Elections 2010 Viongozi wa dini Mwanza wamgomea Membe ujumbe wake kuhusu JK

Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
263
WAZIRI Benard Membe leo alikuwa na wakati mgumu kuwabembeleza viongozi wa madhehebu na Dini za Kikristu pale alipokuwa akifanya nao kikao kuwasii wasimchukue JK na kupuuza uvumi unaoenezwa na kwamba serikali yake inao udini.

Alisema kuwa katika uvumi huo inadaiwa serikali ya Tanzania itajiunga na OIC mwaka 2012 na kuanzisha Mahakama ya kadhi kipindi cha utawala wa JK na kusema hayo siyo kweli na kwamba ametumwa na JK kuja kusafisha hali ya Hewa kwa viongozi wa dini Mwanza.

Katika majibu ya viongozi hao wa dini walimjibu Membe kuwa kama nchi haina Udini kwa nini JK hakemei udini na kwamba kwa nini aibuke na kumtuma Membe wakati huu wa uchaguzi tu kama siyo siasa.

Pili walimueleza kuwa ameshindwa kuwawajibisha mafisadi na kuwanadi jukwaani hivyo kumtamkiwa wazi kuwa hawako tayari kumchagua kuwa kiongozi na kama alitambua jambo hilo alipaswa kuwaona yeye mwenyewe na kutamka wazi mbele yao kuwa Tanzania haijaingia katika Udini na siyo kuwatumia mtu kwani kufanya hivyo ni sawa na kujisafisha katika kampeni.

Membe aliondoka bila muafaka wa viongozi hao wa dini na hata alipofika nje alikataa kuongea na waandishi wa habari.
 
Pili walimueleza kuwa ameshindwa kuwawajibisha mafisadi na kuwanadi jukwaani hivyo kumtamkiwa wazi kuwa hawako tayari kumchagua kuwa kiongozi na kama alitambua jambo hilo alipaswa kuwaona yeye mwenyewe na kutamka wazi mbele yao kuwa Tanzania haijaingia katika Udini na siyo kuwatumia mtu kwani kufanya hivyo ni sawa na kujisafisha katika kampeni.

Jk ajiandae kutukabidhi nchi yetu na huyo Membe mipango yake ya kumrith JK sasa imefikia tamati. yey aende kupiga kampeni jimboni kwake kwa sababu Dr. Slaa atakapofika huko basi jimbo atalitema mwenyewe bila ya kukusudia............
 
Nilisema Juzi kuwa JK anataka kwenda mwanza sasa kaona atume mtu...hahaaa timu beki hazikabi
 
tena huyu Membe wangempasua kabisa kama dereva wao huko Maswa...analeta mambo yake ya ajabu hapa....Akasasifishe hali ya hela nyumbani kwake mwaka huu lazima kieleweke.Yaani mwanza JK atapata kura zinajaa kabakuli
 
Nilisema Juzi kuwa JK anataka kwenda mwanza sasa kaona atume mtu...hahaaa timu beki hazikabi

Nimeongea na Mpiganaji Frederick Katulanda ambaye anafuatilia hali ilivyokuwa na aliyenipatia maelezo hayo, ameniambia kuwa Ujui wa membe ni kama wa Yohana Mbatizaji kwani anatayarisha mapito tu JK yeye anaingia Jumamosi lakini atakuwa Geita kusaka kura.
 
Kijasho chembamba kimewatoka wanamtandao. Ndo waelewe kuwa watz hawawezi kuwa wajinga always!
 
Nimeongea na Mpiganaji Frederick Katulanda ambaye anafuatilia hali ilivyokuwa na aliyenipatia maelezo hayo, ameniambia kuwa Ujui wa membe ni kama wa Yohana Mbatizaji kwani anatayarisha mapito tu JK yeye anaingia Jumamosi lakini atakuwa Geita kusaka kura.

hahaaa JK presha inapanda presha inashuka .....asante kiongozi kwa kutoa muongozo huu...
 
"Dr" kikwete baada ya kuona vijana wengi nchini wanamuunga Dr Slaa sasa amepanga kukutana na vijana wa Jiji la Dar es salaam ilikuwashawishi wAmpigie kura. Tarehe ya kampeni hiyo ya vijana itatangazwa kwenye vyombo vya habari. Chanzo cha habari hii ni UV CCm- Dar.
 
HILO NIMELITHIBITISHA NA NIMAMALIZA KUONGEA NA SIMU NA MMOJA WA VIONGOZI WA DINI MWANZA.

Kiongozi mwingine amesema kuwa Rais ni kama ameamua kuwatukana watanzania. Kwani kuamua kwa makusudi kuwapigia debe watu wenye tuhuma nzito za ufisadi ni kuwafanya watanzania wajinga na wasio weza kufanya lolote. Na wao wamesisitiza kuwa tatizo lao sio dini ya mtu ni maadili.

WIZI UNAFANYIKA NA WATU WALINDWA KAMA WAFALME BADALA YA KUADHIBIWA AU BASI KUACHWA SHERIA ISHIKE MKONDO WAKE.
 
Iv Membe ni hausboi wa baba Lizy au? Au mkata majani wa wale mifugo pale Feli, pole Membe, cku nyingine uckubali ku2mwa sawa eeeh!!!!!!
 
Membe njoo Mwanza tarehe 15 november nitawakusanya viongozi wa dini tuzungumze kwa sasa sooorrrryy. G:A S-confused1:eek:odnight!!!!!
 
Jamani uyu Membe huwa simpendi ata kumuona huwa anajifanya kuongea kwa msisitizo while anachotetea ni vumbi.
Mnataka kutupeleka OIC wakati Tz ni non secural state.Nonesense
 
Back
Top Bottom