Viongozi wa CHADEMA kutokumtambua Rais ni Kosa?

Hii nimenukuu kutoka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kosa la CHADEMA liko wapi kulingana na Katiba hii waliyoapa kuilinda na kuitetea?Soma

13.-(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki,bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.
Sheria ya Na.4
ya 1992 ib.8
Sheria ya 2000
Na.3 ib.5

(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambaloni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.
(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya yawatu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombo
vinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
Page 17

(4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi.
(5) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno "kubagua" maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini,jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neno "kubagua" halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia Serikali kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo katika jamii.
(6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria, Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia misingi kwamba:
(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi wa Mahakama au chombo kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kingenecho kinachohusika.

Masharti ya Jumla

Haki ya wajibu
muhimu
Sheria
ya 1984 Na.15
ib.6
29.-(1) Kila mtu katika Jamhuri ya Muungano anayo haki yakufaidi haki za msingi za binadamu, na matokeo ya kila mtu
kutekeleza wajibu wake kwa jamii, kama zilzivyofafanuliwa katika ibara ya 12 hadi ya 28 za sehemu hii ya Sura hii ya Katiba.
(2) Kila mtu katika Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kupata hifadhi sawa chini ya sheria za Jamhuri ya Muungano.
(3) Raia yoyote wa Jamhuri ya Muungano hatakuwa na haki,hadhi au cheo maalum kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi
wake.
(4) Ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheo maalum kwa raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi.
(5) Ili watu wote waweze kufaidi haki na uhuru vilivyotajwa na Katiba hii kila mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli zake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.

Mipaka kwa
haki
na uhuru na
hifadhi kwa haki
na wajibu
Sheria ya 1984
Na.15
ib.6
Sheria ya 1994
Na.34 ib.6

30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
(2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya: -

(a) kuhakikisha kwamba haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma haviathiriwi na matumizi mabaya ya uhuru na haki za watu binafsi;
(b) kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii, amani katika jamii, maadili

(3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii ya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu.

(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika Katiba hii, Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kwa mara ya kwanza na kuamua shauri lolote lililoletwa mbele yake kwa kufuata ibara hii; na Mamlaka ya Nchi yaweza kuweka sheria kwa ajili ya-

(a) kusimamia utaratibu wa kufungua mashauri kwa mujibu wa ibara hii;
(b) kufafanua uwezo wa Mahakama Kuu katika kusikiliza mashauri yaliyofunguliwa chini ya ibara hii;
(c) kuhakikisha utekelezaji bora wa madaraka ya Mahakama Kuu, hifadhi na kutilia nguvu haki, uhuru na wajibu kwa mujibu wa Katiba hii.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
page 25

(5) Endapo katika shauri lolote inadaiwa kwamba sheria yoyote iliyotungwa au hatua yoyote iliyochukuliwa na Serikali au mamlaka nyingine inafuta au inakatiza haki, uhuru na wajibu muhimu zitokanazo na ibara ya 12 hadi 29 za Katiba hii, na Mahakama Kuu inaridhika kwamba sheria au hatua inayohusika,kwa kiwango inachopingana na Katiba ni batili au kinyume cha Katiba basi Mahakama Kuu ikiona kuwa yafaa au hali au masilahi ya jamii yahitaji hivyo, badala ya kutamka kuwa sheria au hatua hiyo ni batili, itakuwa na uwezo wa kuamua kutoa fursa kwa ajili ya Serikali au mamlaka nyingine yoyote inayohusika kurekebisha hitilafu iliyopo katika sheria inayotuhumiwa au hatua inayohusika katika muda na kwa jinsi itakavyotajwa na Mahakama Kuu, na sheria hiyo au hatua inayohusika itaendelea kuhesabiwa kuwa ni
halali hadi ama marekebisho yatakapofanywa au muda uliowekwa na Mahakama Kuu utakapokwisha, mradi muda mfupi zaidi ndio uzingatiwe.
 
- Mkuu kuna njia za Demokrasia za kuonyesha kwa ushaidi kwamba ushindi wa CCM haukupatikana kwa njia za Demokrasia, ndicho sisi wengine tunachokiomba ni kuonyeshwa jinsi Dr. Slaa, alivyoibiwa u-Rais ambao alishinda kama ninakuelewa vizuri!, kwa sababu binafsi siamini kwamba wananchi wengi wamechagua wabunge wa CCM, lakini walikuwa wanamchahua Rais wa Chadema at the same time,

- Halafu ni haki ya kila mwananchi wa taifa hili kutoa maoni yake, isipokuwa hapa JF kwa vile ni uwanja wa werevu tujadili kwa kuonyesha uerevu wetu yaani hoja kwa hoja na ikibidi na evidence mkuu!

William.

Njia ya mojawapo ya kidemokrasi ni kutokutambua utawala uliongia madarakani kwa njia zisizo za kidemokrasi.
 
Wabunge wa CHADEMA, kwanza nataka kuwapa pongezi kwa kuchaguliwa na wananchi kkuwawakilisha bungeni pamoja na CCM kuiba baadhi ya kura zenu huko majimboni kama vile Shinyanga na Tarime, kwa mfano.

Sisi wananchi hata walioko nje ya nchi, tuliona na tulijua kwamba sasa CCM siku zake zimekwisha, wananchi wamechoka kula maharage kila siku, mwaka huu walitaka nao waonje kidogo nyama choma au steki, ndiyo maana wakawachagua viongozi wao kutoka chama cha CHADEMA.

Kitendo mlichofanya wabunge wetu huko Dodoma, si cha kiungwana. Sisi tuliwatuma huko mtuwakilishe na mpige kura humo bungeni kufuatana na maombiyetu, siyo kwenda na kumzilia Rais akitoa hotuba. Kikwete kwa nguvu za NEC na CCM kapitishwa tena ili wakamilishe miradi yao ya miaka 10 waliyoanzisha the last 5 years. Sasa ninyi hata mkizira hotuba yake na kutoka nje ya bunge si sahihi, afdhali kabisa wala msingeenda huko Dodoma. Je posho mtachukua au vipi?. Mimi naona afdhali mjitokeze mbele ya kadamnasi na mtuombe msahama wananchi, na muache upuuzi na tabia za kitoto, muendelee kuwemo bungeni kama wapinzani wa CCM na mjaribu kushirikiana na vyama vungine vya upinzani. Kwa njia hii then tutaweza kuidhoofisha CCM, lakini si kwa kumzilia Rais ambaye hata mfanyeje amekwisha chaguliwa na ataongoza kwa miaka 5 hadi 2015. Tuambieni au mjiuzulu ubunge tuliowapa then tujue wazi kwamba CCM itaendelea kuwatawala mpaka mbaki mifupa mitupu.

Sisi tuliowachagua mtuwakilishe hatukubaliani na kitendo mlichomfanyia Kikwete, Spika , Wabunge, Waziri Mkuu huko Dodoma. Mlijua kabisa kwamba serikali haijaundwa, kwa hiyo ni lazima Rais atoe hotuba ya kumpongeza Spika na Waziri Mkuu, ambao wote wawili nayi mliwapigia kura. Kitendo cha kutoka Bungeni si cha kumdharau Rais Kikwete, ni cha kumdharau Spika na wabunge wenzenu na sisi wananchi tuliowapeleka huko. JIREKEBISHENI NA MUOMBE MSAHA AU LA BASI MJIUDHURU MAPEMA KABLA YA MAMBO KUWA MABAYA ZAIDI.
 
Hawakutaka kumsikiliza jk akiongea kama rais kwani hawamtambui. Tatizo liko wapi???????????? Acha kuandika bila tafakuri.
 
bot_tabimg.gif

Chadema 'yaitikisa' nchi :NI KUTOKANA NA WABUNGE WAKE KUSUSIA HOTUBA YA JK Send to a friend Saturday, 20 November 2010 07:11 0diggsdigg

bungekikwetemno.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Maswa Magharibi kupitia CHADEMA, John Shibuda wakati wa hafla ya kuwapongeza wabunge iliyofanyika katika viwanja vya bunge mjini Dodoma jana usiku.

Na Waandishi WetuHATUA ya wabunge wa Chadema kutoka nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma wakati Rais Jakaya Kikwete akianza kuhutubia, imetikisa nchi kutokana na wasomi, wanasiasa, viongozi wa dini na wananchi kuibuka na maoni tofauti.
Chadema wametangaza kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais wakidai kuwa kulikuwa na kasoro nyingi kwenye zoezi zima la uchaguzi na kwamba Tume ya Uchaguzi (Nec) ilikuwa imelenga kumbeba mgombea urais kutoka chama tawala.
Chadema, ambayo safari hii imeingiza watu wengi bungeni, imeamua kutumia njia hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais kushinikiza kuundwa kwa katiba mpya kutokana na katiba ya sasa kutotoa haki ya kupinga matokeo ya urais na inataka kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.
Katika mahojiano ambayo Mwananchi iliyafanya jana katika mikoa tofauti nchini lilibaini kuwa wapo wanaoona kitendo hicho kilikuwa halali wakieleza uamuzi huo unaweka bayana msimamo wao wa kutokubaliana na mfumo uliomweka madarakani Rais Jakaya Kikwete , huku wengine wakikosoa kwa kusema kwamba hawakustahili kufanya hivyo mbele ya rais, wakitafsiri kuwa huenda hizo ni chokochoko za kuvuruga amani na utulivu nchini.

Wasomi, wanazuoni wanaounga mkono
Mhadhri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abdallah Safari alisema kitendo hicho nio cha ni aibu kwa serikali ya Kikwete na Nec na kutaka kitafsiriwe kuwa ni kiashirio cha udhaifu katika uchaguzi na mahitaji ya tume hiyo.
"Ni silaha ya haki kwa kila mwanasiasa, ndio maana hata katika historia wabunge waliokuwa kwenye mabunge aliyokuwa akihutubia Fidel Kastro walikuwa wakitoka nje. La kujitakia halina majuto," alisema Profesa Safari.
Mhadhiri mwingine katika Chuo hicho, Dk Azaveli Lwaitama alisema kitendo cha Chadema cha kawaida kwa kuwa siasa huambatana na suala la kisheria na hisia.
"Wao wamesema kuwa hawamtambua, lakini tayari rais wetu ameshaapishwa, hivyo kinachowafanya waseme hivyo ni hisia tu. Wanataka kuwaonyesha Watanzania kuwa hawakubaliani na matokeo ya urais, lakini kisheria hawawezi kufanya lolote kwa kuwa sheria inawabana," alisema Dk Lwaitama.
Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Tumaini mkoani Kilimanjaro ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema hakuna kosa lolote kwa wabunge kutumia njia hiyo kuonyesha dhamira yao ya kutokubaliana na matokeo ya Urais kwa kuwa hawana njia nyingine.
"Ibara ya 41 Ibara ndogo ya 7 ya katiba yetu inakataza matokeo ya urais kuchunguzwa baada ya kutangazwa na Nec… sasa kama umemfunga mshindani wako mikono, afanyeje kukuonyesha hakubaliani nawe," alihoji.
"Katika hali ya kawaida ni jambo lisilowezekana kukubali goli ambalo unaamini limefungwa kwa mkono na kwamba hakuna mfumo unaomlazimisha mtu kumsikiliza Rais."
Alisema haiwezekani Tanzania kujisifu kwa maendeleo ya kidemokrasia wakati katiba inazuia watu kuhoji uhalali wa matokeo ya urais, lakini katiba hiyo inaruhusu watu kuhoji uhalali wa matokeo ya wabunge na madiwani.
"Senegal kuna mahakama ya katiba ambayo inataka baada ya matokeo ya uchaguzi wa rais kutangazwa, ni lazima yathibitishwe na Mahakama ya Kikatiba… kunakuwepo kipindi maalumu cha kushughulikia malalamiko kabla ya Rais kuapishwa," alisema.
Harod Tairo, mhadhiri wa sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema kitendo cha Chadema hakikumfurahisha kwa sababu kilijenga taswira ya mgawanyiko na machafuko bungeni.
"Mimi nashauri CCM wakae chini na Chadema wazungumze tatizo lilikuwa wapi ili kuziba mianya itakayoweza kuleta machafuko kama yaliyotokea Zanzibar," alisema Tairo na kuongeza kuwa kama serikali inataka kukuza demokrasia, ni lazima ikubali msimamo na kitendo kilichofanywa na Chadema.
Naye mhitimu wa shahada ya sheria wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Iringa, Clement Kihoko alisema kitendo hicho ni kabisa japokuwa wanaweza kueleweka tofauti.
"Ni utaalamu wa kifalsafa na ni mambo ya kuangalia kwa umakini zaidi kwa sababu kama walivyosema awali kwamba hawamtambui Kikwete kama rais ,wangebaki kumsikiliza bungeni wangeonyesha kumuunga mkono na kumkubali," alisema Kihoko.
Kihoko alibainisha kuwa katika tafsiri ya kifalsafa na hata falsafa ya sheria, kitendo walichokifanya chadema ni sahihi kabisa.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro (MUM), Ali Nassor alisema kitendo cha Chadema ni kuwaonyesha wananchi kwamba wako makini na wanatambua jukumu walilokabidhiwa na wananchi bungeni.
"Kwa kitendo hiki Chadema wanajiweka hadharani ili kupata wanachama wengi," alisema Nassor.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Dk Fairles Ilomo alielezea Chadema kuwa ni wapigania makabadiliko wachache waliojitoa kuwambwa msalabani kwa manufaa ya wananchi wengi.
Hata hivyo Dk Ilomo hakuunga mkono njia waliyotumia kupigania mabadiliko kwa kusema kuwa hawakupaswa kususia hotuba ya rais bali walipaswa kuwa wavumilivu na kutumia Bunge kufanya mabadiliko.
"Ni kitendo kilichoonyesha ujasiri kwa sababu kukiwa na viongozi ambao ni waoga watupu itachukua muda mrefu kufanya mabadiliko," alisema Dk ILomo.
"Hayati Baba wa taifa Julias Nyerere alipoanza kupigania uhuru wakoloni walisema ni mvurugaji wa amani na kumweka rumande kwa saa kadhaa, lakini sasa tunafaidi matunda ya uhuru aliopigania. Vivyo hivyo wananchi watakuja kufaidi matunda ya mgomo Chadema."
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) walisema kitendo cha wabunge wa Chadema kinastahili kupongezwa kwa kuwa wameonyesha kwa vitendo kuwa uchaguzi ulikuwa na dosari.
Wanafunzi hao ambao wapo Jijini Tanga kwa ajili ya mazoezi walisema wabunge hao hawakutaka kuwa wanafiki mbele ya Rais Kikwete na badala yake wakaonyesha kilichokuwa mioyoni mwao.
"Walichofanya ni kupaza sauti ili dunia ielewe kwamba kulikuwa na dosari kubwa katika zoezi zima la kutangaza matokeo na hilo linaegemea kwa upande wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi," alisema Saida Hamis mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo hicho.

Mawakili na Wanasheria
Mwanasheria wa Ngorongoro mkoani Arusha, Imanuel Saringe alisema: "Kisheria jambo hili halina tatizo na binafsi ninaaamini ujumbe wao umefika kwa walengwa bila vurugu au damu kumwagika."
Hata hivyo, alisema hutuba ya Rais Kikwete imekuwa ya ujumla sana na hivyo ni vigumu kuitathimini katika utekelezaji wa aliyosema.
Naye wakili mashuhuri mjini Moshi (jina limehifadhiwa) alisema kwa mtu mwenye mawazo finyu anaweza kusema kitendo cha Wabunge hao ni usanii fulani, lakini mtu upeo mpana atagundua Tanzania ina mgogoro wa kikatiba.
"Tuna tatizo la ubovu wa sheria nzima ya uchaguzi na kwa bahati nzuri sana wabunge hawa wameishia tu kutoka nje lakini tukiendelea na mfumo huu wa katiba unaokataza kuhoji matokeo ya rais, iko siku tutamwaga damu."
Alisema: "Tukiendelea na katiba hii tutajikuta tunakuwa na kiongozi aliyetangazwa kuwa ni rais, lakini si kiongozi aliyeshinda urais... kisheria anakuwa Ikulu, lakini kiuhalali hastahili na hapa ndipo mgogoro unapoanzia."

Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali
Mkurugenzi mtendaji wa wanaharakati wa Agenda 2000, Moses Malaba alisema kitendo kilichofanywa na Chadema, kimefikisha ujumbe uliokusudiwa.
"Kisiasa walichofanya Chadema ni sawa; wamefanikiwa kufikisha ujumbe wa kutoridhishwa na mchakato wa uchaguzi kama walivyokusudia," alisema Malaba lakini akaonyesha wasiwasi kama wananchi wataelewa lengo la chama hicho.
"Lakini wameenda mbali sana... wanachotaka wananchi waliowachangua ni kupata uwakilishi bungeni. Kwa sasa wanataka kujivunia kuwa na wabunge wengi."
Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Karanga wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Fred Njama alisema haoni kosa lolote kwa wabunge hao kufanya kitendo hicho.
"Kwa maoni yangu walichokifanya ni sahihi kwa sababu usipokubaliana na mtu huwezi kumsikiliza... ni vizuri hisia zako usizifanye ni siri ni vizuri ukazionyesha badala ya unafiki; mimi sioni tatizo hapa," alisema.

Vyama vya siasa
Aliyekuwa mgombea urais wa TLP, Mutamwega Mugahwa alisema kitendo cha Chadema kinampasa Rais Kikwete kukaa chini na kutafakari tatizo lililopo na kulipatia ufumbuzi.
"Ningekuwa mimi ndio nimesusiwa Bunge, kiukweli nisingeweza kuchukulia kirahisi; lazima ningekaa na wahusika na kujua tatizo lililopo na kutafuta njia ya kulitatua kwa mujibu wa sheria za nchi," alisema Mugahwa.
Alisema kwa mujibu wa katiba mtu ana uhuru wa kusikiliza na kutosikiliza ili mradi tu katika maamuzi yake asiingilie uhuru wa mtu mwingine.
Muasisi wa Chadema, Edwin Mtei alisema kitendo hicho binafsi kimempa faraja na kwamba huo ni mwendelezo wa kupinga katiba na kutaka ibadilishwe.
Mtei ambaye pia aliwahi kuwa gavana wa Benki Kuu nchini pia alimuunga mkono mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini, Jaji Amir Manento kuwa sasa ni muda wa kulilia katiba mpya.

Wananchi na makundi mengine
Mkoa wa Iringa
Baadhi ya wananchi wamewapongeza wabunge wa Chadema kwa hatua yao wakieleza kuwa msimamo huo unaweza kumfanya rais ajue kwamba wapo Watanzania wengi ambao hawana imani na utendaji kazi wa Nec.
Walisema Chadema wangeweza kuitisha maandamano na kufanya fujo kama ilivyowahi kutokea nchini Kenya, lakini kwa busara wametumia njia ya kususia hotuba kuonyesha kuwa hawamtambui rais kama alivyotamka katibu mkuu wa Chadema, Dr Willibrod Slaa.
Enock Mwasondole ambaye ni mkazi wa Mtwivila alisema umefika wakati ambao Nec inapaswa kuwa huru ili malalamiko yatokanayo na uchaguzi yapungue.
"Ni bora kususia kuliko wangeitisha mgomo na maandamano makubwa kama yaliyotokea Kenya. Rais asipuuzie hali ile badala yake anapaswa kuhakikisha Tume ya Uchaguzi inakuwa huru na kutenda haki," alisema Mwasondole.
Mkazi mwingine wa Gangiolonga, Anania Mlelwa alisema huu ni wakati wa Tanzania kubadilisha katiba ambayo Iliandaliwa wakati wa chama kimoja na hivyo kusababisha tume hiyo kuwa mikononi mwa rais ambaye ni mwanachama wa chama kimoja.
"Katiba ndiyo tatizo kubwa; kama katiba ingelingana na wakati wa vyama vingi, tume isingekuwa ikilalamikiwa kwa kuwa isingekuwa chini ya rais," alisema.
Naye rais wa Muungano wa Vyama vya Waandishi wa Habari, Keneth Simbaya alisema suala hilo ni la kiitikadi zaidi la kwamba wabunge hao wanapaswa kusikilizwa kwa kuwa yawezekana wana madai sahihi,
"Mara nyingi tuhuma za wanasiasa zinatakiwa kuangaliwa pande mbili kwa kuwa upande mmoja inaweza kuwa ni kweli na kwa upande wa pili inaweza kuwa si kweli, hivyo wabunge hao wasikilizwe ili kubaini wanachokilalamikia," alisema mwanahabari huyo.

Mkoa wa Mwanza
Uamuzi wa Chadema pia uliungwa mkono mkoani Mwanza ambako walisema unalenga kurejesha thamani ya kura.
Yohana Kagenzi, mkazi wa jijini Mwanza, alisema Chadema wameanzisha njia ya amani na ya kiungwana ya kudai katiba na tume huru ya uchaguzi ambayo haiwezi kusababisha umwagaji wa damu na kuzusha vurugu.
"Walisema kuwa hawayatambui matokeo, lakini serikali iliona ni jambo la kawaida nadhani njia hii sasa itamkera rais na kuamua kuwasikiliza. Kama hakuchakachua kura kwa nini asisikilize malalamiko yao," alihoji Kagenzi.
Mkazi mwingine, Saida Mbwana alisema kitendo hicho kisipuuzwe kwa kuwa kinaweza kuwa na athari kubwa.
"Kama hawamtambua Rais Kikwete, basi hata serikali atakayoiunda hawataitambua, jambo ambalo litawakosesha maendeleo katika majimbo," alisema.

Mkoa wa Arusha
Arnold Kamde, Gervas Mgonja pamoja na Prosper Mfinanga ambao ni wakazi wa Arusha walidai ya kuwa kitendo hicho si tu kwamba kimeonyesha dalili za kukua kwa demokrasia nchini, bali pia kinatoa ujumbe kwa serikali ya Rais Kikwete kuwa Chadema hawakubaliani na matokeo ya urais kwa kuwa yalichakachuliwa.
"Sheria ya nchi inasema kuwa mara matokeo ya urais yakishatangazwa, hakuna mtu wa kuyapinga mahakamani. Sasa hiki kitendo si tu kwamba kinaonyesha kukua kwa hali ya demokrasia nchini bali pia ni ujumbe tosha kwa serikali ya Kikwete," alisema Mgonja.
Mfanyabiashara John Lyimo wa soko kuu la Arusha alipongeza wapinzani kwa kuonyesha hasira zao za kupinga matokeo na pia alimpongeza Rais Kikwete kwa kutoa hutuba nzuri.
"Mimi sina chama ila naona Chadema wamefanya vizuri tu na wamefanikiwa kufikisha ujumbe... rais aliongea vizuri na ameonyesha ameupata ujumbe," alisema Lyimo.
Mkoa wa Mbeya
Watu wengi walioongea na Mwananchi mkoani Mbeya waliunga mkono kitendo cha Chadema wakisema ujumbe waliotaka kumfikishia rais ulifika.
"Chadema wana ujumbe ambao wamewasilisha kwa serikali ya Rais Kikwete na ni haki yao kufanya hivyo," alisema Jeremiah Osward ambaye ni mkazi wa Vwawa wilayani Mbozi.
"Kutokana na tamko lao la kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais, isingekuwa ni rahisi kwao kumsikiliza."
Mkazi wa Mwanjelwa, Zawadi Pangani alisema wabunge hao walikuwa sahihi kwa kuwa wanajua wanachokifanya ni kwa ajili ya maslahi ya wananchi na kwamba bila kufanya hivyo, haki haitaweza kupatikana.
Alisema inawezekana Chadema wana uhakika kuwa mgombea wao wa urais, Dk Slaa alishinda, lakini matokeo yakatangazwa kuwa ameshindwa, hivyo wana haki ya haki yao kufanya hivyo.

Mkoa wa Morogoro
Mmoja wa wakazi wa Morogoro, Anthony Chalamila alisema tukio hilo lilitarajiwa kwa sababu mgombea wao alitamka wazi kuwa hakubaliani na matokeo yaliyomtangaza Kikwete kuwa rais kwa madai yana walakin.
"Ni lazmima wasimamie na kuyatetea maamuzi yao, hivyo haingewezekani mtu ambaye walisema hawamtambui, wakae kumsikiliza," alisema.
"Kama wangekubali kukaa na kumsikiliza rais akihutubia, ingeonyesha wazi kuwa hawana msimamo."
Mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Naye Simon alisema ni haki yao kufanya hivyo kwa kuwa walishatoa sababu za msingi za kutomtambua rais.

Wanaopinga kitendo cha Chadema
Wasomi na wanazuoni
Mbali na wengi kuunga mkono kitendo hicho, wapo ambao wanakipinga wakiongozwa na kiongozi wa zamani wa waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Profesa Ernest Wamba dia Wamba ambaye alisema si cha kiungwana.
Akizungumza katika mkutano wa wanafalsafa ulioandaliwa na Chama wa Falsafa Tanzania (Phata) uliofanyika jijini Dar es Salaam, Wamba alisema ni vizuri kama chama hicho kingekubaliana na matokeo hayo.
"Kawaida katika siasa changamoto ni jambo la kawaida, lakini kwa jinsi ulivyoniuliza kuhusu uchaguzi wa hapa Tanzania ni kweli umefanyika na mshindi kapatikana, lakini ingekuwa vizuri kama walioshindwa wangekubali tu matokeo," alisema Profesa Wamba.
"Wabunge wameshakula kiapo, lakini wanasema hawatambui ushindi wa rais. Wana haki ya kuzungumza kwa kuwa hiyo ndio maana ya falsafa, lakini kwa hili la kiapo litawabana. Wangekubaliana na matokeo."

Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali......
Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) limeelezea kutofurahshwa na kitendo kilichofanywa na Chadema na kukitaka kutafuta njia mbadala ya kutoa dukuduku lao.
Katibu wa TEC, Padri Antony Mkunde alisema vyama vya siasa na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kutambua kuwa amani iliyopo haikushuka kutoka mahali popote bali ni mshikamano na busara katika uongozi.
"Mahali penye vurugu hata viongozi wa dini hawawezi kuhubiri; kinachotakiwa ni busara za viongozi wa nchi katika kuhakikisha amani na utulivu vinakuwapo," alisema Makunde.
Kwa upande wake Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISATAN) imekielezea kitendo cha Chadema kuwa ni utovu wa nidhamu.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Rose Haji alisema viongozi wa Chadema ni kati ya viongozi waliokula kiapo walipoapishwa hivyo wasingepaswa kususia hotuba ya rais.
"Chadema wanatakiwa kumheshimu rais kama baba mzazi kwa sababu baba anapokosea huwezi kumdhalilisha mbele ya kadamnasi hivyo heshima inatakiwa pia katika suala la uongozi," alisema Haji.
Naye mwenyekiti wa taasisi ya kiislamu ya Imam Bukhary, Sheikh Khaliha Khamis alisema uamuzi wa Chadema utasababisha chuki dhidi ya chama hicho na wananchi waliowachagua.
Alisema kitendo hicho kinaonyesha dhahiri kuwa chama hicho hakiko tayari kukubali misingi ya demokrasia nchini na kuwatumikia wananchi.
Vyama vya siasa....
CCM imewataka wabunge wote waliokiri kutomtambua rais kujitoa haraka bungeni vinginevyo wataondolewa na azimio la bunge hadi watakapotambua uwepo wa rais.
Katibu wa kamati kuu ya CCM, John Chiligati alisema kuwa kila mbunge amekula kiapo cha kutii na kulinda katiba na kitendo cha kutomtambua rais ni uvunjaji wa katiba na hivyo wabunge hao wanatakiwa kujiondoa bungeni.
Chiligati alisema kitendo cha Chadema kuruhusu wabunge na madiwani wake kuendelea na kazi wakati hawamtambui rais na serikali ni unafiki wa hali ya juu.
Chiligati aliwataka wananchi kukataa tabia za viongozi wanaokataa matokeo kwa kuwa ni tabia inayoweza kusababisha matatizo na kuchochea vurugu nchini.
Katibu mwenezi wa NCCR-Mageuzi, David Kafulila alisema kitendo hicho hakikuwa cha kiungwana huku akikielezea kuwa ni sanaa ya maigizo.

Wananchi na makundi mengine
Mkoa wa Kagera

Aliyewahi kuwa waziri kwa nyakati tofauti katika awamu ya kwanza na pili Balozi Joseph Rwegasira amewaponda wabunge wa Chadema kwa kususia hotuba hiyo.
Mwanasiasa huyo alisema kitendo hicho kilikosa hekima kwa madai kuwa hawakujua sheria na taratibu.
Balozi Rwegasira, ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge, alisema rais hawezi kususiwa na wabunge kwa kuwa kwa mujibu wa taratibu hata yeye ni sehemu ya Bunge na kuhoji iweje wasisusie Bunge zima.
Mkoa wa Kilimanjaro
Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashar Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoani Kilimanjaro, Patrick Boisafi alisema kilichofanywa na wabunge hao wa Chadema hakikuwa cha uungwana na si mfano mzuri wa kuigwa.
"Kama hawataki kutambua matokeo yaliyompa Kikwete urais ina maana kwa miaka yote mitano hakuna siku watashiriki kutunga sheria Bungeni kwa sababu ni lazima mwisho wa siku iidhinishwe na Rais wanayemkataa," alisema.
Alisema anachokiona ni ubinafsi wa Chadema kwamba kionekane ndicho chama kikuu cha upinzani nchini kama ilivyo CUF kwa Zanzibar ili siku za usoni wapate nafasi ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Bendera Isinika, ambaye mkazi wa Kaloleni anayefanya kazi ya uchoraji, alipinga kitendo cha wabunge wa Chadema kususia hotoba ya Rais Kikwete kwa madai kuwa hawakuwatendea haki wananchi waliowachagua kwa kuwa walipaswa kuwashirikisha kwanza kabla ya kufanya tukio hilo.
"Kama kuna tatizo la uchakachuaji wa kura wao walipaswa kutumia njia bora na sio kususia hotuba ya Rais Kikwete kwa kuwa wao tumewachagua sisi hivyo wangetuambia kwanza kama wanataka kutoka nje ya Bunge na si kuchukua maamuzi yao," alisema Isinika.

Mkoa wa Mbeya
Mkazi wa wilayani Mbozi, Imelda Ngarawa alisema kuwa hayo ndiyo matokeo ya upinzani kwa kuwa wanafikiri bungeni ni mahali pa kufanya sanaa, hivyo wameenda huko si kwa ajili ya kuwatetea wananchi bali kufanya sanaa.
Naye mkazi wa Tukuyu wilayani Rungwe, Fadhili Sikumoja alisema kuwa wabunge hao hawajafanya vizuri kwani rais Kikwetye bado ni rais wao kwani yupo madarakani na kwamba ilikuwa vizuri wangemsikiliza hotuba yake na kama wanahopja za msingi wangewasilisha wakati wa bunge lijalo.

Mkoa wa Morogoro
Mkazi wa Morogoro Leonard Mtete alisema kuwa hatua iliyoonyeshwa na wabunge wa chama cha Chadema haikuwa nzuri kwa vile inaweza kuwashushia umaarufu ulioanza kujijenga katika chama hicho.
Alisema kuwa hali hiyo pia inaweza kuionyesha jamii kuwa chama hicho ni chama cha washari na wagomvi tofauti na jinsi ambavyo watu walinavyokichukulia kuwa mapambano yake ni kidemokrasia na ya amani.
"Mimi nafikiri wabunge wa chadema wangetumia fursa waliyonayo bungeni kupambana kwa hoja na siyo kutoka kama walivyofanya wao" alisema mkazi huyo wa Morogoro.

Mkoa wa Iringa
Mkazi wa Iringa, Fanuel Kagambo alisema haoni kama msimamo huo unaweza kuwa na manufaa zaidi ya kuwaumiza Chadema na akawashauri kuanzisha njia nyingine ya kudai madai yao kwa vile kumkataa rais na kushiriki kupiga kura za kumthibitisha waziri mkuu aliyeteuliwa naye kuonaonyesha kumtambua.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe anasemaje...
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu jana, Mbowe alisema wanaowapinga au kuwa na mawazo tofauti na uamuzi huo, wasilitazame suala hilo juu juu na badala yake waangalia hoja wanazozitoa.
Alisema Chadema haikuamka tu na kutangaza kutomtambua rais, bali inazo sababu za msingi ambazo imeziweka bayana na imekuwa ikizieleza kila kukicha na kulaumu vyombo vya habari vinavyoshindwa kuainisha malalamiko au hoja zao kwa wananchi.
Mbowe alisema, msingi wa madai na malalamiko ya Chadema ni kutaka mazingira mazuri katika chaguzi zijazo wananchi wapate viongozi waliowachagua.
"Harakati ni kitu endelevu, michakato huzaa tunda la haki, miaka 19 sasa tangu siasa za vyama vingi ziruhusiwe, kumekuwa na vilio vingi toka kambi ya upinzani na kwa wananchi, lakini wenzetu walioko madarakani hawaonekani kusikia, tunatafuta lugha mbadala baada ya lugha ya upole kusikia" alisema.
Alisema, jambo wanalopigia kelele sio kilio cha Chadema pekee, bali ni kilio cha watanzania wote na akasema wanachofanya ni kutengeneza mazingira mazuri ya uchaguzi wa mwaka 2015.
"Yapo matatizo ya msingi na ni lazima yafanyike mabadiliko ya haraka na ya msingi, kwanza ni suala la katiba, tutahitaji kuangalia katiba kama chombo muhimu kinachoweza kumkomboa mtanzania na kupunguza vilio vya watu wengi" anasema.
Akizungumza kwanini wanayakubali matokeo ya wabunge na kuyakataa yale ya rais, Mbowe anasema, "Hili ni muhimu likawa wazi, sheria iko wazi kabisa, kwamba Rais akishatangazwa na Tume ya Uchaguzi hakuna anayeweza kubadilisha wala kwenda mahakamani, lakini ukiwa huridhiki na ushindi kwa wabunge au madiwani, sheria inaruhusu kwenda mahakamani kupinga" anasema.
Anasema, kutokana na sheria hizo ambazo anasema ni miongoni mwa mambo wanayoyapigia kelele wameamua kutumia njia hiyo ya kutomtambua rais ikiwa ni katika hatarakati za kutaka marekebisho katika sheria kandamizi kama hiyo ya kutokuwa na haki ya kupinga endapo wagombea wengine watakuwa hawajaridhishwa na ushindi wa mgombea mwingine.
Hata hivyo Mbowe alisema, Chadema inatambua kuwa kwa kufanya hivyo hakuwezi kubadilisha matokeo na hakuwezi kuzuia Kikwete kuwa rais au kuongoza serikali isipokuwa kwa kufanya hivyo kutafikisha ujumbe wao kwake Kikwete na serikali yake pamoja na dunia nzima.

Habari hii imeandaliwa na Joyce Mmasi, Nora Damian, Tumsifu Sanga, Fidelis Butahe, Hussein Kauli, Minael Msuya, Fredy Azzah, Michael Matemanga, Petro Tumaini, Hussein Issa, Aziza Masoud, Hidaya omary, Burhani Yakub,Tanga, Daniel Mjema, Moshi, Moses Mashalla na Mussa Juma,Arusha, Brandy Nelson, Mbeya, Tumaini Msowoya na Habel Chidawali,Iringa,Venance George, Morogoro, Phinias Bashaya,Bukoba, Geroda Mabumo na Masoud Masasi Dodoma na Frederick Katulanda, Mwanza.

Chanzo: Mwananchi
 
Mkuuu nunua gazeti usome na habari zingine kuliko kudulufu kwny net ya mwananchi je unawazo jipya ?.copy na pest
 
Na Waandishi Wetu
HATUA ya wabunge wa Chadema kutoka nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma wakati Rais Jakaya Kikwete akianza kuhutubia, imetikisa nchi kutokana na wasomi, wanasiasa, viongozi wa dini na wananchi kuibuka na maoni tofauti.
Chadema wametangaza kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais wakidai kuwa kulikuwa na kasoro nyingi kwenye zoezi zima la uchaguzi na kwamba Tume ya Uchaguzi (Nec) ilikuwa imelenga kumbeba mgombea urais kutoka chama tawala.
Chadema, ambayo safari hii imeingiza watu wengi bungeni, imeamua kutumia njia hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais kushinikiza kuundwa kwa katiba mpya kutokana na katiba ya sasa kutotoa haki ya kupinga matokeo ya urais na inataka kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.
Katika mahojiano ambayo Mwa

bungekikwetemno.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Maswa Magharibi kupitia CHADEMA, John Shibuda wakati wa hafla ya kuwapongeza wabunge iliyofanyika katika viwanja vya bunge mjini Dodoma jana usiku.

nanchi iliyafanya jana katika mikoa tofauti nchini lilibaini kuwa wapo wanaoona kitendo hicho kilikuwa halali wakieleza uamuzi huo unaweka bayana msimamo wao wa kutokubaliana na mfumo uliomweka madarakani Rais Jakaya Kikwete , huku wengine wakikosoa kwa kusema kwamba hawakustahili kufanya hivyo mbele ya rais, wakitafsiri kuwa huenda hizo ni chokochoko za kuvuruga amani na utulivu nchini.

Hii inaonyesha nchi yetu imegawanyika sana kwa sasa, hata hivyo jambo moja ni wazi hapa wale wanaounga mkono wabunge kususia hotuba ya raisi wanazo sababu za msingi sana kama ubovu wa katiba, thamani ya kura, sheria mbovu n.k. Kundi la pili la wanopinga sijaona hoja za msingi, wengi wanasema sio ustaarabu, mara ni viashirio vya fujo n.k. Mimi naona kundi hili ndilo la watu waoga na wenye fikra hasi na ndio hawa wamechangia kurudisha nyuma maendeleo yetu.

Pia kuna post ya tamko la wasomi wa UDOM ambayo nimeshangaa kuona kuwa hapa kwenye hii habari wanafunzi wa UDOM wameunga mkono kitendo cha kutoka nje. Ile post lazima imetoka kwa fisadi kama ilivyodhaniwa mwanzo na wenzetu.
 
Mkuuu nunua gazeti usome na habari zingine kuliko kudulufu kwny net ya mwananchi je unawazo jipya ?.copy na pest

Comment on the topic bana umbea mwingine uache. Yani wewe ulichoona cha kutuambia ni kuwamtu anunue gazeti? kweli watu wengine siwaelewi kabisa.
 
nashangaa sana CUF pamoja na kuungwa mkono na umma wa watanzania ,...kwenye hili la kudai katiba mpya na uhuru wa tume wanashindwa kuliona....

ndio maana tunafika mbali kuona kuwa wameinajisi nchi kwa madume mazima yenye sharubu kukubali kuolewa na CCM wasio na ndevu...

Tukiwa Jeshini Tulikuwa na wimbo wa uhamasishaji ukiimbwa hivi,..nadhani jakaya anaukumbuka.....

AMIN....AAAH AHAAA ..
AMINI..
AMEOLEWA ..NA NANI AAHAA AHAA NA NANI NA MWINGEREZA ..
WAPI? AHAAA AHAAA WAPI ..HUKO ULAYA...

SASA TUTAIMBA .....

CUF AHAA AHAA CUF WAMEOLEWA
NA NANI??
AHAA AHAA NA NANI NA CCM
WAPI ..AHAA AHAA WAPI?
HUKO DODOMA!!!!
 
Hahahahahahaha CUF ahaaha CUF wameolewa ....... safiii nitaimba kila siku kabla na saa ya kula
 
BOOKMARK THIS PAGE
Chadema 'yaitikisa' nchi :NI
KUTOKANA NA WABUNGE WAKE
KUSUSIA HOTUBA YA JK
Send to a friend
Saturday, 20 November 2010 07:11
0
digg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na Mbunge wa Maswa
Magharibi kupitia CHADEMA, John
Shibuda wakati wa hafla ya
kuwapongeza wabunge iliyofanyika
katika viwanja vya bunge mjini
Dodoma jana usiku.
Na Waandishi Wetu
HATUA ya wabunge wa Chadema
kutoka nje ya ukumbi wa bunge mjini
Dodoma wakati Rais Jakaya Kikwete
akianza kuhutubia, imetikisa nchi
kutokana na wasomi, wanasiasa,
viongozi wa dini na wananchi kuibuka
na maoni tofauti.
Chadema wametangaza kupinga
matokeo ya uchaguzi wa rais wakidai
kuwa kulikuwa na kasoro nyingi
kwenye zoezi zima la uchaguzi na
kwamba Tume ya Uchaguzi (Nec)
ilikuwa imelenga kumbeba mgombea
urais kutoka chama tawala.
Chadema, ambayo safari hii imeingiza
watu wengi bungeni, imeamua
kutumia njia hiyo ya kupinga matokeo
ya uchaguzi wa rais kushinikiza
kuundwa kwa katiba mpya kutokana
na katiba ya sasa kutotoa haki ya
kupinga matokeo ya urais na inataka
kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.
Katika mahojiano ambayo Mwananchi
iliyafanya jana katika mikoa tofauti
nchini lilibaini kuwa wapo wanaoona
kitendo hicho kilikuwa halali
wakieleza uamuzi huo unaweka
bayana msimamo wao wa
kutokubaliana na mfumo uliomweka
madarakani Rais Jakaya Kikwete , huku
wengine wakikosoa kwa kusema
kwamba hawakustahili kufanya hivyo
mbele ya rais, wakitafsiri kuwa huenda
hizo ni chokochoko za kuvuruga amani
na utulivu nchini.
Wasomi, wanazuoni wanaounga
mkono
Mhadhri wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Profesa Abdallah Safari
alisema kitendo hicho nio cha ni aibu
kwa serikali ya Kikwete na Nec na
kutaka kitafsiriwe kuwa ni kiashirio
cha udhaifu katika uchaguzi na
mahitaji ya tume hiyo.
“Ni silaha ya haki kwa kila mwanasiasa,
ndio maana hata katika historia
wabunge waliokuwa kwenye
mabunge aliyokuwa akihutubia Fidel
Kastro walikuwa wakitoka nje. La
kujitakia halina majuto, ” alisema
Profesa Safari.
Mhadhiri mwingine katika Chuo hicho,
Dk Azaveli Lwaitama alisema kitendo
cha Chadema cha kawaida kwa kuwa
siasa huambatana na suala la kisheria
na hisia.
“Wao wamesema kuwa
hawamtambua, lakini tayari rais wetu
ameshaapishwa, hivyo
kinachowafanya waseme hivyo ni hisia
tu. Wanataka kuwaonyesha
Watanzania kuwa hawakubaliani na
matokeo ya urais, lakini kisheria
hawawezi kufanya lolote kwa kuwa
sheria inawabana, ” alisema Dk
Lwaitama.
Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu
cha Tumaini mkoani Kilimanjaro
ambaye aliomba jina lake lisitajwe
gazetini alisema hakuna kosa lolote
kwa wabunge kutumia njia hiyo
kuonyesha dhamira yao ya
kutokubaliana na matokeo ya Urais
kwa kuwa hawana njia nyingine.
“Ibara ya 41 Ibara ndogo ya 7 ya katiba
yetu inakataza matokeo ya urais
kuchunguzwa baada ya kutangazwa na
Nec … sasa kama umemfunga
mshindani wako mikono, afanyeje
kukuonyesha hakubaliani nawe, ”
alihoji.
"Katika hali ya kawaida ni jambo
lisilowezekana kukubali goli ambalo
unaamini limefungwa kwa mkono na
kwamba hakuna mfumo
unaomlazimisha mtu kumsikiliza Rais.”
Alisema haiwezekani Tanzania kujisifu
kwa maendeleo ya kidemokrasia
wakati katiba inazuia watu kuhoji
uhalali wa matokeo ya urais, lakini
katiba hiyo inaruhusu watu kuhoji
uhalali wa matokeo ya wabunge na
madiwani.
“Senegal kuna mahakama ya katiba
ambayo inataka baada ya matokeo ya
uchaguzi wa rais kutangazwa, ni
lazima yathibitishwe na Mahakama ya
Kikatiba … kunakuwepo kipindi
maalumu cha kushughulikia
malalamiko kabla ya Rais kuapishwa,”
alisema.
Harod Tairo, mhadhiri wa sheria wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema
kitendo cha Chadema
hakikumfurahisha kwa sababu
kilijenga taswira ya mgawanyiko na
machafuko bungeni.
“Mimi nashauri CCM wakae chini na
Chadema wazungumze tatizo lilikuwa
wapi ili kuziba mianya itakayoweza
kuleta machafuko kama yaliyotokea
Zanzibar, ” alisema Tairo na kuongeza
kuwa kama serikali inataka kukuza
demokrasia, ni lazima ikubali
msimamo na kitendo kilichofanywa na
Chadema.
Naye mhitimu wa shahada ya sheria
wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Iringa,
Clement Kihoko alisema kitendo hicho
ni kabisa japokuwa wanaweza
kueleweka tofauti.
“Ni utaalamu wa kifalsafa na ni mambo
ya kuangalia kwa umakini zaidi kwa
sababu kama walivyosema awali
kwamba hawamtambui Kikwete kama
rais ,wangebaki kumsikiliza bungeni
wangeonyesha kumuunga mkono na
kumkubali, ” alisema Kihoko.
Kihoko alibainisha kuwa katika tafsiri
ya kifalsafa na hata falsafa ya sheria,
kitendo walichokifanya chadema ni
sahihi kabisa.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kiislamu
cha Morogoro (MUM), Ali Nassor alisema
kitendo cha Chadema ni kuwaonyesha
wananchi kwamba wako makini na
wanatambua jukumu walilokabidhiwa
na wananchi bungeni.
“Kwa kitendo hiki Chadema
wanajiweka hadharani ili kupata
wanachama wengi, ” alisema Nassor.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini,
Dk Fairles Ilomo alielezea Chadema
kuwa ni wapigania makabadiliko
wachache waliojitoa kuwambwa
msalabani kwa manufaa ya wananchi
wengi.
Hata hivyo Dk Ilomo hakuunga mkono
njia waliyotumia kupigania mabadiliko
kwa kusema kuwa hawakupaswa
kususia hotuba ya rais bali walipaswa
kuwa wavumilivu na kutumia Bunge
kufanya mabadiliko.
“Ni kitendo kilichoonyesha ujasiri kwa
sababu kukiwa na viongozi ambao ni
waoga watupu itachukua muda mrefu
kufanya mabadiliko, ” alisema Dk
ILomo.
“Hayati Baba wa taifa Julias Nyerere
alipoanza kupigania uhuru wakoloni
walisema ni mvurugaji wa amani na
kumweka rumande kwa saa kadhaa,
lakini sasa tunafaidi matunda ya uhuru
aliopigania. Vivyo hivyo wananchi
watakuja kufaidi matunda ya mgomo
Chadema."
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma
(UDOM) walisema kitendo cha
wabunge wa Chadema kinastahili
kupongezwa kwa kuwa wameonyesha
kwa vitendo kuwa uchaguzi ulikuwa
na dosari.
Wanafunzi hao ambao wapo Jijini
Tanga kwa ajili ya mazoezi walisema
wabunge hao hawakutaka kuwa
wanafiki mbele ya Rais Kikwete na
badala yake wakaonyesha kilichokuwa
mioyoni mwao.
“Walichofanya ni kupaza sauti ili dunia
ielewe kwamba kulikuwa na dosari
kubwa katika zoezi zima la kutangaza
matokeo na hilo linaegemea kwa
upande wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, ” alisema Saida Hamis
mwanafunzi wa mwaka wa kwanza
katika chuo hicho.
Mawakili na Wanasheria
Mwanasheria wa Ngorongoro mkoani
Arusha, Imanuel Saringe alisema:
"Kisheria jambo hili halina tatizo na
binafsi ninaaamini ujumbe wao
umefika kwa walengwa bila vurugu au
damu kumwagika."
Hata hivyo, alisema hutuba ya Rais
Kikwete imekuwa ya ujumla sana na
hivyo ni vigumu kuitathimini katika
utekelezaji wa aliyosema.
Naye wakili mashuhuri mjini Moshi
(jina limehifadhiwa) alisema kwa mtu
mwenye mawazo finyu anaweza
kusema kitendo cha Wabunge hao ni
usanii fulani, lakini mtu upeo mpana
atagundua Tanzania ina mgogoro wa
kikatiba.
“Tuna tatizo la ubovu wa sheria nzima
ya uchaguzi na kwa bahati nzuri sana
wabunge hawa wameishia tu kutoka
nje lakini tukiendelea na mfumo huu
wa katiba unaokataza kuhoji matokeo
ya rais, iko siku tutamwaga damu. ”
Alisema: ”Tukiendelea na katiba hii
tutajikuta tunakuwa na kiongozi
aliyetangazwa kuwa ni rais, lakini si
kiongozi aliyeshinda urais... kisheria
anakuwa Ikulu, lakini kiuhalali
hastahili na hapa ndipo mgogoro
unapoanzia. ”
Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali
Mkurugenzi mtendaji wa wanaharakati
wa Agenda 2000, Moses Malaba
alisema kitendo kilichofanywa na
Chadema, kimefikisha ujumbe
uliokusudiwa.
“Kisiasa walichofanya Chadema ni
sawa; wamefanikiwa kufikisha ujumbe
wa kutoridhishwa na mchakato wa
uchaguzi kama walivyokusudia, ”
alisema Malaba lakini akaonyesha
wasiwasi kama wananchi wataelewa
lengo la chama hicho.
“Lakini wameenda mbali sana...
wanachotaka wananchi
waliowachangua ni kupata uwakilishi
bungeni. Kwa sasa wanataka kujivunia
kuwa na wabunge wengi. ”
Mchungaji kiongozi wa Usharika wa
Karanga wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT), Fred Njama
alisema haoni kosa lolote kwa
wabunge hao kufanya kitendo hicho.
“Kwa maoni yangu walichokifanya ni
sahihi kwa sababu usipokubaliana na
mtu huwezi kumsikiliza... ni vizuri hisia
zako usizifanye ni siri ni vizuri
ukazionyesha badala ya unafiki; mimi
sioni tatizo hapa, ” alisema.
Vyama vya siasa
Aliyekuwa mgombea urais wa TLP,
Mutamwega Mugahwa alisema kitendo
cha Chadema kinampasa Rais Kikwete
kukaa chini na kutafakari tatizo lililopo
na kulipatia ufumbuzi.
“Ningekuwa mimi ndio nimesusiwa
Bunge, kiukweli nisingeweza
kuchukulia kirahisi; lazima ningekaa na
wahusika na kujua tatizo lililopo na
kutafuta njia ya kulitatua kwa mujibu
wa sheria za nchi, ” alisema Mugahwa.
Alisema kwa mujibu wa katiba mtu
ana uhuru wa kusikiliza na kutosikiliza
ili mradi tu katika maamuzi yake
asiingilie uhuru wa mtu mwingine.
Muasisi wa Chadema, Edwin Mtei
alisema kitendo hicho binafsi kimempa
faraja na kwamba huo ni mwendelezo
wa kupinga katiba na kutaka
ibadilishwe.
Mtei ambaye pia aliwahi kuwa gavana
wa Benki Kuu nchini pia alimuunga
mkono mwenyekiti wa Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora nchini,
Jaji Amir Manento kuwa sasa ni muda
wa kulilia katiba mpya.
Wananchi na makundi mengine
Mkoa wa Iringa
Baadhi ya wananchi wamewapongeza
wabunge wa Chadema kwa hatua yao
wakieleza kuwa msimamo huo
unaweza kumfanya rais ajue kwamba
wapo Watanzania wengi ambao
hawana imani na utendaji kazi wa Nec.
Walisema Chadema wangeweza
kuitisha maandamano na kufanya fujo
kama ilivyowahi kutokea nchini Kenya,
lakini kwa busara wametumia njia ya
kususia hotuba kuonyesha kuwa
hawamtambui rais kama alivyotamka
katibu mkuu wa Chadema, Dr Willibrod
Slaa.
Enock Mwasondole ambaye ni mkazi
wa Mtwivila alisema umefika wakati
ambao Nec inapaswa kuwa huru ili
malalamiko yatokanayo na uchaguzi
yapungue.
“Ni bora kususia kuliko wangeitisha
mgomo na maandamano makubwa
kama yaliyotokea Kenya. Rais
asipuuzie hali ile badala yake
anapaswa kuhakikisha Tume ya
Uchaguzi inakuwa huru na kutenda
haki, ” alisema Mwasondole.
Mkazi mwingine wa Gangiolonga,
Anania Mlelwa alisema huu ni wakati
wa Tanzania kubadilisha katiba
ambayo Iliandaliwa wakati wa chama
kimoja na hivyo kusababisha tume
hiyo kuwa mikononi mwa rais ambaye
ni mwanachama wa chama kimoja.
“Katiba ndiyo tatizo kubwa; kama
katiba ingelingana na wakati wa
vyama vingi, tume isingekuwa
ikilalamikiwa kwa kuwa isingekuwa
chini ya rais, ” alisema.
Naye rais wa Muungano wa Vyama vya
Waandishi wa Habari, Keneth Simbaya
alisema suala hilo ni la kiitikadi zaidi la
kwamba wabunge hao wanapaswa
kusikilizwa kwa kuwa yawezekana
wana madai sahihi,
"Mara nyingi tuhuma za wanasiasa
zinatakiwa kuangaliwa pande mbili
kwa kuwa upande mmoja inaweza
kuwa ni kweli na kwa upande wa pili
inaweza kuwa si kweli, hivyo
wabunge hao wasikilizwe ili kubaini
wanachokilalamikia," alisema
mwanahabari huyo.
Mkoa wa Mwanza
Uamuzi wa Chadema pia uliungwa
mkono mkoani Mwanza ambako
walisema unalenga kurejesha thamani
ya kura.
Yohana Kagenzi, mkazi wa jijini
Mwanza, alisema Chadema
wameanzisha njia ya amani na ya
kiungwana ya kudai katiba na tume
huru ya uchaguzi ambayo haiwezi
kusababisha umwagaji wa damu na
kuzusha vurugu.
“Walisema kuwa hawayatambui
matokeo, lakini serikali iliona ni jambo
la kawaida nadhani njia hii sasa
itamkera rais na kuamua kuwasikiliza.
Kama hakuchakachua kura kwa nini
asisikilize malalamiko yao, ” alihoji
Kagenzi.
Mkazi mwingine, Saida Mbwana
alisema kitendo hicho kisipuuzwe kwa
kuwa kinaweza kuwa na athari kubwa.
"Kama hawamtambua Rais Kikwete,
basi hata serikali atakayoiunda
hawataitambua, jambo ambalo
litawakosesha maendeleo katika
majimbo," alisema.
Mkoa wa Arusha
Arnold Kamde, Gervas Mgonja pamoja
na Prosper Mfinanga ambao ni wakazi
wa Arusha walidai ya kuwa kitendo
hicho si tu kwamba kimeonyesha dalili
za kukua kwa demokrasia nchini, bali
pia kinatoa ujumbe kwa serikali ya Rais
Kikwete kuwa Chadema
hawakubaliani na matokeo ya urais
kwa kuwa yalichakachuliwa.
"Sheria ya nchi inasema kuwa mara
matokeo ya urais yakishatangazwa,
hakuna mtu wa kuyapinga
mahakamani. Sasa hiki kitendo si tu
kwamba kinaonyesha kukua kwa hali
ya demokrasia nchini bali pia ni
ujumbe tosha kwa serikali ya
Kikwete," alisema Mgonja.
Mfanyabiashara John Lyimo wa soko
kuu la Arusha alipongeza wapinzani
kwa kuonyesha hasira zao za kupinga
matokeo na pia alimpongeza Rais
Kikwete kwa kutoa hutuba nzuri.
"Mimi sina chama ila naona Chadema
wamefanya vizuri tu na wamefanikiwa
kufikisha ujumbe... rais aliongea vizuri
na ameonyesha ameupata ujumbe,"
alisema Lyimo.
Mkoa wa Mbeya
Watu wengi walioongea na
Mwananchi mkoani Mbeya waliunga
mkono kitendo cha Chadema
wakisema ujumbe waliotaka
kumfikishia rais ulifika.
“Chadema wana ujumbe ambao
wamewasilisha kwa serikali ya Rais
Kikwete na ni haki yao kufanya hivyo,”
alisema Jeremiah Osward ambaye ni
mkazi wa Vwawa wilayani Mbozi.
"Kutokana na tamko lao la kupinga
matokeo ya uchaguzi wa rais,
isingekuwa ni rahisi kwao kumsikiliza."
Mkazi wa Mwanjelwa, Zawadi Pangani
alisema wabunge hao walikuwa sahihi
kwa kuwa wanajua wanachokifanya ni
kwa ajili ya maslahi ya wananchi na
kwamba bila kufanya hivyo, haki
haitaweza kupatikana.
Alisema inawezekana Chadema wana
uhakika kuwa mgombea wao wa urais,
Dk Slaa alishinda, lakini matokeo
yakatangazwa kuwa ameshindwa,
hivyo wana haki ya haki yao kufanya
hivyo.
Mkoa wa Morogoro
Mmoja wa wakazi wa Morogoro,
Anthony Chalamila alisema tukio hilo
lilitarajiwa kwa sababu mgombea wao
alitamka wazi kuwa hakubaliani na
matokeo yaliyomtangaza Kikwete
kuwa rais kwa madai yana walakin.
“Ni lazmima wasimamie na kuyatetea
maamuzi yao, hivyo haingewezekani
mtu ambaye walisema hawamtambui,
wakae kumsikiliza, ” alisema.
"Kama wangekubali kukaa na
kumsikiliza rais akihutubia,
ingeonyesha wazi kuwa hawana
msimamo."
Mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa
jina la Naye Simon alisema ni haki yao
kufanya hivyo kwa kuwa walishatoa
sababu za msingi za kutomtambua rais.
Wanaopinga kitendo cha Chadema
Wasomi na wanazuoni
Mbali na wengi kuunga mkono kitendo
hicho, wapo ambao wanakipinga
wakiongozwa na kiongozi wa zamani
wa waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo, Profesa Ernest Wamba dia
Wamba ambaye alisema si cha
kiungwana.
Akizungumza katika mkutano wa
wanafalsafa ulioandaliwa na Chama
wa Falsafa Tanzania (Phata)
uliofanyika jijini Dar es Salaam, Wamba
alisema ni vizuri kama chama hicho
kingekubaliana na matokeo hayo.
“Kawaida katika siasa changamoto ni
jambo la kawaida, lakini kwa jinsi
ulivyoniuliza kuhusu uchaguzi wa hapa
Tanzania ni kweli umefanyika na
mshindi kapatikana, lakini ingekuwa
vizuri kama walioshindwa
wangekubali tu matokeo, ” alisema
Profesa Wamba.
“Wabunge wameshakula kiapo, lakini
wanasema hawatambui ushindi wa
rais. Wana haki ya kuzungumza kwa
kuwa hiyo ndio maana ya falsafa, lakini
kwa hili la kiapo litawabana.
Wangekubaliana na matokeo. ”
Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali......
Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC)
limeelezea kutofurahshwa na kitendo
kilichofanywa na Chadema na kukitaka
kutafuta njia mbadala ya kutoa
dukuduku lao.
Katibu wa TEC, Padri Antony Mkunde
alisema vyama vya siasa na
Watanzania kwa ujumla wanapaswa
kutambua kuwa amani iliyopo
haikushuka kutoka mahali popote bali
ni mshikamano na busara katika
uongozi.
"Mahali penye vurugu hata viongozi
wa dini hawawezi kuhubiri;
kinachotakiwa ni busara za viongozi
wa nchi katika kuhakikisha amani na
utulivu vinakuwapo," alisema
Makunde.
Kwa upande wake Taasisi ya Vyombo
vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la
Tanzania (MISATAN) imekielezea
kitendo cha Chadema kuwa ni utovu
wa nidhamu.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Rose Haji
alisema viongozi wa Chadema ni kati
ya viongozi waliokula kiapo
walipoapishwa hivyo wasingepaswa
kususia hotuba ya rais.
"Chadema wanatakiwa kumheshimu
rais kama baba mzazi kwa sababu baba
anapokosea huwezi kumdhalilisha
mbele ya kadamnasi hivyo heshima
inatakiwa pia katika suala la uongozi,"
alisema Haji.
Naye mwenyekiti wa taasisi ya
kiislamu ya Imam Bukhary, Sheikh
Khaliha Khamis alisema uamuzi wa
Chadema utasababisha chuki dhidi ya
chama hicho na wananchi
waliowachagua.
Alisema kitendo hicho kinaonyesha
dhahiri kuwa chama hicho hakiko
tayari kukubali misingi ya demokrasia
nchini na kuwatumikia wananchi.
Vyama vya siasa....
CCM imewataka wabunge wote
waliokiri kutomtambua rais kujitoa
haraka bungeni vinginevyo
wataondolewa na azimio la bunge
hadi watakapotambua uwepo wa rais.
Katibu wa kamati kuu ya CCM, John
Chiligati alisema kuwa kila mbunge
amekula kiapo cha kutii na kulinda
katiba na kitendo cha kutomtambua
rais ni uvunjaji wa katiba na hivyo
wabunge hao wanatakiwa kujiondoa
bungeni.
Chiligati alisema kitendo cha Chadema
kuruhusu wabunge na madiwani wake
kuendelea na kazi wakati
hawamtambui rais na serikali ni unafiki
wa hali ya juu.
Chiligati aliwataka wananchi kukataa
tabia za viongozi wanaokataa matokeo
kwa kuwa ni tabia inayoweza
kusababisha matatizo na kuchochea
vurugu nchini.
Katibu mwenezi wa NCCR-Mageuzi,
David Kafulila alisema kitendo hicho
hakikuwa cha kiungwana huku
akikielezea kuwa ni sanaa ya maigizo.
Wananchi na makundi mengine
Mkoa wa Kagera
Aliyewahi kuwa waziri kwa nyakati
tofauti katika awamu ya kwanza na pili
Balozi Joseph Rwegasira amewaponda
wabunge wa Chadema kwa kususia
hotuba hiyo.
Mwanasiasa huyo alisema kitendo
hicho kilikosa hekima kwa madai kuwa
hawakujua sheria na taratibu.
Balozi Rwegasira, ambaye pia aliwahi
kuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge,
alisema rais hawezi kususiwa na
wabunge kwa kuwa kwa mujibu wa
taratibu hata yeye ni sehemu ya Bunge
na kuhoji iweje wasisusie Bunge zima.
Mkoa wa Kilimanjaro
Mwenyekiti wa Umoja wa
Wafanyabiashar Wenye Viwanda na
Kilimo (TCCIA) mkoani Kilimanjaro,
Patrick Boisafi alisema kilichofanywa
na wabunge hao wa Chadema
hakikuwa cha uungwana na si mfano
mzuri wa kuigwa.
“Kama hawataki kutambua matokeo
yaliyompa Kikwete urais ina maana
kwa miaka yote mitano hakuna siku
watashiriki kutunga sheria Bungeni
kwa sababu ni lazima mwisho wa siku
iidhinishwe na Rais wanayemkataa, ”
alisema.
Alisema anachokiona ni ubinafsi wa
Chadema kwamba kionekane ndicho
chama kikuu cha upinzani nchini kama
ilivyo CUF kwa Zanzibar ili siku za usoni
wapate nafasi ya kuunda Serikali ya
Umoja wa Kitaifa.
Bendera Isinika, ambaye mkazi wa
Kaloleni anayefanya kazi ya uchoraji,
alipinga kitendo cha wabunge wa
Chadema kususia hotoba ya Rais
Kikwete kwa madai kuwa
hawakuwatendea haki wananchi
waliowachagua kwa kuwa walipaswa
kuwashirikisha kwanza kabla ya
kufanya tukio hilo.
"Kama kuna tatizo la uchakachuaji wa
kura wao walipaswa kutumia njia bora
na sio kususia hotuba ya Rais Kikwete
kwa kuwa wao tumewachagua sisi
hivyo wangetuambia kwanza kama
wanataka kutoka nje ya Bunge na si
kuchukua maamuzi yao," alisema
Isinika.
Mkoa wa Mbeya
Mkazi wa wilayani Mbozi, Imelda
Ngarawa alisema kuwa hayo ndiyo
matokeo ya upinzani kwa kuwa
wanafikiri bungeni ni mahali pa
kufanya sanaa, hivyo wameenda huko
si kwa ajili ya kuwatetea wananchi
bali kufanya sanaa.
Naye mkazi wa Tukuyu wilayani
Rungwe, Fadhili Sikumoja alisema
kuwa wabunge hao hawajafanya
vizuri kwani rais Kikwetye bado ni rais
wao kwani yupo madarakani na
kwamba ilikuwa vizuri wangemsikiliza
hotuba yake na kama wanahopja za
msingi wangewasilisha wakati wa
bunge lijalo.
Mkoa wa Morogoro
Mkazi wa Morogoro Leonard Mtete
alisema kuwa hatua iliyoonyeshwa na
wabunge wa chama cha Chadema
haikuwa nzuri kwa vile inaweza
kuwashushia umaarufu ulioanza
kujijenga katika chama hicho.
Alisema kuwa hali hiyo pia inaweza
kuionyesha jamii kuwa chama hicho ni
chama cha washari na wagomvi tofauti
na jinsi ambavyo watu
walinavyokichukulia kuwa
mapambano yake ni kidemokrasia na
ya amani.
“Mimi nafikiri wabunge wa chadema
wangetumia fursa waliyonayo
bungeni kupambana kwa hoja na siyo
kutoka kama walivyofanya wao ”
alisema mkazi huyo wa Morogoro.
Mkoa wa Iringa
Mkazi wa Iringa, Fanuel Kagambo
alisema haoni kama msimamo huo
unaweza kuwa na manufaa zaidi ya
kuwaumiza Chadema na akawashauri
kuanzisha njia nyingine ya kudai madai
yao kwa vile kumkataa rais na kushiriki
kupiga kura za kumthibitisha waziri
mkuu aliyeteuliwa naye
kuonaonyesha kumtambua.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman
Mbowe anasemaje...
Akizungumza na Mwananchi kwa njia
ya simu jana, Mbowe alisema
wanaowapinga au kuwa na mawazo
tofauti na uamuzi huo, wasilitazame
suala hilo juu juu na badala yake
waangalia hoja wanazozitoa.
Alisema Chadema haikuamka tu na
kutangaza kutomtambua rais, bali
inazo sababu za msingi ambazo
imeziweka bayana na imekuwa
ikizieleza kila kukicha na kulaumu
vyombo vya habari vinavyoshindwa
kuainisha malalamiko au hoja zao kwa
wananchi.
Mbowe alisema, msingi wa madai na
malalamiko ya Chadema ni kutaka
mazingira mazuri katika chaguzi zijazo
wananchi wapate viongozi
waliowachagua.
“Harakati ni kitu endelevu, michakato
huzaa tunda la haki, miaka 19 sasa
tangu siasa za vyama vingi ziruhusiwe,
kumekuwa na vilio vingi toka kambi ya
upinzani na kwa wananchi, lakini
wenzetu walioko madarakani
hawaonekani kusikia, tunatafuta lugha
mbadala baada ya lugha ya upole
kusikia ” alisema.
Alisema, jambo wanalopigia kelele sio
kilio cha Chadema pekee, bali ni kilio
cha watanzania wote na akasema
wanachofanya ni kutengeneza
mazingira mazuri ya uchaguzi wa
mwaka 2015.
“Yapo matatizo ya msingi na ni lazima
yafanyike mabadiliko ya haraka na ya
msingi, kwanza ni suala la katiba,
tutahitaji kuangalia katiba kama
chombo muhimu kinachoweza
kumkomboa mtanzania na kupunguza
vilio vya watu wengi ” anasema.
Akizungumza kwanini wanayakubali
matokeo ya wabunge na kuyakataa
yale ya rais, Mbowe anasema, “Hili ni
muhimu likawa wazi, sheria iko wazi
kabisa, kwamba Rais akishatangazwa
na Tume ya Uchaguzi hakuna
anayeweza kubadilisha wala kwenda
mahakamani, lakini ukiwa huridhiki na
ushindi kwa wabunge au madiwani,
sheria inaruhusu kwenda mahakamani
kupinga ” anasema.
Anasema, kutokana na sheria hizo
ambazo anasema ni miongoni mwa
mambo wanayoyapigia kelele
wameamua kutumia njia hiyo ya
kutomtambua rais ikiwa ni katika
hatarakati za kutaka marekebisho
katika sheria kandamizi kama hiyo ya
kutokuwa na haki ya kupinga endapo
wagombea wengine watakuwa
hawajaridhishwa na ushindi wa
mgombea mwingine.
Hata hivyo Mbowe alisema, Chadema
inatambua kuwa kwa kufanya hivyo
hakuwezi kubadilisha matokeo na
hakuwezi kuzuia Kikwete kuwa rais au
kuongoza serikali isipokuwa kwa
kufanya hivyo kutafikisha ujumbe wao
kwake Kikwete na serikali yake
pamoja na dunia nzima.
Habari hii imeandaliwa na Joyce
Mmasi, Nora Damian, Tumsifu Sanga,
Fidelis Butahe, Hussein Kauli, Minael
Msuya, Fredy Azzah, Michael
Matemanga, Petro Tumaini, Hussein
Issa, Aziza Masoud, Hidaya omary,
Burhani Yakub,Tanga, Daniel Mjema,
Moshi, Moses Mashalla na Mussa
Juma,Arusha, Brandy Nelson, Mbeya,
Tumaini Msowoya na Habel
Chidawali,Iringa,Venance George,
Morogoro, Phinias Bashaya,Bukoba,
Geroda Mabumo na Masoud Masasi
Dodoma na Frederick Katulanda,
Mwanza.
 
CCM imewataka wabunge wote waliokiri kutomtambua rais kujitoa haraka bungeni vinginevyo wataondolewa na azimio la bunge hadi watakapotambua uwepo wa rais.
Katibu wa kamati kuu ya CCM, John Chiligati alisema kuwa kila mbunge amekula kiapo cha kutii na kulinda katiba na kitendo cha kutomtambua rais ni uvunjaji wa katiba na hivyo wabunge hao wanatakiwa kujiondoa bungeni.

Chiligati ana kipindupindu cha akili kiasi kwamba anasahau msingi wa kiapo cha kutii na kulinda katiba. Hii ni pamoja na kutumia haki ya kugoma na uhuru wa maoni (ibara ya 18) pia haki ya kulinda na kusimamia katiba(ibara ya 26)
 
C mmeona? Asilimia kubwa ya waliosupport ni wasomi na wanataaluma wakubwa hapa nchini.... Na waliopinga ni wale wakawaida kabisa wasiojua kufikiria kwa undani.... Ebu tuendeleeni kuwaelimisha kwani ipo siku wataelewa maana ya demokrasia!?
 
Hakuna kosa lolote kwa mujibu wa katiba ya jmt ibara ya 100(1)(2)

Jamani muoneeni huruma mleta mada hii. yawezekana hajui kabisa anachofanya ila anataka tu naye aonekane kaleta mada. Kwanza kabisa ningependa huyu bwana ajue kuwa CHADEMA wamefanya kitendo cha kishujaa na ninawapongeza sana.Kama siyo kuwa na ufinyu wa kuona mambo kwa mbali asingethubutu kusema alichokisema. au naye ni miongoni mwa mafisadi?? hata kama mtu ambaye hana akili timamu hawezi kusema eti Chadema wamefanya kosa inabidi waombe radhi kwa kikwete. Au huwa hafatilii siasa za Tanzania??
Mara nyingi sana wapinzani hasa wakati wa bunge lililopita walisema sana kuhusu kufanyika kwa marekebisho ya katiba, kuundwe tume huru ya uchaguzi lakini hija hizo zilipingwa vikali sana na wabunge wa chama cha mafisadi na serikali yake kwa ujumla. na Hayo yaliyo tokea wakati wa uchaguzi ni matokeo ya wana CCM na serikali yake kutosikiliza hoja za wapinzani. CCM wamekuwa wababe mno hasa kwa kutotaka sikiliza maoni ushauri na mengineyo mengi kwa kujifanya kuwa wao ndo wanajua kila kitu kumbe sivyo. Hakuna binadamu katika uso wa dunia anayejua kila kitu. watu wote unajifunza kutoka kwa wenzetu.
CCM wamekuwa wadhalimu wa kuzurumu haki za msingi za raia. kama tulivyoshuhudia wakichakachua matokeo ya uchaguzi. wamezurumu haki ya raia ya kujichaghulia kiongozi wanayemtaka. Je huyu mleta mada hakuona kuwa hilo ni KOSA KUBWA kuliko hata hilo la CHADEMA analoliona yeye kuwa ni kosa wakati si kweli???

Mimi kwa mtazamo wangu nasema CHADEMA wametumia haki yao ya msingi kutosikiliza Hotuba ya mtu aliyetumia madaraka yake kujipatia nafasi ambayo hakustahili. na wala si vinginevyo.
Ndugu zangu watanzania wenzangu, tuangalie mambo kwa mapana siyo tu kukulupuka kwa ushabiki bila hata kutafakali. Tanzania inakoenda siko kwenyewe. Amini usiamini.Kubali usikubali kwa mtindo huu wa CCM kujiwafanya wababe kwa kutumia vyombo vyao vyo dola kudhulumu haki za wananchi.. tunaenda kubaya mno. Upende usipende machafuko yatatokea tu Tanzania muda si mrefu. Na hii ni kwa sababu ya utawala mbaya wa KIkwete na CCM yake. Tanzania si shwari tena kama wengi tunavyo dhani.. hilo tulitoe akili mwetu kama CCM itaendelea kutowasikiza maoni na ushauri kutoka vyama vya upinza, mauwaji ya sisi kwa sisi yatatokea tu. hili hapingiki.
Tena mimi Binafsi nawapongeza sana Chadema kwa ujasiri waliofanya wakati wa uchaguzi na kipindi cha kutangazwa mshindi aliyepewa nafasi hiyo kwa njia ya udanganyi. CHADEMA hawakuleta fujo; hiki ni kitendo cha Kistaarabu sana walichoonyesha.
Kwa hiyo ndugu yangu kama wewe unaitakia mema Tanzania, mwambie CCM na Kikwete wasitumie ubabe.wasisubiri mpaka machafuko ndo wakubali mabadiliko. wasisubiri mpaka raia wapoteze maisha ndo waunde tume ya kuchunguza ndo wakubali mabadiliko, wasisubiri watu kutoka mataifa ya nje ndo walete mabadiliko ya demokrasia Tanzania.
wakubali mabadiliko kwa njia ya mazungumzo ili kumaliza tatizo litakalo leta machafuko Tanzania.
Asanteni sana
 
Back
Top Bottom