Nzoka yihenge
Member
- Jan 14, 2011
- 44
- 29
Jamani ndugu zangu viongozi wa Jiji la Mwanza nawaombeni fikirini nje ya boksi na anzeni sasa ujenzi wa barabara mbadala wa zile kuu ziendazo Musoma, Shinyanga na Uwanja wa ndege. Nionavyo mimi hali ya foleni za Magari inaelekea kubaya na sioni jitihada zinazofanyika juu ya hilo. Fungukeni jamani ! unganisheni maeneo mfano Airport-Buswelu-Nyamhongolo-Buhongwa. Jaribuni kujifunza kutokana na hali ilivyo Jiji la Dar.