Mbeya: Mchungaji Pentekoste adaiwa kuuza kanisa, atimkia Zambia

Ngekewa

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
7,705
1,288
Mchungaji Pentekoste adaiwa kuuza kanisa, atimkia Zambia

2009-03-14 11:14:13
Na Thobias Mwanakatwe, Mbeya


Kanisa la Pentekoste Evangelistic Church lililopo mkoani hapa limeendelea kuandamwa na mikosi baada ya mchungaji wake, Ezekia Mwangomo, kudaiwa kuuza majengo ya kanisa na kukimbilia Lusaka, Zambia.

Mchungaji Mwangomo alikuwa akitoa huduma za kiuchungaji kwenye kanisa lililopo eneo la Sogea Wilaya Rungwe.

Taarifa za mchungaji huyo kudaiwa kuuza majengo ya kanisa zimekuja huku sakata la mchungaji Cosmas Mwasenga wa kanisa hilo lililopo kijiji cha Idiwili wilayani Mbozi, akisota rumande akituhumiwa kukamatwa na viungo vya binadamu.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste Evangelistic Church, Zebadia Mwakatage, hivi karibuni alisema mchungaji Mwangomo alikimbilia nchini Zambia baada ya kuuza majengo ya kanisa.

Askofu Mwakatage alisema kutokana na mchungaji huyo kuuza majengo ya kanisa yaliyopo Kijiji cha Sogea wilayani Rungwe, tayari huduma za ibada zimesitishwa kwa muda mrefu.

Hata hivyo, Mwakatange alisema kanisa lake limeendelea kutoa huduma za ibara kwenye makanisa yapatayo 15 yaliyopo Mbeya, Mara, Mwanza, Dar es Salaam na nchi jirani ya Zambia.

Juhudi za mwandishi wa habari hizi kumpa mchungaji anayetuhumiwa hazikufanikiwa kwa sababu, yupo nje ya nchi.

Hivi karibuni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Zelothe Stephen, alisema mchungaji Mwasenga na mwenzake Luseshelo Mwashilindi walikamatwa na viungo vya binadamu vinavyosadikiwa kuwa vya albino ambavyo walikutwa wakiviuza kwa Sh milioni 30.

SOURCE: Nipashe
 
manabii wa uongo,ndo hao tayari,cjui bado nini tukingochacho.tumrudie mungu!
 
Hapo pana tatizo la mhusika mwengine ambae ndio natumai ni msimamizi mkuu wa kanisa hilo lililopigwa bei aliebambwa na viungo vya Albino ,sasa namna baadhi ya watu walivyo akaona akimbie zake na ili kutafuta hela ya kusafiria na kuanzisha makazi mepya imebidi atapeli wasiokuwa na akili, sidhani kama kulikuwa na hati za kuaminika katika biashara hiyo haramu ya kuuza kitu si chako,ila jamaa inaonyesha alikuwa amepiga longolongo ya hali ya juu hadi kumkubalisha mteja kuuvaa mkenge huo ,kwa maana alienunua huenda akaingia kwenye matatiso kisheria.
 
Back
Top Bottom