Viongozi hawawezi leta Maendeleo - Mkapa

two to go posts you are becoming member welcome.
to this all are mafisadi so differ in fisadism..
 
Ujasiri aliopata Mkapa ni siku ile kwenye sherehe ya kuwekwa wakfu na kutawaza Askofu wa Mbinga ambapo Kikwete katika hotuba yake kwa kuwanyooshea kidole viongozi wa dini wakati kosa labda ni mtu fulani mmoa au wawili wasio na umaarufu katika mashirika ya dini wakati Mkapa akishuhudia imeonyesha dhahiri udhaifu mkubwa alio nao Kikwete na ukosefu wa busara kutoangalia watu, nafasi, tukio na mazingira anapotoa tamko .

Kwa mtazamo wangu Marais wote waliomtangulia Kikwete, kuanzia Nyerere, Mwinyi na Mkapa wasingeota tamshi kama lile kwa watu wale, mazingira yale, nafasi ile na tukio lile na nina hakika kati ya wahudhuriaji viongozi wa dini pale hakuna hata mmoja ambaye anahusika na biashara ya madawa ya kulevya.

Mkapa ujasiri huo aliopata ni kutokana na aibu aliyoipata kama kiongozi mwandamizi mstaafu kushuhudia kiongozi aliopo madarakani kutoa matamshi kama yale kwa watu ambao hakutegemea kwa nafasi na heshima yao kwa jamii. Kuna ya kuvumilika kisiasa lakini inapofikia kuwavunjia heshima watu wenye nyadhifa kama za maaskofu wale katika jamii mtu mwenye dhamira ya kujali nafasi zao anapata uchungu na ujasiri wa kufumba macho na kuongelea ukweli wa hali halisi ilivyo.
 
Kama hukupata kumsikiliza Mkapa hapa unaambulia zero au unachanganyikiwa kabisa
 
Mkuu kama maneno haya ni kweli nambie kimetokea nini Rwanda hadi wamefanikiwa na pia kimetokea nini Zimbabwe hadi wakafilsika. Nionyeshe ni wapi uwezo wa wananchi umechangia mabadiliko yote hayo!

Na mwisho wa yote nipe nchi yeyote iliyoendelea na viongozi wake hawakuwa mstari wa mbele ktk uongozi na ujenzi wa maendeleo hayo.

Mara nyingine tunapochangia hapa, huwa tunategemea kuwa watu wanauelewa wakutosha kuweza jazia sehemu ambazo ziko obvious zaidi. Kwa mfano, tunaposema serikali haitakuletea mwananchi maendeleo sebuleni kwako, hatumaanishi kuwa serikali haina kazi ya kufanya katika maendeleo ya kiuchumi. Serikali ina nafasi yake muhimu, kama walivyoainisha wachangiaji wengine, k.m;

- kujenga miundombinu
- kuhakikisha usalama wa raia, dhidhi ya maadui wa ndani na nje
- kuhakikisha usalama wa mali za raia, ikiwapo usalama dhidhi ya utaifishaji wa jasho la mtu
- kujenga uwezo wa wananchi, kupitia elimu - na siyo kupitia uwezeshaji wa kifedha

nk

Sasa;

Rwanda: Serikali imehakikisha usalama wa wananchi kujifanyia shughuli zao na ni kutokana na shughuli hizi za wananchi ambapo unasikia ile nchi inafanikiwa.

Zimbabwe: Serikali imeshindwa kulinda mali za watu kwa hiyo wananchi wameacha kujishughulisha na uchumi na ndipo nchi ikadidimia. Utakumbuka kuwa Zimbabwe walifanya ile dhambi ya kutaifisha. Ukishataifisha mali, unawaambia wananchi wasihangaike kujitafutia kwani watanyang'anywa jasho lao.

Mwisho, ili nchi iendelee, ni lazima wananchi wake wawe na mwamko, uwezo na ari ya kujiletea maendeleo yao binafsi. Ni kwa kujiendeleza binafsi ambapo wananchi huleta maendeleo kwa taifa kwa ujumla. Viongozi wanaweza wakachangia kufikia hili, lakini siyo lazima kama wananchi wamekaa sawa.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom