Viongozi wa DECI wapelekwa rumande

JosM

JF-Expert Member
Oct 11, 2008
679
17
Viongozi wa DECI wamefikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi ya kula pesa za wananchi,wamekosa dhamana na wamepelekwa rumande.
wenye habari zaidi mnaweza kutuhabarisha zaidi.
viongozi wa DECI.jpg
VIONGOZI WA DECI WAKIWA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU LEO, WAKIKABILIWA NA MASHTAKA MAWILI.
1. KUENDESHA NA KUSIMAMIA MRADI WA UPATU
2. KUPOKEA AMANA KUTOKA KWA UMMA BILA LESENI
 
Last edited:
Watashtakiwa vipi kwa kula hela ambazo serikali inajua kwamba ziko kwenye akaunti ambayo wameifreeze!
 
Watashtakiwa vipi kwa kula hela ambazo serikali inajua kwamba ziko kwenye akaunti ambayo wameifreeze!

mkuu fedha lilizoko kwenye Akaunti ya DECI ni billion 1. Wakati wananchi wamewekeza zaidi ya billion 12.hizo billion 11 hazijulikani ziko wapi,hivyo lazima viongozi wa DECI waeleze hizo pesa ziko wapi.
 
Still i dont get a clue kwenye hii ishu
kesi ilikuwa saa ngapi na mahakama ipi?? au ndo wikend imeanza??
Mtoa hoja pls tupe mwanga ktk hili
 
Hiyo ndiyo serikali ambayo kwa miaka imefumbia macho pyramid schemes ambazo zimekuwa tatizo kwa wananchi halafu sasa ndipo wanajitokeza na kuona ilikuwa ni criminal!! Where are we heading???

Unajua tusiwalaumu wanananchi, ni sawa na wewe kukaa mbali na familia yako halafu mume/mke na watoto wanatafuta sympathy somewhere else. Sera na Shera zetu hazimwezeshi mtanzania wa kawaida kufurukuta, sasa ni kwa nini asitafute vitu kama DECI, MALINGUMU, etc.?/
 
wakati serikali inawaambia DECI ni taasisi ya kitapeli waliandamana na mabango kuitetea,

hao viongozi bora tu waachiwe huru.
 
Still i dont get a clue kwenye hii ishu
kesi ilikuwa saa ngapi na mahakama ipi?? au ndo wikend imeanza??
Mtoa hoja pls tupe mwanga ktk hili

Mchana huu mkuu,ni mahakama ya Kisutu,na wamefunguliwa mashtaka kama matano hivi.
 
Hawa viongozi wa DECI inasemekana walikamatwa saa nane za usiku wa kuamkia leo.
 
hiari vipi? hapa wanaangalia uvunjaji wa sheria. hairuhusiwi kufanya michezo ya upatu na pia hairuhusiwi kuchukua amana kwa wananchi bila kibali?

Ahsante kwa kumemuelemisha huyu mdau.
 
Taarifa zilizotufikia na kuthibitishwa na magazeti ya jioni Viongozi wa DECI wamekamatwa usiku wa manane na kusweka lupango.
Hawa wezi wakishirikiana na wafanyakazi wao wamehamisha hela nyingi na kuzificha tume ya manumba wabaneni p......hao viongozi watasema wameficha wapi hela mikoani ndio balaa wameficha hela nyingi za wadanganyika
 
Sasa sirikali wafanye kazi ya kurudisha mafungu ya wafuja jasho wenzetu, inauma sana mjomba kuona hera zetu zinaliwa kiurahisi 2 kwa mchezo haram wa upatu! Lakin mi naona tatizo ni la hii hii sirikali, make wameshindwa kuwaletea wananchi maisha bora na kutafuta minubu mbadara wa kuwaondoa kwenye lindi la umasikini! Matokeo yake wananchi wamelizwa! Lakin wangefanya nini ikiwa walikuwa hawajui kesho yao? Natania 2 mjomba, lakini kweli nikipata nauri ntaenda kutoa pole kwa wanaupatu waliotapeliwa fedha zao
 
Hivi kuna DECI ngapi ndani ya SIRIKALI na zinafumbiwa macho? Hawa minority wamekamatwa kwasababu hakuwapa ulaji mafisadi wa SIRIKALI. lol
 
Hakuna aliyelazimishwa,ila serikali haiwezi kukaa kimya ikiangalia wananchi wakiibiwa fedha zao na wajanja wachache.

Ni kweli kabisa Mkuu Josm... Tanzania watu wanaoruhusiwa kuwaibia wananchi ni kina Rostam Aziz, Andrew Chenge, Edward Lowassa, Yusufu Manji, Idris Rashidi (wa Tanesco) na Ben Mkapa. Akitokea mwingine yeyote kamata usiku wa manane na peleka rumande bila dhamana.
 
Na tena hapo Serikali wanasema ... 'TUPO SERIOUS' hatutaki wananchi waibiwe! Hatutaki watanzania wapate shida. Rungu lililotumika kuwakamata hawa viongozi wa DECI litumike na kwa hao waheshimiwa. Au pia wanatuzuga?? Baada ya siku 2, watapewa dhamana... then wanakuwa huru kwelikweli
 
Heri wakamatwe maana maisha yao yako hatarini sana

Unajua heri wakamatwe wakamatwe wwakamatwe
 
Ni kweli kabisa Mkuu Josm... Tanzania watu wanaoruhusiwa kuwaibia wananchi ni kina Rostam Aziz, Andrew Chenge, Edward Lowassa, Yusufu Manji, Idris Rashidi (wa Tanesco) na Ben Mkapa. Akitokea mwingine yeyote kamata usiku wa manane na peleka rumande bila dhamana.

macho_mdiliko,

This is the post of the day!
 
Ni kweli kabisa Mkuu Josm... Tanzania watu wanaoruhusiwa kuwaibia wananchi ni kina Rostam Aziz, Andrew Chenge, Edward Lowassa, Yusufu Manji, Idris Rashidi (wa Tanesco) na Ben Mkapa. Akitokea mwingine yeyote kamata usiku wa manane na peleka rumande bila dhamana.

Inasikitisha sana kuona nchi yetu inateketezwa na watu wachache tulio wapa madaraka tukiamini watatuletea maendeleo,leo hii ndio wametugeuka na kujilimbikizia mali wao na shkaji zao.
 
Back
Top Bottom