macho_mdiliko
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 21,791
- 39,584
Lakini huyu mwana mama nae mwambieni atulize mapepo yake. Kama aliona mwenyekiti amepotoka kwanini yeye azidi kuleta matatizo? Nae ni kicheche tu. Ni kundi moja na wewe na Zitto.Absolutely Candid scope,
actually kuna mahali nimesema hivi..
I Expected BAVICHA cadres and organs to organize more activities with more appeal to young citizens, and strengthen the youth council's construction to increase the council's influence among Tanzanian's youth.Petty squables are not healthy.
Tarehe 28/5/2012(jumatatu ijayo) Baraza la vijana Chadema Taifa linamaliza mwaka mmoja tangu lichaguliwe.
Nategemea wiki hiii itakuwa ni wiki maalumu kwao katika kujitathmini kwamba ndani ya Mwaka mmoja BAVICHA imefanya nini.
Nilikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kabisa kutoa tahadhari.JF haikuwa Hewani lakini waliokuwa wanachama wa JF facebook tulijadili.Nilisema Shibuda hastahili kujibiwa.Anastahili kuachwa tu bila kujibizana nae kwenye media kwani huo ndiyo mchezo anaoutaka.Anataka kupandishwa chati kisiasa(najua kamanda shibuda ni member wa hapa JF unachungulia humu).Ulichungulia humu hata nilipokuwa nakutolea mfano kuhusu mtizamo wangu na cross-carpeting za wanasiasa kutoka chhama kimoja kwenda kingine.Nilisema bila darasa la Itikadi hapa itakuwa kazi kweli kweli.Itabidi kuwe na timua timua za ovyo kwenye vyama vya siasa.
Akiwa CCM alitangaza kugombea Urais kupambana na Jk mwaka 2010.Hakuna mwana-CCM makini aliyemjibu isipokuwa Mzee Makamba aliyeapa kwamba yupo radhi kwenda Jela kuliko kuruhusu upinzani dhidi ya JK,2010.mnalijua hilo,linajulikana
The best way to deal with comrade Shibuda is to ignore him.
Makosa yanafanyika pamoja na kwamba ni demokrasia lakini utani mwingine ni gharama kweli kweli.Huwezi kutangaza kugombea Urais Chadema halafu ukataka meneja kampeni wako awe mwenyekiti wa CCM halafu tukuchukulie mtu serious.Haya ni makusudi kwa kuwa Shibuda ni mzoefu wa michezo ya kisiasa na anajua analenga nini.
Hata mimi ningekuwa mwenyekiti wa vijana nisingevumilia kuona hili.
Sasa naamini hili suala litatauliwa kwa busara.Makamu Mwenyekiti Juliana Shonza ni kiongozi makini na shupavu kweli kweli.Ni kiongozi hodari.ni kiongozi adimu ambaye hawezi kupatikana kwingine isipokuwa ndani ya chadema tu.Anapenda kusema kile anachoamini.Nilipogombea uenyemkiti wa vijana huyu ndiye alikuwa chaguo langu.Aliniunga mkono na nilimuunga mkono.Sijawahi kutilia mashaka uwezo wake wa kuongoza.Kama kuna tatizo la flow of information nadhani tatizo hili litamalizika ndani ya vikao vya chama tu.It's not a big deal at all
Laiti tungekuwa na muundo kama wa ANC-YL ya Afrika Kusini basi leo tungekuwa na msemaji wa kama alivyo comrade floyd shivambu wa ANCYL.Mabaraza yote na jumuiya zote za vijana ndani ya vyama vya siasa Tanzania hatuwa na muundo kama huo kitu ambacho kinaweza kutoa mwanya kwa vijana kujikanganya au kuburuzana katika uendeshaji wa shughuli za kila siku kisaiasa na pengine hata maadui wa demokrasia kutumia mwanya huo kuleta mvurugano.
Naamini Baraza la vijana,litamaliza tatizo hili.Tusiwe na papara za kuhukumu watu.Tuwe na subira,tusikurupuke.Diplomasia na Busara inahitaji kutumika hapa.This is the right time to show leadership.
Malumbano ya watu binafsi yasiharibu taasisi.Shutuma kwamba Baraza la vijana ni wahuni hazivumiliki