mkomatembo
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 1,477
- 816
DAh! inasikitisha sana! sana mpaka nimetaka kulia ! watoto walimkosa nini lakini? kuna watu wakatili duniani! hata hivo hongera mkuu kwa kisa hiki !
sad story ever
Mkuu Mtambuzi pamoja na ugumu wa ushahidi wa kumtia hatiani Vincent brothers lakini hapa unaona namna utaalamu wa kisayansi unavyofanya kazi.
Changamoto kubwa kwa wapelelezi wetu wa jeshi la Mwema ni upatikanaji na matumizi ya sayansi katika kutafuta na kupata ushahidi.
Nina uhakika hapa kwetu kuna kesi za namna hii nyingi sana lakini wahusika wako nje wanadunda bila wasiwasi, kwakuwa pamoja na kutokuwa na uwezo wa kisayansi wa kufanya utambuzi, hata rushwa nayo imewafanya wapelelezi watindikiwe weledi katika kazi zao.
Mwita Maranya ............... Nimeisoma kwa makini sana hii kesi kabla sijaiandika, kwa kweli wenzetu wana kitu wanaita Attention to the details, Wenzetu huwa hawapendi kushindwa na wana kitu wanaita kukamia yaani mpaka kieleweke. Mwanamke kama Lisa Green ni mfano wa kuigwa, hakuichukulia hii kesi kwa pupa na kwa kushirikiana na FBI walitumia miaka mitatu mizima wakikusanya ushahidi ambao ndio uliomtia huyu jamaa hatiani.............Mkuu Mtambuzi pamoja na ugumu wa ushahidi wa kumtia hatiani Vincent brothers lakini hapa unaona namna utaalamu wa kisayansi unavyofanya kazi.
Changamoto kubwa kwa wapelelezi wetu wa jeshi la Mwema ni upatikanaji na matumizi ya sayansi katika kutafuta na kupata ushahidi.
Nina uhakika hapa kwetu kuna kesi za namna hii nyingi sana lakini wahusika wako nje wanadunda bila wasiwasi, kwakuwa pamoja na kutokuwa na uwezo wa kisayansi wa kufanya utambuzi, hata rushwa nayo imewafanya wapelelezi watindikiwe weledi katika kazi zao.
Mwita Maranya ............... Nimeisoma kwa makini sana hii kesi kabla sijaiandika, kwa kweli wenzetu wana kitu wanaita Attention to the details, Wenzetu huwa hawapendi kushindwa na wana kitu wanaita kukamia yaani mpaka kieleweke. Mwanamke kama Linda Green ni mfano wa kuigwa, hakuichukulia hii kesi kwa pupa na kwa kushirikiana na FBI walitumia miaka mitatu mizima wakikusanya ushahidi ambao ndio uliomtia huyu jamaa hatiani.............
Hebu jiulize... Mtu anadai hakuwahi kutoka nje ya jimbo la Ohio na ana ushahidi wa risiti za manunuzi aliyoyafanya wakati mauaji yanatokea........ Isitoshe ana maelezo kwamba alihusika na ajali ndogo akiwa hapao Ohio siku hiyo ya mauaji........... kama ingekuwa ni hapa kwetu tungesema "Dismiss a case" lakini kwa wenzetu mambo ni tofauti sana.................
Kisa cha kusikitisha
FirstLady1 ................Sijui hata hao wanawake walikuwa wanampendea nini.........!?very sad story vicent alikuwa na wanawake kama mabehewa ya treni
Haswa na wahakikishe kila jambo wanalifuatilia hadi mwisho wake na kuweka record zinazoweza kubaini wahalifu halisi!Mimi ni Ex mpelelezi na niliacha hiyo kazi kwa zengwe. Nimevutiwa sana na kesi hii na kwa wapelelezi wetu kuna kitu cha kujifunza. Pamoja na yote haya serikali inapaswa kuwajengea uwezo wapelelezi wetu na vifaa vya upelelezi viweze kuboreshwa zaidi ili haki iweze kutendeka kwa wakati
Mwita Maranya, Mkuu wangu tuna nchi ya ajabu sana... wakati dunia inaenda mbio na sayansi na teknolojia sisi bado tunalia-lia eti nchi changa!Changamoto kubwa kwa wapelelezi wetu wa jeshi la Mwema ni upatikanaji na matumizi ya sayansi katika kutafuta na kupata ushahidi.
jouneGwalu ......... Nimependa sana maoni yako........... Nilikuwa nasita kusema hilo, lakini nimefurahi hatimaye ametokea mtu aliyeona nje ya box.............. Ile sababu ya kwamba Motive ilikuwa ni kuuwa familia yote ili aondokane na mzigo wa financial suport kwa familia yake ina mapungufu........ Inawezekana ni kweli aliuwa lakini upelelezi uliomtia hatiani ulikuwa haujajitoshleza...........Ni pale atakapokamatwa mtu mwingine ndipo atakapokuwa hana hatia machoni mwa watu.............Mtambuzi
Binfsi namlaani sana huyo muuaji pia mauaji ya vitoto ndio imeniuma sana juzi nilishindwa kuendelea kusoma nilipofika ile part ya mtoto Marquez Harper jinsi alivyouawa nikawa na-imagine jinsi uchungu alioupata hadi kakajing'ata vidole dah machozi yalinitoka kwa kweli, pia ako ka Lyndsey jamani vitoto vizuri sana mtu wa kawaida unawezaje kuua hao malaika hivyo??
Ila kwa kuwa fair zaidi na kwa jinsi kazi za upelelezi zinavyoenda ni dhambi sana kumhukumu tena kifo Vicent kwa mazingira tu!
Hao wapelelezi wamechemka sana, binafsi nimeisoma hii stori toka juzi bado sioni uhusika wa moja kwa moja wa Vicent kwa kupitia upelelezi yakinifu, unajua ninachomaanisha ie kushindwa kupata DNA, alama za vidole vya muuaji, bastola iliyoua na video za kwenye petrol stations ni upungufu mkubwa sana jamani.
Amehukumiwa kwa hisia tu...
Ila huo utitiri wa wanawake aliowapitia kweli Brothers ni soo hata akifa ana hadithi ya kusimulia huko aendako lol