Viongozi Chadema - must read

Kosa ni kosa tu, ila kurudia kosa ni udhaifu usiokubalika na huhatarisha. Tukumbuke kwamba vijana bado wadogo na upeo wao katika masuala ya kijamii bado ni mdogo, ndio maana wanaandaliwa wakomae kwa siku za usoni kuwa watendaji wazuri.

Nisingependezwa sana na ibuko la hoja ya kumfukuza Makamu mwenyekiti, kwani kufukuzana si dawa ya kujenga chama, bali kudhoofisha chama. Jambo muhimu ni kumweka kitako Makamu mwenyekiti ajue kosa alilofanya ili asirudie kosa kama hilo tena. Asiposikia na kufuata ushauri hapo hakuna namna nyingine zaidi ya termination from her post. Afundwe namna bora ya utendaji katika ofisi yao kuwa ni mawasiliano, na katu asiwe tayari kutumiwa na wengine kutoa matamko. Tuelewe tamko lile si lake binafsi kuna walio nyuma ya pazia. Akifukuzwa huyu dada atakuwa ameonewa tu kwa vile ametumiwa kama chambo tu. Kuna waliojificha nyuma yake ambao hawataki wajulikane kwamba wako kinyume cha mwenyekiti. Hayo ni makovu ya uchaguzi uliopita ukiangalia kwa jicho la upembuzi.

Angefukuzwa Shibuda tangu alipoanza mizengwe yake huenda kungekuwa na athari zaidi kuliko alivyoachwa. Ndio maana dhana ya ignore imemweka Shibuda katika kapu kisiasa badala ya kuwa jukwaani kama wengine wanavyozidi kuchanja mbuga katika kutangaza magwanda yao. Aanachofanya sasa ni kujikomba upande wa CCM kwa vile ameshapoteza mwelekeo upande wa chama chake alivyotarajia.

Kwa vyo vyote vijana hawa wanahitaji kijana mwenzao kama Zitto au Mnyika kuwasaidia kukaa sawa ofisini mwao, la sivyo matamko yanayokinzana yanatoa mwanya wa kuweka nyufa za kupitisha mende kisha siafu watafuta harufu ya mende na hakutakalika huko ndani.
Mkuu Candid scope, Kama huyu ni kijana mdogo basi makosa yake yangelingana na udogo wake. Umesema sawia kabisa kuwa huenda katumwa na kuna watu nyuma yake. Yeye amekubali kutumiwa akiwa kama kiongozi. Hapo hakuna udogo kuna ujinga na hilo tu linamuondolea sifa ya uongozi na kumwacha na udogo wake.

Kumbuka CDM kikiwa chama tawala leo hawa ndio wanategemewa kuunda serikali, sasa tuwasamehe kwa udogo upi wakati ukubwa umeshatimia.

Kitendo cha kutumiwa ni dalili njema kuwa yeye kama kiongozi analea mbinu chafu na hilo linamuondolea sifa ya uongozi

Nimeainisha kwanini afukuzwe na nitashangaa sana kama CHADEMA hawatamfukuza uongozi. Lakini pia nimependekeza option ya yeye kuomba radhi.

Narudia tena kuwa CHADEMA huyu ni mtu hatari sana kwa ustawi wa chama chenu. Aondolewe ili waliomtuma wafahamu kuwa hakuna mkubwa zaidi ya chama na kwamba sheria ni msumeno. Akiachwa ataendelea kupika majungu na kukiangamiza chama kama CCM ilipo.

Asifukuzwe uanachama hata kidogo, AFUKUZWE UONGOZI. Hafai huyu, kuna maelefu ya vijana wenye akili nzuri, ni aibu chama pinzani kuwa na mtu mmoja anayevuruga chama kwa wiki sasa. Watu wamesahu shughuli nyingine kwasababu ya huyu Dada na chama kinazidi kupakwa matope kwa sababu ya huyu mtu mmoja.

Nitawashangaa sana CDM kama watamwacha aendelee na uongozi. Chadema watapoteza moral authority ya kunyooshea kidole CCM. CDM itakuwa inafanyia kazi template ya CCM.Ni aibu kubwa sana na hapaswi kulelewa kisiasa kwasababu dalili za awali zimeonyesha ni sumu na wala hataelewa hata kama atafundishwa. Hafai huyu CDM!

Tuliwapa 'open book exam' yeye amefeli. Tuliwatahadharisha yeye amefeli. Hafai huyu na kama BAVICHA ni tofauti na UVCCM basi imuondoe haraka sana katika uongozi. Kumuacha huyu itakuwa UVCCM-B na wakae kimya daima milele. Tusijewasikia wakisema tena maana hawatakuwa tofauti na huyu dada ambaye ni miongoni mwao. Hafai hata kwa bahati mbaya!
 
huyu dada asiharibu mtazamo mzuri tulio nao kwa wanawake kuhusu kupata nafasi za uongozi na kuzitumia vema na kwa busara.
viongozi wanawake tanzania ni wachache sana aisee, halima mdee, is among them, huyu makamu mwenyekiti wa BAVICHA ndo nimemfahamu leo kwa upumbavu wake,
 
Mkuu Candid scope, Kama huyu ni kijana mdogo basi makosa yake yangelingana na udogo wake. Umesema sawia kabisa kuwa huenda katumwa na kuna watu nyuma yake. Yeye amekubali kutumiwa akiwa kama kiongozi. Hapo hakuna udogo kuna ujinga na hilo tu linamuondolea sifa ya uongozi na kumwacha na udogo wake.

Kumbuka CDM kikiwa chama tawala leo hawa ndio wanategemewa kuunda serikali, sasa tuwasamehe kwa udogo upi wakati ukubwa umeshatimia.

Kitendo cha kutumiwa ni dalili njema kuwa yeye kama kiongozi analea mbinu chafu na hilo linamuondolea sifa ya uongozi

Nimeainisha kwanini afukuzwe na nitashangaa sana kama CHADEMA hawatamfukuza uongozi. Lakini pia nimependekeza option ya yeye kuomba radhi.

Narudia tena kuwa CHADEMA huyu ni mtu hatari sana kwa ustawi wa chama chenu. Aondolewe ili waliomtuma wafahamu kuwa hakuna mkubwa zaidi ya chama na kwamba sheria ni msumeno. Akiachwa ataendelea kupika majungu na kukiangamiza chama kama CCM ilipo.

Asifukuzwe uanachama hata kidogo, AFUKUZWE UONGOZI. Hafai huyu, kuna maelefu ya vijana wenye akili nzuri, ni aibu chama pinzani kuwa na mtu mmoja anayevuruga chama kwa wiki sasa. Watu wamesahu shughuli nyingine kwasababu ya huyu Dada na chama kinazidi kupakwa matope kwa sababu ya huyu mtu mmoja.

Nitawashangaa sana CDM kama watamwacha aendelee na uongozi. Chadema watapoteza moral authority ya kunyooshea kidole CCM. CDM itakuwa inafanyia kazi template ya CCM.Ni aibu kubwa sana na hapaswi kulelewa kisiasa kwasababu dalili za awali zimeonyesha ni sumu na wala hataelewa hata kama atafundishwa. Hafai huyu CDM!

Tuliwapa 'open book exam' yeye amefeli. Tuliwatahadharisha yeye amefeli. Hafai huyu na kama BAVICHA ni tofauti na UVCCM basi imuondoe haraka sana katika uongozi. Kumuacha huyu itakuwa UVCCM-B na wakae kimya daima milele. Tusijewasikia wakisema tena maana hawatakuwa tofauti na huyu dada ambaye ni miongoni mwao. Hafai hata kwa bahati mbaya!

Kama umenipata vizuri ni kwamba apewe nafasi ya kujenga utetezi wake, na anatakiwa kumwomba radhi mwenyekiti wake na huo ndio ukomavu wa kisiasa. Hali kadhalika akalishwe chini kupata ushauri wa kufaa. Akitambua kosa na kujkiri kutorudia tena asamehewe. Lasivyo anaendelea na ushupavu wake bila kukiri kosa na kuomba radhi basi termination itakuwa ni njia mbadala ili kunusuru mpasuka katika umoja wa vijana.
 
Mbona Heche Mnasema kakosea straight bila Kumung'unya maneno, ofcourse amekosea kweli, Lakini huyo Dada Juliana hamtaki kusema kuwa straight kuwa na yeye kakosea, Usiwe Biased Ben , watu wanaweza wakasema Pengine unachuki Binafsi na Heche coz u competed for the same post.

Nataka useme hivi, Heche alikurupuka kutoa tamko, na Pia huyo Dada alikurupuka Zaid kutoa tamko na kumkosoa Mwenyekiti bila kutumia vikao halali, tusiwe na Double standard jaman eeeh.

Duh! mkuu si wamekosea? ulitaka lazima Ben amtaje na huyo mwingine, sijui nani....maana sikuwahi kusikia jina la huyo binti!! Kichwa cha bavicha ni Heche!! kuwa kachemka, sasa lazimisha yako eti angewasema wote ndio kunatoa maswali mengi!!!! na umejijibu vizuri kuoanisha ushauri wa Ben na uchaguzi wa Bavicha, you were into this man!! puuuuuu

aibu!!
 
Mkuu Candid,

Mimi nataka nikuulize, Hivi tutafanya vikao kwa kila jambo? Hivi hata mwanachama wa Chadema akisema CDM hakiwezi na hakina uwezo wa kushika dola kumjibu tunahitaji vikao vya nini? Hicho ndicho kinachoicost CCM kutokana na viongozi hawafanyi majukumu yao wanakuja na excuses kila siku... Mimi nafikiri Shibuda alishavumiliwa sana na Mchwa wapo CDM baada ya kuona matumaini ya kupata Mpunga CDM haupo kinachotakiwa ni kazi kwa kwenda mbele, basi ameamua kuanza kuta matapishi yake tangu Baada ya Uchaguzi.

Na wote wanaomtetea Shibuda ni kuwatema Uanachama.. Ni heri kuwa wachache CDM na mkadeliver kinachoeleweka kuliko kuwa wengi halafu yaendelee yale yale ya CCM... Shibuda inaonyesha ananjaa sana na kashaahidiwa Mpuunga... Na hao wanaompa ulinzi ndani ya CDM... Wajue ulinzi huo wanaompa siyo Bure... Kama ni bure basi na wao hawastahili kuwepo kwenye Meli hii ya Ukombozi wa Taifa letu.
 
Nguruvi; umesema vizuri sana lakini huyu dada kadokeza kitu kimoja ambacho sidhani kama watu wamekifikiria na ambacho umekisema pia kuwa ni kufuata template ya CCM. Huyu dada alisema maneno ya Heche (mwenyekiti wa taifa) siyo ya Bavicha kwa sababu hakuna "kikao" kilichokaa na kuamua hivyo. Naita hili uongozi wa "vikao" kwamba hakuna lolote linaloweza kufanywa na viongozi au kutendwa bila vikao. Sasa hili ni zuri kwenye kupitisha sera n.k lakini linapokuja suala la kutenda wale waliopewa madaraka ya kutenda ni lazima watende.

Sijui Katiba ya BAVICHA inasema nini kuhusu madaraka ya viongoziwake lakini tunatarajia kuwa kiongozi anapokuwa kiongozi ana madaraka yote ya kiongozi. Kauli ya Heche ilipotolewa ilitakiwa kutetewa na viongozi wengine wote kwa sababu yeye ndiye kiongozi mkuu wa Bavicha na inawezekana ndiye "msemaji mkuu" wa Bavicha kwa mujibu wa katiba yao. Huyu makamu hana madaraka wala uwezo wa kusimama na kusema "ile" siyo kauli ya bavicha!

Lakini tatizo ninalolizungumzia ni hili la 'vikao'. Kwamba, watu wenye madaraka kamili wanashindwa kusema au ufanya jambo lililo ndani ya uwezo wao bila vikao. Hivi, ina maana kila wakati jambo linatokea baraza lazima liitwe liulizwe litoe kauli yake? sasa kuna maana gani ya kuwa na Mwenyekiti? Mbona ni kana kwamba dhana ya madaraka (authority) haijaeleweka? Kama kauli ya Heche ambaye ndiye kiongozi mkuu wa vijana wa CDM haina nguvu yenyewe hadi ipepewe na kufukizwa udi na kikao kuna maana gani ya kuwa na Mwenyekiti? si kamati tu iwe inaongoza na kila jambo lifanywe na kamati hiyo?

Ndio maana naamini ningekuwa na uwezo huyu binti angeomba msamaha kwanza kwa kuingilia mambo yasiyo yake na akikataa anaambiwa ajiuzulu - bila kujali watu watasema nini. Somebody in CDM needs to show leadership. Shibuda anawajaribu na sasa huyu naye mwisho 2015 itafika na tutarudi exactly at status quo ya 2010!

Mkuu Mwanakijiji sikubaliani na muono wako katika hili.
Ni wazi kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA alitoa ile kitu inaitwa "Gut feeling", msukumo wake binafsi.
Makamu wake amescore a major point-HAKUNA KIKAO KILICHOJADILI SUALA HILO.

Pengine ningeuliza tena kwa herufi kubwa-HII KITU INAITWA DEMOKRASIA NI MNYAMA GANI?
Hasa kwenye sensitive issues like these.

Na je tutawaamini vipi hawa watu watakaoendeleza kukurupuka kichama kwa kuwakabidhi nchi?
Sasa CDM kama itachukua nchi na kiongozi wao akatusiwa na kiongozi wa nje-kitu cha kawaida katika siasa, ataamrisha majeshi yajibu mapigo.

I am stretching the scenario to its limits, lakini inabidi CDM iwe careful katika kutengua masuala ambayo kinsingi yanaweza kuleta utata zaidi.
Na huko ndio kukua kwa chama chenu.
 
huyu binti katokea wapi? mbona kwenye kujenga chama haonekani lakini hili moja tu la heche amelirukia.
mwepesi wa kuharibu kuliko kujenga, tena ishu yenyewe inamhusu shibuda hivi anafikiri kwa kutumia nini?

sikatai heche alichemka kutoa kauli bila kuitisha kikao cha chama ambacho kingejadili vizuri na kufahamu ukweli halisi kuhusu kauli ya shibuda kwani lazima tukubali kuwa wakati mwingine kuna waandishi wa habari wamewekwa mifukoni na ccm na wanatabia ya kubadilisha kauli za baadhi ya wanasiasa. hivyo inatupasa kuwa makini wakati wa kujadili kauli za watu, lakini kukosea kwa heche hakuwezi kuwa kosa zaidi ya kurudia kosa kama alivyofanya huyu binti.

kurudia kosa lilelile bila kuitisha kikao na kujadili swala hili kwa umakini zaidi, anakidhoofisha chama na mwisho tutataka aondoke kwa sababu mchango wake wa kujenga chama haupo. Ni ukweli usiofichika kwamba Heche ni binadamu na anaweza kuwa amesema hisia zake kama zilivyo kwa wanachadema wengi. Hivyo kutokana na kuona mtu mmoja anataka kukivuruga chama kwani shibuda siku zote amekuwa yuko mrengo wa kushoto.

lakini pia napenda kutoa tahadhari kwa CHADEMA kuwa makini na huyu Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA. kwani amekuwa tayari kumpigia kifua shibuda mtu ambae hayuko serious bila ya kuangalia hisia za wanachama wengi wa CHADEMA ambao kwa uwelewa wao hawana imani na huyu mtu kutokana na matendo yake.

kama ishu ndogo hivi inayosababishwa na mtu kama Shibuda ambae ni mtu wa kupuuza na sisi kuendelea na maswala muhimu hasa Katiba yeye anakurupuka na kurudia kosa lilelile la Heche keshokutwa kwenye mambo ya kimaslai atafanya nini?

Mwisho nasisitiza vikao vya chama vitumike, na heshima iwepo ili tamko likitoka liwe moja.
 
Mkuu Candid,

Mimi nataka nikuulize, Hivi tutafanya vikao kwa kila jambo? Hivi hata mwanachama wa Chadema akisema CDM hakiwezi na hakina uwezo wa kushika dola kumjibu tunahitaji vikao vya nini? Hicho ndicho kinachoicost CCM kutokana na viongozi hawafanyi majukumu yao wanakuja na excuses kila siku... Mimi nafikiri Shibuda alishavumiliwa sana na Mchwa wapo CDM baada ya kuona matumaini ya kupata Mpunga CDM haupo kinachotakiwa ni kazi kwa kwenda mbele, basi ameamua kuanza kuta matapishi yake tangu Baada ya Uchaguzi.

Na wote wanaomtetea Shibuda ni kuwatema Uanachama.. Ni heri kuwa wachache CDM na mkadeliver kinachoeleweka kuliko kuwa wengi halafu yaendelee yale yale ya CCM... Shibuda inaonyesha ananjaa sana na kashaahidiwa Mpuunga... Na hao wanaompa ulinzi ndani ya CDM... Wajue ulinzi huo wanaompa siyo Bure... Kama ni bure basi na wao hawastahili kuwepo kwenye Meli hii ya Ukombozi wa Taifa letu.

Kwa kila kosa adhabu iwe tu ni panga tu, yaani kufukuza uanachama au kung'olewa uongozi si dhana nzuri ya kujenga utu wa watu na usitawi wa nchi. Binadamu ana akili na utashi, ndio maana ya kuweka taratibu za maonyo na uangazi kumpa nafasi ya kujirekebisha. Asipojirekebisha hapo hatua inayofuata ni kubwa zaidi.

Kitu cha msingi si kuangalia tu kufukuza mtu bila kuwa na maono ya athari zake za papo kwa papo na za baadaye. Uvumilivu na ustahimilivu vikijengeka na busara ni dhana muhimu katika kuboresha chama chao na kuwa na manufaa kwa nchi. Hiyo ndiyo sababu ya kuweka kiwango cha mtu kugombea cheo cha juu kabisa Urais katika nchi ni kutokana na kuwa na umri wenye sifa hizo, vinginevyo ni papara papara na kukurupuka katika maamuzi bila mwono wa kugeuza pando zote kusoma matokea yanayoweza kuadhiri au kuendeleza nchi.
 
0000001anajulia.jpg
275738_100002659456794_1144001_n.jpg

Matamko ya mmoja mmoja hata kama anakinga ya kikatiba hayakubaliki kwa ajili ya kulinda mshikamano na umoja katika utawala wa kisheria. Ni dalili ya kuwepo ufa katika mfumo wa uongozi na nihatari kutohimili vishindo vya tetemeko la ardhi litokeapo nyumba yenye ufa.

Narudia kauli ambayo nilishawahi kumwambia Katibu Mkuu Dr. Slaa ambaye kwa sasa amefanikiwa kurekebisha kutoka safu ya juu Chadema, lakini tatizo ni kwa Ngazi ya juu Umoja wa Vijana Chadema.

Lazima kuondokana na mlipuko wa kujibu kwenye vyombo vya habari ghafla bila upembuzi wa kutosha, bila kutuliza kwanza nerves, bila kikao cha kushauriana nini cha kujibu na papo kuangalia upande wa pili wa sarafu athari zake kwa tamko litakalotolewa.

Busara inavyoonekana katika uongozi wa juu kwenye Uongozi wa Chadema naheshimu na ndicho kinachotakiwa, ila ipo kazi kuwaweka sawa viongozi wa BAVICHA.

Candid Scope naheshimu michango yako na hata Avatar yako. La msingi hapa ni hawa viongozi kujifunza kwamba kwa sasa wanapoongea, wanakisemea chama hata kama wapo nyumbani au baa. Kwenye vyombo vya habari ndo kabisa. Kwa hiyo wanatakiwa kujifunza kusemea chama na siyo wao tu. Hii itawafanya kufikiria chama na kuomba ushauri kabla ya kuongea na vyombo vya habari. Kuhusu huyu makamu wa mwenyekiti, labda ndivyo alivyo shauri . Sasa tujiulize, lipi ni tamko la BAVICHA, la mwenyekiti au makamu mwenyekiti? Je tutajuaje kuwa sasa mwenyekiti anaongea mawazo yake? Mambo yanapokuwa mambaya watu huyakimbia na kuyaacha kwa mhusika, lakini yakiwa mazuri, ya chama. Wapewe semina elekezi, lakini mambo ya kuja kutoa maelezo eti ni mawazo ya kiongozi kama yeye, mimi haiji akilini. Kwa sababu inaonyesha uwezo wa kiongozi huendani na chama.
 
Akina Mnyika na Kabwe wawasaidie vijana wenzao hawa kufanya kazi pamoja kitaasisi. Sababu ya kumweka msemaji kwenye nafasi hizi ni sababu ya kuondoa kasoro za matamko kama haya ambayo hukanganya.

Jambo la msingi si vema kuyachukulia yatolewayo na waandishi wa habari, hawa wako kwa ajili ya kuuza habari zao na vyombo vyao vya habari vipate soko. Bora kuvuta subira ili kujiridhisha na habari iliyotolewa vinginevyo kurukia kutoa matamko kutokana na kusoma magazetini utakuwa wanajiingiza vichwa vichwa kwenye makaa ya moto bila kujijua.

Kwa mtazamo wangu Shibuda wamempa tu kichwa kwa habari hii, kwani alipoongea na Kikwete ulikuwa ni utani wa kisiasa tu. Ndio maana alipomjibu Heche akageukia kwa Slaa kuwa atakuwa mpiga debe wake katika kampeni za urais.
 
Ninadhani hapa kutakuwa kuna mkono wa TISS dhidi ya CDM, Haiwezekani, tena nasema haingii akilini kuwa leo Makamo mwenyekiti anaweza kuwa na power ya kumuignore mwenyekiti wake! kuna kitu tusubiri... nadhani ile dhana ya juridiction na separation of power bado ni tatizo kwa walio wengi, sasa tazama jinsi huyu binti alivyo jiua kisiasa
 
Wanajifunza uongozi, muda uliobakia unatosha kabisa kabla ya uchaguzi 2015. Isipokuwa huyo Heche kwa kweli alikurupuka nadhani alikuwa na kinyongo na Shibuda akasahau kufikiri kwanza kabla ya kutoa tamko. Kwa hiyo ajifunze kwamba uongozi hauendi kwa chuki na kuviziana kwenye kona

Sawa kukurupuka kwa Heche hakuhalalishi alichokifanya huyo dada. Kama bosi wako kakurupuka, kweli ni sahihi kwenda kumtangaza hadharani? kwa nini asifanye busara ya kumchukua chemba na kuelezana na kama ikibidi litolewe tamko rasmi la baraza. Heche alichemka lakini Huyo bibie ndie kachemsha zaidi na kufukia kuliko pitiliza. Na namshauri awe mwangalifu sana sisi tumeshaanza kumuogopa.
 
Leadership is a process... CDM will have to go through it... and this is the time.... Kuongoza Chama ni tofauti na Serikali... in government you can command etc... but not in political party... tuwape muda vijana wajifunze....
Nyie ndio mmeiangushia Tz jehanamu halafu eti mnajidai ''tuwape muda wajifunze''. Mnajua uongozi?
 
Mbona Heche Mnasema kakosea straight bila Kumung'unya maneno, ofcourse amekosea kweli, Lakini huyo Dada Juliana hamtaki kusema kuwa straight kuwa na yeye kakosea, Usiwe Biased Ben , watu wanaweza wakasema Pengine unachuki Binafsi na Heche coz u competed for the same post.

Nataka useme hivi, Heche alikurupuka kutoa tamko, na Pia huyo Dada alikurupuka Zaid kutoa tamko na kumkosoa Mwenyekiti bila kutumia vikao halali, tusiwe na Double standard jaman eeeh.

Sijawa biased.Nimeongelea kuwa Shibuda hastahili kupewa attention kiasi hiki.Nimesema makosa yatatuliwa ndani ya vikao vya chama watu wasifanye hii ni big deal kwamba kuna mgogoro.

Kuhusu kuwa na chuki binafsi na Heche.Aint that type.Siwezi kuwa na chuki binafsi.Baada ya uchaguzi mimi naangalia mbele.Katika maandishi yangu nionyeshe nilichokosea ili nijisahihishe

Lakini huyu mwana mama nae mwambieni atulize mapepo yake. Kama aliona mwenyekiti amepotoka kwanini yeye azidi kuleta matatizo? Nae ni kicheche tu. Ni kundi moja na wewe na Zitto.

Duh....

kwahiyo hata hapa bado mwaungana mikono......! nadhani bado kuungana mwili...! umeshajipambanua wazi kuwa HECHE alikubwaga mlipogombea uenyekiti. sasa utamsifia kwa lipi tena....weye siulisema waenda jimboni rombo kucompete na selasini ubunge? huyo bibie ndo meneja campaign wako ee...kaza buti kijana..!
Mr.Clean,

Kuwa mstaarabu kidogo.Tatizo lako unaamini siasa ni u-simba na U-yanga.

Uchaguzi wa BAVICHA ulikwisha naangalia mbele.Sijawahi kushindwa uchaguzi.....

Kwa nini niwe na tatizo na Heche?Kama ingekuwa tatizo basi ningekuwa na tataizo na kamati ya wazee na siyo Heche kwa sababu sikupata fursa ya kuingia naye kwenye ballot.Na hata ingekuwa hivyo nisingekuwa na tatizo kwani mimi ni muumini wa demokrasia.Sina Tatizo na uongozi wa Bavicha.Usilishe watu sumu

Naomba ulete uthibitisho kwamba nimetangaza nitagombea Rombo.Vinginevyo wewe uchukuliwe mzushi tu katika haya uliyoandika

Nguruvi; umesema vizuri sana lakini huyu dada kadokeza kitu kimoja ambacho sidhani kama watu wamekifikiria na ambacho umekisema pia kuwa ni kufuata template ya CCM. Huyu dada alisema maneno ya Heche (mwenyekiti wa taifa) siyo ya Bavicha kwa sababu hakuna "kikao" kilichokaa na kuamua hivyo. Naita hili uongozi wa "vikao" kwamba hakuna lolote linaloweza kufanywa na viongozi au kutendwa bila vikao. Sasa hili ni zuri kwenye kupitisha sera n.k lakini linapokuja suala la kutenda wale waliopewa madaraka ya kutenda ni lazima watende.

Sijui Katiba ya BAVICHA inasema nini kuhusu madaraka ya viongoziwake lakini tunatarajia kuwa kiongozi anapokuwa kiongozi ana madaraka yote ya kiongozi. Kauli ya Heche ilipotolewa ilitakiwa kutetewa na viongozi wengine wote kwa sababu yeye ndiye kiongozi mkuu wa Bavicha na inawezekana ndiye "msemaji mkuu" wa Bavicha kwa mujibu wa katiba yao. Huyu makamu hana madaraka wala uwezo wa kusimama na kusema "ile" siyo kauli ya bavicha!

Lakini tatizo ninalolizungumzia ni hili la 'vikao'. Kwamba, watu wenye madaraka kamili wanashindwa kusema au ufanya jambo lililo ndani ya uwezo wao bila vikao. Hivi, ina maana kila wakati jambo linatokea baraza lazima liitwe liulizwe litoe kauli yake? sasa kuna maana gani ya kuwa na Mwenyekiti? Mbona ni kana kwamba dhana ya madaraka (authority) haijaeleweka? Kama kauli ya Heche ambaye ndiye kiongozi mkuu wa vijana wa CDM haina nguvu yenyewe hadi ipepewe na kufukizwa udi na kikao kuna maana gani ya kuwa na Mwenyekiti? si kamati tu iwe inaongoza na kila jambo lifanywe na kamati hiyo?

Ndio maana naamini ningekuwa na uwezo huyu binti angeomba msamaha kwanza kwa kuingilia mambo yasiyo yake na akikataa anaambiwa ajiuzulu - bila kujali watu watasema nini. Somebody in CDM needs to show leadership. Shibuda anawajaribu na sasa huyu naye mwisho 2015 itafika na tutarudi exactly at status quo ya 2010!

Mwanakijiji,

BAVICHA haina Katiba.........

Bavicha inaongozwa na katiba ya chama na muongozo wa mabaraza.Hebu isome katiba ya chadema vizuri
 
Ninadhani hapa kutakuwa kuna mkono wa TISS dhidi ya CDM, Haiwezekani, tena nasema haingii akilini kuwa leo Makamo mwenyekiti anaweza kuwa na power ya kumuignore mwenyekiti wake! kuna kitu tusubiri... nadhani ile dhana ya juridiction na separation of power bado ni tatizo kwa walio wengi, sasa tazama jinsi huyu binti alivyo jiua kisiasa
HABARI YA UHAKIKA: Kikwete ametengeneza mtandao Chadema kwa kutumia TISS. Nina info za ndani, jikoni liliko jungu likitokota. Zinatumika fedha nyingi na ahadi za vyeo kemkem. Ndio maana mambo kama haya yapo na YATAKUWEPO. Chunga sana hii listi.... Zitto, Ben, ''Mzee Shibuda'' kama anavyoitwa na huyo makamu wa mwenyekiti njaa, yeye mwenyewe (makamu bavicha). Wana jeuri mbaya sana na wameahidiwa mengi. Tunawamulika kwa karibu kila nyendo tena kwa kituo. Tumeweza kupenyeza watu wetu. Tunasubiri siku ya siku....
 
Candid Scope naheshimu michango yako na hata Avatar yako. La msingi hapa ni hawa viongozi kujifunza kwamba kwa sasa wanapoongea, wanakisemea chama hata kama wapo nyumbani au baa. Kwenye vyombo vya habari ndo kabisa. Kwa hiyo wanatakiwa kujifunza kusemea chama na siyo wao tu. Hii itawafanya kufikiria chama na kuomba ushauri kabla ya kuongea na vyombo vya habari. Kuhusu huyu makamu wa mwenyekiti, labda ndivyo alivyo shauri . Sasa tujiulize, lipi ni tamko la BAVICHA, la mwenyekiti au makamu mwenyekiti? Je tutajuaje kuwa sasa mwenyekiti anaongea mawazo yake? Mambo yanapokuwa mambaya watu huyakimbia na kuyaacha kwa mhusika, lakini yakiwa mazuri, ya chama. Wapewe semina elekezi, lakini mambo ya kuja kutoa maelezo eti ni mawazo ya kiongozi kama yeye, mimi haiji akilini. Kwa sababu inaonyesha uwezo wa kiongozi huendani na chama.
Kukosea ni hulka ya kibinadamu na inapotokea mhusika huomba radhi. Semina elekezi haitamsaidia huyu Dada kwani ni dhahiri kuna watu wapo nyuma yake, hawa ndio watakaovuruga chama.

Nimesoma thread ya taarifa aliyotoa. Thread hiyo imeanzishwa na mtu aliyejiunga leo au aliyetumia ID nyingine ili kujenga utetezi kwa huyu Dada. Ukisoma taarifa ile ni wazi kuwa mtu asiyeelewa taratibu za uongozi kama Juliana asingeweza kuandika kwa mtitiriko ule, hata hivyo maudhui yanatia kichefu chefu. Ameigeuza hoja ya Heche na kuwa suala la mgombea urais na kuacha kiini halisi cha kwanini Heche alito kauli ile(poor spinning)

Ni utetezi ambao kama mimi ngingelikuwa uongozi wa CDM ningemfukuza uongozi bila kusubiri kikao au baraza.
Bado amejichanganya kuwa alichosema ni maoni yake kwasababu amekerwa na kauli za Heche. Wakati huo huo anamlaumu Heche kutumia nafasi yake kama mwenyekiti na haki ile ile aliyo nayo kuzungumza bila vikao. Yeye hakutuambia alizungumza kwa idhini ya nani.

Bado ninasimamia hoja yangu kuwa huyu binti afukuzwe uongozi kabla ya weekend hii maana ni tatizo kubwa. Kumlea huyu kutakipeleka chama pabaya.

Badala ya kukiri mapungufu amezidi kuonyesha kiburi cha kutoa taarifa kana kwamba watu wanaochangia hapa hawaelewi nini alisema na nini hoja yake

Huyu Dada amekichafua CDM hasa mwenyekiti wa BAVICHA ambaye amedhalilika sana na kumuondolea heshima na hadhi yake. Njia pekee ya kurudisha heshima na hadhi ya Heche ni kumuondoa Juliana Shonzo.

Njia pekee ya kurudisha imani ya kuwa CDM kina mwelekeo tofauti wa kuchukua maamuzi magumu dhidi ya wasio na nidhamu ni kumuondoa Juliana.

Njia pekee ya kuondoa makundi yanayojificha nyuma ya huyu Dada ni kumtia nidhamu.

Njia pekee ya kuwa na 'moral authority' ya kuikemea serikali ya CCM kuhifadhi watu wanaoharibu, kukiuka taratibu na hata kuleta ubadhirifu kwa umma ni kumuondoa Juliana.

Hakuna short cut katika hili. Ametoa taarifa isiyo na shaka kuwa kuna jambo nyuma yake. Juliana ameonyesha Kiburi, upungufu na kutowajibika kama kiongozi. Kumuacha ni kuvuruga CDM. Hili ni angalizo muhimu sana.
 
Back
Top Bottom