Viongozi GNU wahusishwa na uamsho Zanzibar

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
Vyama vya upinzani Zanzibar vimesema harakati zinazoendeshwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI) ya kutaka Zanzibar kujitenga katika Muungano, zimepangwa na viongozi ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Tamko hilo limetolewa jana na vyama vya TADEA, SAU, NLD na AFP katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo mjini Zanzibar, kufuatia vurugu zilizotokea Mei 26, mwaka huu na kusababisha makanisa na maduka ya pombe kuchomwa moto.

Akitoa tamko hilo kwa niaba ya vyama hivyo, Katibu Mkuu wa TADEA Juma Ali Khatib alisema kwamba jina la jumuiya ya Uamsho, linatumika kama kivuli, lakini harakati zinaendeshwa na viongozi ambao wamo ndani ya Serikali bila ya kuzingatia amani na umoja wa kitaifa kwa wananchi wa Zanzibar.

"Sisi kama wanasiasa, tunafahamu kwamba jina la jumuiya hii, linatumika kama kivuli, lakini harakati zinaendeshwa na viongozi ambao wamo ndani ya Serikali ya umoja wa kitaifa na vyama vya siasa," alisema Juma Ali Khatib ambaye aliwahi kugombea urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu uliopita.

Alisema kwamba Jumuiya ya Uamsho, imekuwa ikipata ufadhili wa fedha kutoka nje ya nchi, ili kufanikisha ajenda ya kutaka Zanzibar ijitenge ndani ya Muungano, na imeanzisha harakati zake kupitia misikiti, makongamano na mihadhara ya dini.

"ushahidi wa haya ninayozungumza hauhitaji taaluma kubwa kuweza kujua chama kipi cha siasa kinahusika, harakati za jumuiya hii zinaendeshwa kwenye maeneo ya wafuasi wengi wa chama hicho, na hata viongozi wake wanashindwa kuzilaani hadharani harakati za jumuiya hii, licha ya athari zilizojitokeza za kuharibu vibaya jina na sifa ya visiwa vyetu," alisema Juma Ali Khatib ambaye aliambatana na viongozi wa ngazi za juu wa vyama hivyo Zanzibar.

Alisema kwamba vyama hivyo vinalaani vitendo vilivyofanywa na jumuiya ya Uamsho, kwa vile havijazingatia maslahi ya nchi, hasa uchomaji moto wa makanisa, kuharibu mali za umma, na uchomaji wa maduka ya vileo.

"Kupitia mkutano huu, tunawaomba sana wananchi wa Zanzibar na wale wanaoishi nje ya visiwa hivi, kuwa makini sana na kundi hili.

"Kitendo kilichofanywa na kundi hili, cha kuwatanguliza wanawake mbele, hakijapata kutokea katika historia ya nchi hii, tunawatanabahisha akina mama wasikubali kutumiwa namna hiyo, na wasicheze ngoma wasiyoijua", alisema Juma Ali Khatib.

Katibu huyo wa TADEA alikumbusha makundi ya namna hiyo yaliyosababisha matokeo mabaya pamoja na maafa, akifananisha na makundi ya Al Qaeeda, Bokoharam ya Nigeria, Al Shabab ya Somali, ambapo kwa kiasi kikubwa yamesababisha madhara makubwa hasa kwa akina mama na watoto.

Vyama hivi vimependekeza kwa serikali kuangalia usajili wa jumuiya ya Uamsho, kutokana na kwenda kinyume na masharti ya usajili wao na kufanya kazi za kutangaza sera za vyama, kwa mwelekeo wa kuirejesha Zanzibar kwenye mifarakano, vurugu, siasa za chuki na uhasama miongoni mwa wananchi.

Pia wameitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kuchukua juhudi maalum za kuhakikisha hakujitokezi tena vurugu kama hizo, na kuwachukulia hatua wote waliohusika katika mpango huo wa kutaka Zanzibar kujitenga katika Muungano.

"Tumepata taarifa za kundi jingine la wananchi wa Zanzibar wanaopendelea kudumishwa kwa Muungano, linaanzisha harakati dhidi ya wale wanaopinga Muungano wakidai kuwa udongo uliochanganywa wakati wa kuziunganisha nchi mbili ulitoka Unguja na tanganyika na sio kisiwani Pemba" alisema Katibu huyo na kuongeza.

Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud, alisema uchunguzi kuhusu mtandao wa Jumuiya ya Uamsho unaendelea kufanywa na vyombo vya dola na utakapokamilika hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria.

CHANZO: NIPASHE
 
" hao nao!!! hahaha angalau wametukumbusha kama wapo, wallahi binafsi yangu nilikuwa nishawasahau. haya baba endeleeni kutafuta nafasi ya kujipatia umaarufu"
 
" hao nao!!! hahaha angalau wametukumbusha kama wapo, wallahi binafsi yangu nilikuwa nishawasahau. haya baba endeleeni kutafuta nafasi ya kujipatia umaarufu"
Mkuu uwe unawapa watu hongera pale wanapofanya vizuri hata kama huko nyuma waliwahi kufanya madudu, usiwe na roho iliyopinda. Wakosowe kwa hoja pale unapoona wamepotosha, usikimbilie kwenye character assassination ili ku justify mtizamo wako. Ni hayo tu! nakutakia ushiriki mwema kwenye hizi harakati za kuleta mabadiliko ya kweli tanzania.
 
Mbona hilo liko wazi wote walitegeana hata kulisemea na wengine mpaka leo wako kimya, Ni uroho wa madaraka uliopitiliza
 
Vyama vya upinzani Zanzibar vimesema harakati zinazoendeshwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI) ya kutaka Zanzibar kujitenga katika Muungano, zimepangwa na viongozi ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar...


ZANZIBAR IS COMING BACK


552824_10151234021009152_1295757788_n.jpg
 
Mbona hilo liko wazi wote walitegeana hata kulisemea na wengine mpaka leo wako kimya, Ni uroho wa madaraka uliopitiliza
Kweli mkuu, viroho vinawadunda kwa unafiki wao.
Lazima wanaogopa hata kutoka juani wasije kuzomewa na wapenda amani.
 
Back
Top Bottom