Viongozi wa CUF na gari lao wafukuzwa na wamachinga hapa soko la Kilombero, Arusha

Sasa hiyo ndio siasa gani mbona sielewi hapa, hao viongozi walikwenda sokoni kwa ajili gani au hilo jimbo mbunge ni wa cuf, naona baadhi ya wananchi wanavuta bangi. Haingii akilini- lakini tujitahidi kutenda tuliyoyaahidi hata kama tuna mbunge mmoja bungeni mbona kafulila anawatoa kimasomaso nccr- tubadilike tuache kuzunguka kutafuta support hali ya kuwa wawakilishi wetu bungeni hawafanyi kitu- ukishindwa kuitumia fursa ndogo uliyopewa hata ukipewa kubwa hutoweza- hichi ndicho kitakachowaangusha wapinzani wengi wasipoamka mapema
 
Pole sana majeruhi wote waliopatwa na huu mkasa wa kupopolewa mawe nadhani watu sasa wanaijua vizuri Chadema.
 
kila vurugu ni cdm inayolaumiwa mjomba mtatiro kajipange upya........siasa kama hizo zitaigharimu cuf
 
Pole sana majeruhi wote waliopatwa na huu mkasa wa kupopolewa mawe nadhani watu sasa wanaijua vizuri Chadema.

wanaijua vizuri kabisa ni chama kinachodai haki kwa gharama yoyote ile, sio mafisadi na wezi kama ccm, chadema wanaamini kuwa haki inatakiwa ipatikane hata kwa ncha ya upanga, tumechoka na udahifu wa serikali ya mr dhaifu!!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​
27/09/2012​
WANACHAMA WA CUF KUPONDWA MAWE NA WAFUASIA WA CHADEMA ARUSHA.ONYO KWA CHADEMA
CUF Chama cha wanachi kinalaani kitendo cha wafuasi wa CUF kupondwa mawe na wafuasi wa CHADEMA walipokuwa wakiendelea na shughuli kutangaza mikutano inayoendelea Arusha . Chama cha wananchi CUF kinasikitishwa nakulaani kitendo cha viongozi wa chadema mkoani Arusha kuwashawishi wafuasi wao kuwaponda mawe wanachama wa CUF wanaoendelea na mikutano ya kisiasa inayofanywa na CUF tangu mwanzo wa wiki hii.Hii imedhihirishwa na maeno na Godbless Lema juzi alipokuwa waapowahutubia wafuasi wa Chadema kwenye viwanja vya Stendi ya Nduruma alisema kwamba CUF wametuvamia na kuwasihi ile slogan ya “kamata mwizi men” sasa ianze.Na ushahidi tuanao. Hata hivyo wameshawishi vijana kugawa kiwanja vya Levorosi stendi ya Nduruma kwa kisingizio kwamba wanataka kuweka meza za biashara kiwanja ambacho CUF tuantegemea kufanya mkutano wa hadhara siku ya Jumapili. Leo asubuhi wanachama wa CUF wamepondwa mawe walipokuwa mtaa wa Kilombero kata ya Levorosi.Kutokana na vurugu hilo gari la matangazo la CUF limepondwa mawe na mwanachama mmoja aitwaye Athuman Abdurahman alipigwa jiwe jichoni na taarifa tumezifikisha polisi. CUF kinaona Chadema kama chama kisichoweza siasa za ustahimilivu,hawajiamini na bado ni wachanga kisiasa.Hii inadhirishwa na kutoelewa maana ya demokrasia na uhuru wa Mtanzania kuamua kujiunga na chama chochote atakacho.Bado hawajakomaa kisiasa kama jinsi CUF ilivyokaomaa kisiasa hatukudhuru chama chochote wanapofanya siasa maeneo mbalimmbali hapa nchini. CUF inatoa onyo kali kwa viongozi wa Chadema kwamba hali hii ikiendelea wajue hawataweza kufanya shughuli zao sehemu yoyote Tanzania kwani uwezo wa kuwafanya tutakavyo tunao na kwasababu wameanza tuanaweza kumaliza.Ile NGANGARI kwa polisi tunaweza kuwahasishia wao wakose pa kukaa, ila hatupendi tufikie huko na kama wanabusara na ni wanasiasa kweli wenye nia ya kutumia hoja badala ya vurugu kumkomboa mtanzania watafakari hilo. CUF inaendelea kusisitiza tutaendelea na shughuli za kisiasa mkoani Arusha hakuna wa kutuzuia na tutaendelea Oparesheni MCHAKAMCHAKA na mikutano itaendelea kufanyika na kama wao ni wababe kweli na wanatumia hoja ya vurugu waendelee na mipango yao ya hujuma na tutawafundisha siasa kwani bado hawajakomaa. Imetolewa na Naibu Mkurugenzi wa Habari ,Uenezi na Haki za Binadamu CUF. Mh.Abdul Kambaya Simu:0719566567 Chanzo www.cuf2015plus@worlpress.com
 
CUF.nafikiri ili cuf wajue ni kuacha kuchangia thread yoyote ile iliyoanzishwa yenye neno cuf
 
Sijaelewa huu ujumbe na nadhani kamwe sitaelewa Mh.Abdul Kumbaya umejichanganya sana kama nikutumika nadhani fanya mahesabu ya kisiasa uone kama hii propaganda itasaidia chama cha CUF
 
Kwa kuwa ushahidi unao basi ungeuweka hapa tuuone kuliko kuandika maneno tu.
 
moderators .... did you verify that this is an official notice from CUF or it is a spam

the author of this notice sounds like a hooligan
 
"cuf ngangari"

Naipenda sana hii slogan sijui kwanini hawaitumii hawa rafiki zangu tangu Mahita Insp.alipowabambikizia visu vya kukatia nyanya akiviita mapanga dah kweli polisi watata!
 
ulijuaje ghafla tu kuwa hao ni vijana wa chadema na siyo wahuni wa ccm.
Mimi hata siwafahamu nyie gwandaz,kila siku mnasema arusha ni CDM hakuna CCM huko lakini vijana wakifanya fujo mnasema ni wa CCM, hebu kuweni na msimamo mmoja basi.
 
Nipo hapa sokoni Kilombero na wamachinga wanajigawia kwa utaratibu mzuri sana kuliko ule uliofanyika na Mkuu wa wilaya kule nmc.

Gari la CUF la matangazo likawa linakuja kuingia ili litangaze mkutano, wanawake wamachinga wamepiga ukunga CCM B wanafiki wanakuja wamachinga wote wakawapigia kelele na gari la CUF likaondoka na kuzima muziki mara moja.

Siungi mkono kauli yakusema ni wana chadema.huu ni upotoshaji uliomkubwa.chadema hawahusiki na hili.badala yake yale nimaamuzi ya wananchi wenyewe kudai eneo lao.ikumbukwe pale ilikua stand zamani wakati huo soko hilo likiwa kwa doctor babu.stand ilivyotolewa soko likahamia huku kilombero na kule kwa doc babu pakauzwa.hata hapo walipovunja ulikuepo uzio wa bati na kwahabari za uhakika palishauzwa kwa mtu binafis.ndio maana hata wafanyabiashara kupewa eneo la uwanja wa mpira nmc kua soko.hali iliyopelekea wanafunzi kugoma kusoma wakidai uwanja wao.
 
Mbunge mmemnyang'anya ubunge tayari bado mnatuma CCM B wakati mnajua fika kuwa hamna chenu Arusha mnadhani ni rahisi wananchi kuwaelewa?
Hebu jisafisheni kwanza na mtuweke wazi,nyinyi ni wapinzani au watawala?
Muulizeni waziri Mkuu alifanywa nini Mwanza then ndio muanze kuropoka hovyo kama kawaida yenu.
 
Pole sana majeruhi wote waliopatwa na huu mkasa wa kupopolewa mawe nadhani watu sasa wanaijua vizuri Chadema.

Usipotoshe, fujo hizi si za cdm bali wamachinga kupinga kufukuzwa katika eneo lao la kufanyia biashara na kupelekwa eneo ambalo halina huduma za muhimu.
Bado unatumia viungo tofauti na akili kufikiria? I mean Mat***kio?????
 
Back
Top Bottom