Viongozi chadema angalieni hili

kipuyo

JF-Expert Member
Jul 30, 2009
1,785
1,464
Nikiwa mmoja wa wapenzi na mashabiki wakubwa wa mabadiliko makubwa kwenye nchi hii,naomba nichukue nafasi hii kutoa ushauri wangu kwa viongozi watendaji wa chama kinachoelekea kutupeleka kwenye mabadiliko ya kweli( namaanisha CHADEMA).Ushauri wenyewe ni huu hapa

  • Kwa kuwa ruzuku ipo andaeni vipindi maalum angalau mara moja kwa wiki kwenye vituo vya televisheni na redio vyenye wasikilizaji kwenye maeneo mengi ya nchi.Vipindi hivi viwe vya kuelezea kwa kina sera na mlengo wa chama chetu.Hii itarahisisha sana uenezaji wa chama katika maeneo mbalimbali na pia itapunguza sana kazi ya kueleza ilani ya chama wakati wa chaguzi mbalimbali.
  • Kuandaa tafiti mbalimbali katika maeneo tofauti hapa nchini juu ya hali halisi ya kukubalika kwa chama na masuala mengine muhimu kwa mustakabali wa chama chetu.Tafiti hizi zifanywe na vijana wanaharakati kutoka vyuoni.
  • Kuhakikisha kuwa kwenye bajeti ya chama kwa mwaka wa fedha 2012/13 mojawapo ya shughuli yake ni kuwapa mafunzo ya uongozi wale wote waliojitokeza kuipigania CHADEMA kwenye uchaguzi wa mwaka jana.Hii ni kwa wale ambao wanaendelea kuitumikia chama vyema katika maeneo yao na itasaidia sana kuwafanya wasikate tamaa.
  • Kuandaa operesheni za chama kwenye kila kanda itakayoongozwa na vijana wanaharakati kutoka kwenye mikoa husika wakisaidiana na baadhi ya viongozi kutoka kwenye kamati kuu na
  • Kukumbuka kufanya mikutano ya kuwashukuru wapiga kura popote pale uchaguzi utakapofanyika hata kama CHADEMA hawajaibuka washindi.
Ahsante kwa kutopuuza
 
Mawazo mazuri. Ila wasiwasi wangu ni hawa watanzania wasivyo na elimu ya Uraia. Utatumia mbinu zote hizo halafu mzee wa mamvi anatinga na TShirts na kofia za kijani na anashinda uchaguzi
 
Mawazo mazuri sana kwa uongozi wa chadema. Yafanyiwe kazi kwa mustakabali mwema wa chama.
Naunga mkono mawazo haya kwa asilimia mia.
 
mkuu umeua nyok kwa kumpiga kunako kwa kichwa, bravo kwa sana mkuu!
 
Back
Top Bottom