Vincent Nyerere and Deo Filikunjombe

Mjenda Chilo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
1,467
513
Mh.Fuli amekomaa na isue ya TBS, na ameenda mbali na kutamka bila kupindisha maneno kuwa mawaziri ni wezi, Mh Lukuvi akaomba mwongozo wa spika eti mawaziri si wezi, mh akakomaa kuwa ana ushahidi wa huo wizi ghafla spika akaahirisha kikao mpaka jioni hii.

Inasemekana CCM walikuwa na kikao cha dharura mchana huu. Mh. yale magoti uliyopiga kuomba kura hiyo ndo kazi tuliyokutuma. Usimuogope mtu waTz kibao tuko nyuma yako na kama ni chama basi utamconsult Milya akuonyeshe njia. utamu huu!
 
Taarifa kutoka ndani ya kikao cha CCM zinadai kwamba tayari Mhe. Filikunjombe ametaja majina ya mawaziri wezi wa mali za umma. Kuna uwezekano kwamba majina hayo yakawekwa bayana kwenye kikao cha jioni. Bado haijawa wazi. Hata hivyo inasemekana ametaja machache na kusema bado ana majina mengine lakini anaendelea kukusanya ushahidi.
 
swafi hiyoo! asiogope hakuna chama dola tena, wakimzingua kwa uwezo aliouonyesha atarudi tu bungeni tena akiwa na chama safii!
 
Taarifa kutoka ndani ya kikao cha CCM zinadai kwamba tayari Mhe. Filikunjombe ametaja majina ya mawaziri wezi wa mali za umma. Kuna uwezekano kwamba majina hayo yakawekwa bayana kwenye kikao cha jioni. Bado haijawa wazi. Hata hivyo inasemekana ametaja machache na kusema bado ana majina mengine lakini anaendelea kukusanya ushahidi.


tutayapata muda simrefu hivyo vipande vya keki walivyomega
 
Ni kweli wamedhamiria kujisafisha? au ni changa la macho tunapigwa tu watz, kashifa ngapi zilizoibuliwa na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya watumiwa?
 
taarifa kutoka ndani ya kikao cha ccm zinadai kwamba tayari mhe. Filikunjombe ametaja majina ya mawaziri wezi wa mali za umma. Kuna uwezekano kwamba majina hayo yakawekwa bayana kwenye kikao cha jioni. Bado haijawa wazi. Hata hivyo inasemekana ametaja machache na kusema bado ana majina mengine lakini anaendelea kukusanya ushahidi.
kamata wezi meeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeen!
 
Filikunjombe Watanzania wengi wanakuangalia,na wako nyuma yako sasa,umekua mfano wa jinsi ya wabunge wengine wa c.c.m wanavyotakiwa kua,wasiende kukunyamazisha kwenye kikao chenu cha chama,kama wakitishia kukuvua uanachama milango iko wazi kwa vyama vingine kama cuf,tlp,cdm na kadhalika!taifa kwanza
 
kaza buti mh tunaamini Mungu anaweka maneno kinywani mwako
ili ukombozi uingie tanzania, usiogope kufukuzwa chama kwa ajili ya kulinda
matumbo ya wachache, dhambi yao itawatafuna hadi wajukuu
 
Mheshmiwa namkubali sana ndo viongozi tunaowataka karne hii.Tunamsupport kwa hali na mali piga kazi mkuu
 
Wanamjua au wanaambiwa? kasotea sana ubunge huyo na ana usongo nao kiukweli. Na kwa mila za watu wa kule kwao hakunaga kurudi nyuma hadi kieleweke. huyo ni Mnjombe wa kuludewa bwana.
 
Naona hoja nzito alizotoa Vicent Nyerere ni nzito sana kwa Chami na Deo Filikunjombe amegusa kwa Mkullo mwanachama mwenzake wa CCM
 
Nadhani tukiacha au kupunguza kuside na watu fulani, tukaweza kujoa kwenye kujiunga na makundi yoyote, tutakuwa huru, tutaweza kupambanua hoja badala ya kutafuta hoja kwenye pumba za 'watu wetu' au kuziba masikio hoja zilizotolewa na 'wasio wetu'
 
Naona hoja nzito alizotoa Vicent Nyerere ni nzito sana kwa Chami na Deo Filikunjombe amegusa kwa Mkullo mwanachama mwenzake wa CCM
Jamani kweli vijana ni kiboko cha wezi ,mafisadi, majahilri. NIMEMSIKILIZA VICENT NA FILIKUNJOMBE wamesema kwa uzalendo na data waziwazi wazee wamebaki kushika tama kunjombe hama haraka uje cdm ili moto uliouwasha usizimwe na ccm na vikao vya siri

vicent anasema magari hayakaguliwi , yanatozwa na kuuziwa certificates na kampuni za ukaguzi si za nje ni watoto wa mjini hapahapa FILIKUNJOMBE anasema mkulo ni mwizi , fisadi , analila taifa ni mlafi anakula bila kunawa. NGOJA TUONE CCM WATACHUKUA HATUA GANI
 
Ni aibu kubwa sana kwa Pinda, Chami na hata William Lukuvi ambae yupo Bungeni kufichaficha mambo ya Serikali
 
Deo Filikunjombe:Nimekukubali japo mimi siwapendi magamba.Nimekusikiliza tangia asubuhi na jioni hii kweli unadhamira ya kweli,ila huwezi kujifuta kwa kutumia taulo ukiwa ndani ya maji,ww ni mpiganaji mzuru na jasiri huko hakukufai chukua magwanda au kama hutaki magwanda nenda NCCR.
 
Filikunjombe asipoangalia yatamkuta ya Mwakyembe muda si mrefu... Anatakiwa kutoka kwenye lile Genge la wahuni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom