Vinara wa DECI warejeshwa rumande

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,706
155,270
VINARA wa upatu wa Development Enterpreneurship Community Initiative (DECI), wataendelea kusota rumande hadi Februari 8, mwaka huu, kwa kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Watuhumiwa hao, Jackson Mtares, Dominick Kigendi, Timotheo Ole Loitg'nye na Samwel Mtares, wamewasilisha rufaa yao leo asubuhi kutokana na kunyimwa dhamana.

Watuhumiwa hao wapo mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu Aloyce Katemana na Mwendesha Mashitaka Beatrice Mpangala.

Awali imedaiwa kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na makosa ya kula njama, kughushi na kujaribu kuiba sh milioni 118,440,000, mali za wanachama wa DECI kati ya Desemba mosi na 8, mwaka huu.

Imedaiwa kuwa wakurugenzi hao walikamatwa wakiwa na fedha hizo mali ya wanachama wa DECI, katika tawi la Benki ya Standard Chartered tawi la Kariakoo Desemba mwaka huu.

Katika masharti ya dhamana yao ya awali washitakiwa hao ambao ni vigogo wa DECI walizuiwa kufanya shughuli yoyote inayoendana na kampuni hiyo.

Katika kesi ya awali washitakiwa hao walifikishwa kizimbani hapo Juni 12, mwaka huu, ambapo wakurugenzi hao wa DECI, Mhasibu na Msemaji wa kampuni hiyo, Alborgast Kipilimba, walipandishwa kizimbani mahakamani hapo kujibu mashitaka ya kuendesha na kusimamia mradi wa upatu na kupokea amana kutoka kwa umma bila ya leseni.

Katika kesi hiyo iliyopo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema, wanadaiwa kuwa tarehe tofauti kati ya mwaka 2007 na Machi 3, mwaka huu, katika Makao Makuu ya Kampuni hiyo ya DECI Tanzania Ltd, Mabibo Mwisho, Dar es Salaam na maeneo mengine nchini waliendesha na kusimamia mradi wa upatu.

Inadaiwa kwamba walifanya hivyo kwa ahadi ya kuwapa matumani wananchi kupata fedha nyingi zaidi.

Katika mashitaka ya pili wanadaiwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2007 na Machi mwaka huu, Makao Makuu ya DECI Mabibo Mwisho, Dar es Salaam na maeneo tofauti nchini walipokea amana kutoka kwa umma bila ya leseni.

Wakati huohuo, kesi ya watuhumiwa wa wizi wa zaidi ya sh milioni 70 kwa kutumia kadi feki za kutolea fedha benki (ATM), Nedko Stanchen (34) na mkewe Stella Nedelcheva (28), raia wa Bulgaria imeshindwa kusikilizwa kutokana na kusekana kwa mkarimani.

Watuhumiwa hao walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi, Warialwande Lema, ambapo Mwendesha Mashitaka ni Edger Luoga.

Washitakiwa hao wapo nje kwa dhamana ya sh. milioni 21 kila mmoja.

Pia washitakiwa hao wanatakiwa kutosafiri nje ya Dar es Salaam bila kupata kibali cha Mahakama na wawasilishe hati za kusafiria ambapo wametakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili.

Washitakiwa hao Nedko na mke wake Stella wanakabiliwa na mashitaka matatu ya wizi wa sh milioni 70 katika tawi la Benki la Barclay's.

Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa Julai mwaka huu waliiba katika mashine za kutolea fedha za ATM sh milioni 14.5 mali ya Baclays.

Wazungu hao wanatetewa na wakili, Alex Balomi ambapo awali iliambia mahakama kuwa wateja wake hawaelewi lugha iliyotumika kuwasomea mashitaka ambayo ni ya Kiingereza na wanaomba wapatiwe dhamana.

Washitakiwa walikana mashitaka na kesi hiyo itatajwa tena Machi mosi mwaka huu.
 
Back
Top Bottom