na kusoma kwa jinsi ulivo i panga hapo juu,but thanx
 
Back
Top Bottom