Elections 2010 Viongozi wa BAVICHA kujulikana Aprili

Tatizo lako hauwezi kutofautisha JamiiForumn na Website ya Chadema na CCM. Hapa wapo wanachama na wasiowanachama wa vyama vya siasa (CCM, CDM, CUF, TLP etc). Pia kumbuka kuna wanachama wapenda maendeleo na wapenda ufisadi ndani ya hivi vyama. Kama unafikiri kuwa unawaeleza BAVICHA hapa, umepotea njia zaidi ya kubroadcast tuu. Tunataka issue zinazogusa taifa. Lakini sikushangai kwani watu kama nyie mupo na ndo maana nilitoaa hii thread kwa ajili ya wana JF wote.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/120524-hii-lazima-kila-mmoja-asome.html


Mbona UVCCM inachambuliwa hapa?mbona Zitto vs mbowe zinachambuliwa?mbona Slaa vs Makamba zinachambuliwa?

Mimi nachukia hii tabia ya watu kama akina Slaa kuwa traped na ishu za infidelity,kama ilivyokuwa kwa akina Bill Clinton

Haka kajama kutembea na Prof. wake ilikuwa ni kuvuka mpaka hata kama alikuwa demu wa kawaida.Na taarifa tulizo nazo huyu Mwisrael alikuja Tanzania hata baada ya huyu jamaa kutua tu,huyo ndiye alimfundisha kiebrania

Wewe mkuu unaonekana nikimjadili hilo linakukera sana.Kwanza siasa za ubabe hazina nafasi,umafia hauna nafasi.Kuna siku alikuwa analalamika CCM kuingiza mamluki upinzani,yeye mwenye na mission hiyo hiyo kupandikiza mamluki UVCCM ili aiongoze bavicha kimafia.Nitakutafutia hiyothread,hatutaki siasa za kupandikiziana mamluki,nadi sera na ujenge chama basi.Umafia hatutaki,una implications zake
 
Kwa nini unafikiri jinsi unavyofikiri juu ya hawa wapiganaji chipukizi wa CDM??


Mkuu nimetoa hoja,nimetoa positive na negative

Mimi nikiona watu wanamkubali mtu ni lazima niende extra-mile.Sitaki kuburuzwa au kufuata mkumbo,kwani nakosea?
 
Uelewa ktk siasa za dunia ya tatu bado kwako! Unapoleta zuio la kisiasa leta na mswada wa ufumbumbuzi! Siasa zako hasinatofauti na za wasira,makamba,kikwete na wengine wengi wenye mawazo mgando wanaorithishwa fikra!! Ushauri wangu kwako kuwa msomaji tu usijihusishe na chchte utakomaa kifikra,kimoyo na kimwili!! Mlaumu anayekufundisha******!!!!!!!
 
Takbiir,
Nakushukuru kwa kumpigania muislamu mwenzetu Habib Mchange, ila nina tatizo moja juu ya huyu kijana , ni kuwa amefeli UDOM na anadanganya eti ameahirisha mwaka ili agombee uenyekiti wa BAVICHA.
Sasa kama amefeli akiwa mwaka wa kwanza hivi ataweza kweli kuivusha hiyo CDM?
Arudie mwaka aanze masomo kwani watamtukana kuwa ni muislamu asiyekuwa na akili ndio maana amefeli, tumechoka kutukanwa sisi jamani, ukipata nafasi ya kusoma soma sana .
Habib, nafasi anayo ila aende akasome ili wawe waislamu wengi waliosoma ndani ya CDM.KWA Leo ni hayo tuu.
 
Uelewa ktk siasa za dunia ya tatu bado kwako! Unapoleta zuio la kisiasa leta na mswada wa ufumbumbuzi! Siasa zako hasinatofauti na za wasira,makamba,kikwete na wengine wengi wenye mawazo mgano wanaorithishwa fikra!! Ushauri wangu kwako kuwa msomaji tu usijihusishe na chchte utakomaa kifikra,kimoyo na kimwili!! Mlaumu anayekufundisha******!!!!!!!

Wewe ndiye muelewa.Ndugu yangu badala ya kuchangia hoja wewe unakaribia kunitukana,wewe ni mtovu wa nidhamu na mbabe kama huyo jama.Na yupo humu humu JF.

Angalia mchango wake ktk moja wapo ya thread inayohusu Sumaye kulaumu Uvccm,kila mtu alikuwa namfagilia sumaye na baadhi ya wazee wa CCM.Yeye akaibuka na kauli hii nainukuu hapo chini

'Akina Makamba,msekwa,Chiligati na hata sumaye mwenyewe ndiyo walioifikisha UVCCM hapo ilipo.Ndiyo maana we are hell bent to ensure that BAVICHA Haiwi kama UVCCM.Tunaamamini jumuiya au Baraza la Vijana linatoa taswira ya chama au taifa in future

Hiyo UVCCM na mawazo yao unayoyaona ndiyo future ya CCM na kama wataendelea kushika dola hiyo ndiyo future ya chama hicho na Tanzania ya baadae,hili tutalikataa kwa nguvu zetu zote,kwa akili zetu,kwa hoja na umoja wetu wote!

It's rather unfortunate that young men and women are being dragged into the dirty waters of ethno-religious politics which has been d bane of this country.
When are we going to learn from our past and not allow our shameless elders ruin our future by inducting us into the old ways of doing things.
Those agitating for the old order of doing things including the shameless act of perpetuating themselves in power are simply failures.
My argument, is that if men who have served this country before(or is it their ethnic region and friends and pocket) in different capacities do not believe that the younger generation have all it takes to lead this country. It can only mean one thing, and that is that they have failed to raise future leaders and to that extent i see them as failures. And if at their age, they are still ignorant of their failures, then they don't deserve our attention.
''

Mwisho wa kunukuu,kwa envedence zaidi comfirm hapa ili ujue sifanyi majungu
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/121035-sumaye-akutana-na-waandishi-wa-habari%3B-afafanua-msimamo-wake-13.html#post1780231
 
Takbiir,
Nakushukuru kwa kumpigania muislamu mwenzetu Habib Mchange, ila nina tatizo moja juu ya huyu kijana , ni kuwa amefeli UDOM na anadanganya eti ameahirisha mwaka ili agombee uenyekiti wa BAVICHA.
Sasa kama amefeli akiwa mwaka wa kwanza hivi ataweza kweli kuivusha hiyo CDM?
Arudie mwaka aanze masomo kwani watamtukana kuwa ni muislamu asiyekuwa na akili ndio maana amefeli, tumechoka kutukanwa sisi jamani, ukipata nafasi ya kusoma soma sana .
Habib, nafasi anayo ila aende akasome ili wawe waislamu wengi waliosoma ndani ya CDM.KWA Leo ni hayo tuu.

Haki Sawa,

Kuna watu najua lengo lao ni kuupinga Uislam na si CCM au Ufisadi.Sisemi huyu jamaa kama anaupinga uislam,lakini vilevile ingawa anajifanya kupinga udini na ukabila lakini bado aliutumia kuwagawa wakenya hadi alipofanikiwa kupata kura makabila ya wakenya kugombea urais wa Wanafunzi wa kimataifa,akatumia udini kuwagawa wanafunzi wanaotoka Thailand.Akavaa sura ya kikomunist kupata kura za wachina.Huyu mimi ndiyo sijawahi kumuamini katika mienendo yake,hata kama anaungwa mkono na Dunia nzima

Huyo Mchange naye aende shule,BAVICHA inabidi iongozwe na wasomi.So dogo akaze buti tutafika tu.

Nilishangaa sana,kisa cha mgogoro wake na profesa wake wa Uchumi.Ati analazimisha kwamba resources are not scarce,anajaribu kujenga hoja ya kijinga kabisa ati mbona resources za petrol kutumika kwenye magari sasa hivi kuna magari yanayotumia maji.Anamkomalia Prof.ati nadhani scarcity of resources ni state of mind ya individuals tu

Alipoona anachanganya darasa lake Prof.akamwambia akae chini anang'anga'niza bado haelewi hadi Prof alipomtaka atoke,jamaa akagoma pia na kuburuza Darasa likawa linataka Prof yeye atoke.Sasa imagine mtu kama huyu mwenye udikteta wa mawazo ndiye aongeze BAVICHA,kwani tunajenga ukomunisti? aende huko kwa akina Kagame na museveni au venezuela,si Tanzania
 
Jabalpur ni Madhya Pradesh
Allahabad ni uttar Pradesh
Acharya ni Karnataka.
Ilikuwa ina muhusu nini kuharibu uchaguzi wa acharya(KARNATAKA) na yeye alikuwa nasoma Allahbad(Uttar Pradesh)?
sasa huyo Ben Saanane alifanya vp yote hayo kwa wakati mmoja?
Naona hapo kuna uongo unatumiaka kwa sababu watanzania wengi hawaifahamu India.
 
India_map.jpg
Hiyo ndo ramani ya India.
 
Tafadhali kama unaona una haki ya kuendelea kuwapo na kuchangia njoo na hoja za msingi.
Usilete ubinafsi na upotoshaji
 
Takbiir,
Nakushukuru kwa kumpigania muislamu mwenzetu Habib Mchange, ila nina tatizo moja juu ya huyu kijana , ni kuwa amefeli UDOM na anadanganya eti ameahirisha mwaka ili agombee uenyekiti wa BAVICHA.
Sasa kama amefeli akiwa mwaka wa kwanza hivi ataweza kweli kuivusha hiyo CDM?
Arudie mwaka aanze masomo kwani watamtukana kuwa ni muislamu asiyekuwa na akili ndio maana amefeli, tumechoka kutukanwa sisi jamani, ukipata nafasi ya kusoma soma sana .
Habib, nafasi anayo ila aende akasome ili wawe waislamu wengi waliosoma ndani ya CDM.KWA Leo ni hayo tuu.


Heshima kwako Mkuu HS,
Nakubaliana na ushauri unaoutoa kwa Habibu laini sikubaliani na kansa unayoonesha kuiendeleza ya "Mwislam mwenzetu." Hivi inakuwaje kila kitu ninyi mnakitazama kwa macho hayo? Mkuu HS hivi unatenda mema kiasi gani ukajihakikishia pepo katika mazingira haya ya kibaguzi? Nashindwa kukutetea dhidi ya "wanaowatukana" kuwa hamjasoma kwa sababu kwa kweli unathibitisha kabisa kuwa haujasoma. Sioni mantiki ya "kuongeza idadi ya Waislam" wasomi CDM au CCM au TZ kwa kuwa jamii hizi ustawi wake haujengwi na Wakristo au Wahindu wasomi bali Wana-CCM, Wana-CDM na Wa-TZ wasomi.

Ah, hizi fikra hizi!!!! Afrika bwana!!!!
 
Bwana Nuclear1 tunakusoma namna ulivyo...mbinu yako hii ilitumika mwaka 1754 hivyo huna jipya! Kwamba msimchague fulani kwa kua ni wa kanda fulani ila mchagueni huyu kwa kua ni "wa dini yetu" alafu unadhubutu kuonesha umeingia darasani! Kweli kama ninyi ndio wasomi wetu kazi tunayo kufikia malengo ya millenia! salam zako
 
Kwa sababu umetaja mabaya yao tu ukaacha mengine,basi kwa sifa ulizo toa naona hawa wanafaa sana kuongoza BAVICHA
1.Mimi mwenyewe (Speaker)
2.John Heche
3.Ben Saanane

Kwa jinsi ulivo elezea hawapendi kuonewa,wana faa kuongoza na wanasifa kama zangu sema tu mimi bado niko shule,naomba kura yako ili niwe mwenyekiti wa bavicha

 
Ndugu Nuclear1

Baada ya kukusoma nimegundua nia yako hasa si kuishauri CDM kuhusu viongozi wa BAVICHA ila ni kutimiza lengo lako la bifu na Ben Saanane wengine ni uliowataja ni geresha tu. Halafu una elements za udini na ukanda tusimchague huyu kwa sababu anatoka kanda fulani au ni dini fulani. Sisi vijana tunachohitaji ni uwezo wa mtu kuongoza si dini yake wala kabila lake FSP.
 
Vitendo,
Wewe ndiyo Muongo,ati kwamba mtu kusafiri imbo moja hadi lingine ndani ya India ni kazi au haiwezekani?
Huyo jamaa ni member wa huku,mbona hathubutu kugusa hii thread? Inaonekana wewe uko nyuma sana kwa Technolojia ya Mawasiliano.Kwa Taarifa yako maeneo hayo yanafikaka kwa kuwa India kuna network pana ya usafiri,sijui ni kitu gani hukielewi ndugu yangu
 
Kwa sababu umetaja mabaya yao tu ukaacha mengine,basi kwa sifa ulizo toa naona hawa wanafaa sana kuongoza BAVICHA
1.Mimi mwenyewe (Speaker)
2.John Heche
3.Ben Saanane

Kwa jinsi ulivo elezea hawapendi kuonewa,wana faa kuongoza na wanasifa kama zangu sema tu mimi bado niko shule,naomba kura yako ili niwe mwenyekiti wa bavicha


Kwa kuwa hulka zako zinafanana na hao,Tanzania haiko tayari kuendeshwa kidikteta.Kwanza wewe ndiyo hufai,huyo Heche hatuwezi kumzungumzia.Wewe kwanza unakiri hujamaliza Shule,angalia usije uka-disco kama Mchange ambaye hata hivyo kura yangu nitampa yeye.Ninyi wengine mkawa mabaunsa wa night clubs au mkatumikie JKT
 
Ndugu Nuclear1

Baada ya kukusoma nimegundua nia yako hasa si kuishauri CDM kuhusu viongozi wa BAVICHA ila ni kutimiza lengo lako la bifu na Ben Saanane wengine ni uliowataja ni geresha tu. Halafu una elements za udini na ukanda tusimchague huyu kwa sababu anatoka kanda fulani au ni dini fulani. Sisi vijana tunachohitaji ni uwezo wa mtu kuongoza si dini yake wala kabila lake FSP.

Nimesema inabidi chama kichore mstari watu wa kanda ya kaskazini wasijiingize kwenye kinyang'anyiro kwa kuwa chama kimeimarika kule,pia ili kuuwa hoja ya ukabila na Udini

Narudia tena Habib Mchange ndiye chaguo sahihi kwa kuwa atakuwa ameua hoja zote mbili.hata kama nina bifu nae,sikubaliani na makomunist au ma-radicals kushika idara yoyote Tanzania,Matokeo yake ni kuigeuza nchi kama Bolivia.Ni jambo la ajabu kwa Mtu mwenye masters ya Uchumi kukumbatia ujamaa ilihali anajua ujamaa ulishindwa.Mtu anayeamini katika Mapinduzi ni hatari,si hata hapa JF hoja ya Mapinduzi inapigwa vita?iweje mumtetee mtu wa aina hii?Mtu kama anadiriki kulala na profesa wake,unategemea nini?Kwanza hoja ya uzinzi inawatafuna wanasiasa wabongo,Haishangazi wanaJF mnaishadadia.Nitatafuta post zake nikiipata nitaweka ili huyo jama hapo juu aliyenibatiza muongo aumbuke.

Pia,watu aina ya Silinde hawafai kwa kuwa ni mtu wa kurubuniwa na anapenda sifa za kijinga.Sitaki nionekane nafanya majungu lakini mimi napenda haki.
 
Nimesema inabidi chama kichore mstari watu wa kanda ya kaskazini wasijiingize kwenye kinyang'anyiro kwa kuwa chama kimeimarika kule,pia ili kuuwa hoja ya ukabila na Udini

Narudia tena Habib Mchange ndiye chaguo sahihi kwa kuwa atakuwa ameua hoja zote mbili.hata kama nina bifu nae,sikubaliani na makomunist au ma-radicals kushika idara yoyote Tanzania,Matokeo yake ni kuigeuza nchi kama Bolivia.Ni jambo la ajabu kwa Mtu mwenye masters ya Uchumi kukumbatia ujamaa ilihali anajua ujamaa ulishindwa.Mtu anayeamini katika Mapinduzi ni hatari,si hata hapa JF hoja ya Mapinduzi inapigwa vita?iweje mumtetee mtu wa aina hii?Mtu kama anadiriki kulala na profesa wake,unategemea nini?Kwanza hoja ya uzinzi inawatafuna wanasiasa wabongo,Haishangazi wanaJF mnaishadadia.Nitatafuta post zake nikiipata nitaweka ili huyo jama hapo juu aliyenibatiza muongo aumbuke.

Pia,watu aina ya Silinde hawafai kwa kuwa ni mtu wa kurubuniwa na anapenda sifa za kijinga.Sitaki nionekane nafanya majungu lakini mimi napenda haki.
Nuclear1

Nafikiri mambo ya kulala na professor wake hayana nafasi hapa ni makubaliano yao huwezi kuwaingilia, mfano kama umeoa ukiulizwa kwanini hukuoa mwingine ukaoa uliye naye leo unaweza kujibu.
 
Mkuu, unafanya kazi usalama wa taifa? mbona taaarifa zako zimejaa chuki binafsi? Unamkandia Silinde wakati watu wa Mbozi wanamheshimu na kumuamini sana. Mbona hoja za Silinde bungeni ni kubwa na za msingi sana kuliko hata wabunge wazoefu. Wacha majungu yako, wala sioni umhimu wa kuyajadi maisha binafsi ya wahusika. Kwamsingi huo wewe mwenyewe hufai kabisa.
 


Kumbe kuna thread kama Hii?Kuna watu wako hapa kutekeleza miradi ya watu kwa maslahi wanayojua wenyewe,Ni muda mrefu kidogo tangu niingie hapa kutokana na Majukumu,nawashukuru sana Marafiki zangu wa JF kwa kunipa Taarifa juu ya kinachoendelea.Naomba nijibu japo kidogo na kwa ufupi,ingawa najua naweza nisikutosheleze

Nuclear1,

Naomba upate mda uje hapa kuthibitisha tuhuma Hizi ulizotoa hapa,nina uhakika hauna Envedence na sijui Lengo lako ni nini.Mwaka jana ulikuja na thread nyingine za uongo na uchafu mwingi tu kwa malengo unayoyajua

Umeongelea kwamba natoka Kilimanjaro,Sikatai.Mimi ni mzaliwa wa Kilimanjaro kweli.Je,hilo ni kosa kugombea uongozi ndani ya BAVICHA?Ni lini tulianza kuchagua watu kwa kutumia makabila yao au Dini zao?Haya si mamabo ya kujadili kwa sasa,na hayana Tija.

Kuhusu Kuhusika kwangu ku-incite vurugu katika uchaguzi wa serikali za wanafunzi chuoni kwetu,huu ni uongo.Polisi India wangenikamata na kunifungulia Mashtaka.Ni very simple,Njoo uthibitishe hili tafadhali

Kuhusiana na uchaguzi wa Acharya,mimi nilikuwa na haki ya kumpigia kampeni mgombea ambaye angeshinda kule ili tufanye nae kazi kwa urahisi.kipindi kile hatukuwa na uhusiano mzuri na ubalozi wetu hiyo hali tuliikuta.Ubalozi ulikuwa unatumia kugawanyika miongoni mwetu ili wasiwajibike kutuhudumia,kwa hiyo ilikuwa ni lazima tuungane tuwe kitu moja ili kutetea maslahi ya wanafunzi wenzetu.Tusingekubali kuishi kama wakimbizi,huku tukiwa na ubalozi ambao unalipwa kwa kupitia kodi ya Watanzania.Watanzania mlio nje ni mashahidi wa jinsi balozi zetu zinavyopenda kusukumwa katika kutekeleza wajibu wao.Ikumbukwe,Balozi ni mwakilishi wa Rais nje ya nchi.Ubalozi unajukumu la kusimamia Maslahi ya watanzania nje ya nchi.

Kuhusu Kugombea Uongozi wa serikali ya wanafunzi wa kimataifa,Naona pia unapotosha.Mtindo wangu wa kampeni ulikuwa ni kutafuta washirika ambao wangenipigia kampeni.Kila nchi nilihakikisha na kuwa Mshirika mwenye ushawishi bila kujali kabila,dini au class.Sioni kosa lolote nililofanya

Kuhusu kugombana na Profesa,hilo ni suala la uwongo.Nilihitaji clarifications,argument ikahusisha Darasa Zima.Kama ni ugomvi ulitokea katika sura nyingine na ilikuwa ni Darasa vs profesa wao.Hii ni hoja ya kitoto mno

Umeongelea kuhusu kumkataza balozi asijihusishe na matawi ya vyama vya siasa.Ndiyo nakubali nilifanya hivyo,kwa kuwa mimi naamini Watanzania tulikuwa wachache sana nje.tulitakiwa kuishi kwa umoja wetu.Hata mimi sikufungua Tawi la CHADEMA kwa kuwa niliamini kabisa kwa kufanya hivyo tunarudisha nyuma au kufifisha spirit ya umoja wetu kama Watanzania.Balozi ni wa Watanzania,si wa wana-ccm wala Cuf,wala CHADEMA.

Tafadhali naomba uache kupotosha kwa kutumia jina la uongo,njoo hapa uongee ukweli.Halafu unadiriki kuji-associate na CHADEMA na wakati tunajua wewe ni CCM Damu Damu. Kaeni muimarishe chama chenu,kachukue fomu za UVCCM pia mwakani kama umri wako utakuwa unaruhusu,vinginevyo subirini tuongoze BAVICHA,Mtaona cha mtema kuni.Stop Hating brother!
 
Duh....e bana eeh hoja zakoo zina mashiko..ingawa ina udini kwa mbaliiiiii(hoja ya mwisho)..mwenye macho aone na mwenye masikioa aikie,mweny akili afanyie kazi hili..!!
Ushauri wangu kwako ni kwamba usiwaogope hawa mods, smtm ni wachakachuzi sana, sasa mambo kama haya mods wanataka tusiyafahamu...nakumbuka kuna post yako moja ilikuwa na mtiririko kama huu...niliipenda ila sikujuwa baada ya pale ulipigwa ban. Mi nilikuja india na wale vijana wa acharya(akina Nape) sema baadae tulipelekwa state moja inaita Kerala..na wengine walipelekwa Alahabad(ndo hao akina saanane)


Namaste Sizinga,

Jumuiya za watanzania India unazijua,Uhusiano wetu na balozi aliyekuwepo ulikuwa unaujua.Balozi ambaye yupo mpaka sasa hivi hakufuata nyayo za mtangulizi wake,alikubaliana na sisi na aliona kuwa wanafunzi tulihitaji haki.tulihitaji kupata msaada,na pia kunufaika na jukumu la Ubalozi kutuunganisha watanzania.Kwa hali ilivyo sasa,ukienda kwenye ubalozi wetu pale New Delh utapewa ushirikiano wa kutosha na unajiona uko nyumbani.Zamani palionekana kama gerezani kuna watu wali-sacrifice,kuna watu waliokuwa wanawasaliti watanzania wenzao na kujipendekeza kwa maofisa wa ubalozi at the expense of others.Sisi wengine tulipenda haki,tunajua ni kwa nini tuna balozi nje ya nchi

Matatizo mengine yaliyopo ni matokeo ya sera mbovu ya mambo ya nje.

Sizinga,wewe ni shahidi.Kwa nini wanafunzi wa Kerala hasa TKM walikuwa wanapindua uongozi wao mara kwa mara.Ni kwa sababu ya suspicion na mistrust.Wengine kweli niliwaunga mkono.Kulikuwa na lile sakata la serikali yetu kulipa hela nyingi vyuoni hasa Hostel,kitu kilichotulazimu kuanzisha Movement ya kutaka kuchukua hela ili tuzipangie bajeti wenyewe.Tunajua tulikotoka.Wenzetu wa Bangalore walituunga mkono,na hata wanafunzi wa nchi nyingine nao waliamua kuasi hadi chuo kika-surrender pamoja na zile balozi zao.

Hela zile tulitumia kupanga mitaani,chenji iliyobaki watu wengine waliamua kujisomesha masters na wengine Diploma au Course nyingine.Tulikuwa tunatetea haki yetu.Baada ya hap Hata watu wa Kerala walitoka nje pia,kwa hiyo walinufaika na kitendo chetu cha kujitoa mhanga



 
Back
Top Bottom