Vincent Nyerere amstaafisha rasmi Ben Mkapa siasa

aache siasa amekosa mvuto amebaki kudanganya uma kwa uongo tu,mwambie akapumzike kwenye hekalu lake la lushoto,siasa imemshinda
 
Nifamilia ya Nyerere (Julius Kambarage Nyerere RIP) iliyomweka Mkapa ktk siasa, maana kabla ya kuwa Raisi Mkapa hakujulikana, Na familia hiyo hiyo(Vicent Nyerere) ndio imemrudisha alikotoka.

Mavumbini tulitoka hakika mavumbini tutarudi! Go Mkapa
 
Inawezekana huu mwaka wa 2012 ndio mwisho wa Ben Mkapa kisiasa na hata ndio mwanzo wa kuporomoka kwa umaarufu na heshima miongoni wa Watanzania..,Ben Mkapa ulikuwa mwiba mkali uliowashinda Agustino Mrema,Ibrahim Lipumba,James Mbatia lakini kijana mdogo toka kule Musoma Mh.Vincent Nyerere ameweza kuumeza mfupa uliowashinda wapinzani wengi baada ya kumpa Ben Mkapa vidonge stahiki wakati wa Kampeni Arumeru hadi kufikia hatua ya kuhaha kwa ndugu wa nyerere kuomba msamaha...! Namfananisha Vincent Nyerere na David aliyemwangua Goliath (ben mkapa) kwenye mapambano..., Nafikiri kazi aliyekuwa nayo sasa hv Ben Mkapa ni kurudi tu kijijini kwao Mtwara kufanya shughuli za kilimo kama wastaafu wenzake..Baada ya kupata mbabe wake kwenye uringo wa siasa

Anko BEN kamasi zilimtoka.. Vincent Nyerere chiboko bwana!
 
Mh. Nasari,MUNGU NI MWENYE NEEMA NA REHEMA,MTUMAINI YEYE SIKU ZOTE,HATA DAUDI ALIKUWA KIJANA,NA YERUSALEM UKAITWA MJI WA DAUDI .USITISHWE NA FISADI YOYOTE,TUPO PAMOJA NA WEWE KIROHO.MTUMAINI BWANA UTAISHI...peoples pow....er. AMEN.
 
Mkapa alipaswa kuwa jela na sio kwenye majukwaa ya siasa.

Kusema Mkapa kastaafishwa mi nadhani ni kupotoka kidogo, huyu mzee kaifisadi nchi hii na kuiingiza kwenye levels nyingine za matatizo. Tusimpe heshima asiyestahili heshima.

Bado natamani na kusubiri kuona siku hawa "watawala" wakisimama mahakamani kama Mubarak, Saddam na Taylor.
 
Nifamilia ya Nyerere (Julius Kambarage Nyerere RIP) iliyomweka Mkapa ktk siasa, maana kabla ya kuwa Raisi Mkapa hakujulikana, Na familia hiyo hiyo(Vicent Nyerere) ndio imemrudisha alikotoka.
....alie kupandishe ndiyo atakae kushusha....
 
hilo dubwana halikaagi tena mtwara,lilipoolewa na mama wa kimachame hata huko kwao huwa linakaa hata miaka tano bila kufika kule,chezea machame wewe?pale hana lwake aki nyanyua mdomo tu anakula mboko zakutosha,unakumbuka alishavunjwa mguu na yule mama kwa kipigo takatifu.hana lolote huyo mtu wala mchango wowote kwa taifa kwa sasahivi.siku tunachukua nchi magereza itajaa hao majizi mnayoyaita wastaafu
 
wanafamilia wanagombana ushabiki wa nini. nawasihi baada ya kutofautiana hadharani warudi ngazi ya familia wakapate suluhu
 
hapa si chadema na ccm au suala la vincent na mkapa ni suala familia siasa zinaingia vipi
 
ovu moja tu hutosha kuufuta wema wa miaka yote,sioni alichokifanya mkapa tena,
ameyataka mwenyewe tuyaseme haya hatuogopi tena vitisho vyao,
 
inawezekana huu mwaka wa 2012 ndio mwisho wa ben mkapa kisiasa na hata ndio mwanzo wa kuporomoka kwa umaarufu na heshima miongoni wa watanzania..,ben mkapa ulikuwa mwiba mkali uliowashinda agustino mrema,ibrahim lipumba,james mbatia lakini kijana mdogo toka kule musoma mh.vincent nyerere ameweza kuumeza mfupa uliowashinda wapinzani wengi baada ya kumpa ben mkapa vidonge stahiki wakati wa kampeni arumeru hadi kufikia hatua ya kuhaha kwa ndugu wa nyerere kuomba msamaha...! Namfananisha vincent nyerere na david aliyemwangua goliath (ben mkapa) kwenye mapambano..., nafikiri kazi aliyekuwa nayo sasa hv ben mkapa ni kurudi tu kijijini kwao mtwara kufanya shughuli za kilimo kama wastaafu wenzake..baada ya kupata mbabe wake kwenye uringo wa siasa

wala sio mtwara siku hizi anaishi lushoto kwa kina mzee makamba kajenga kulee
 
huyu mzee aliyataka mwenyewe...may be anabembeleza wasimgeuke kwa maovu aliyofanya
tuna wazee wengi wamebaki na legacy yao coz hawashiriki haya mambo like mkapa..think of warioba,salim,mwinyi
 
Ubabe wa Mkapa kwa kweli unaniudhi sana sana! Wakati wa utawala wake kidogo aue upinzani kabisa Tz, alikuwa mbabe, dikteta na fisadi mkubwa. Alithubutu kufanya biashara kwa anuani ya Ikulu bila ya soni wala aibu yoyote! Asante sana Vicent kwa kumsaidia kujijua yukoje.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom