fyddell
JF-Expert Member
- Dec 19, 2011
- 11,072
- 19,865
Duu Mazizi mazuri kiliko hata baadhi ya madarasa mengi nchini wanayosomea wanafunzi/watoto wetu
Umeniwahi mkuu. Hii kitu inasikitisha sana.
Duu Mazizi mazuri kiliko hata baadhi ya madarasa mengi nchini wanayosomea wanafunzi/watoto wetu
Sitakuwa na muda wa kukueleza kila kitu hapa. Ila waweza kufunguka macho kwa kusikiliza mara kwa mara RTD na kuangalia TBC1. Kuna vipindi vizuri sana vya mafanikio yetu kwenye kila nyanja ikiwa ni pamoja na kilimo. Utashangaa kwamba tumepiga hatua sana na dunia inasifia maendeleo yetu hususan kwenye kubadilisha kilimo.
Kama huoni alichofanya..... basi, inawezekana una macho lakini hayaoni.
Huyo jamaa mtoa tuzo ametoka wapi? Naona alianza na Inkosikati Ntombi kisha akaenda kwa viongozi wa Afrika kusini mwa jangwa la sahara. Asije akawa anainyemelea ardhi au asije akawa ndiyee muuza matrekta yale ya Kihindi.
Ukiwa kilaza ua rahisi kuchezewa jua utachezewa na kila tapeli.Hili ndilo tatizo tulilo nalo hapa Afrika. Watawala wetu wanapenda sana madaraka na sifa kiasi cha kujikuta wakinaswa na kila aina ya tapeli. Huyu mhindi si angepeleka tuzo yake kwao India kama siyo kutafuta kuwa karibu na Kikwete ili amtumie vibaya?