Vilio, simanzi vyatawala kumuaga MJAZITO ALIEUWAWA NA MAJAMBAZI-Jackline

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,138
Vilio, simanzi vyatawala kumuaga Jackline

na David Frank, Arusha

amka2.gif
VILIO, simanzi na kwikwi jana vilitawala karibu nusu saa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Selian, mjini hapa, huku baadhi ya waombolezaji wakizimia ovyo katika tukio la kuaga miili ya marehemu Jackline Minja (27) na mwanaye aliyetolewa tumboni kwa njia ya upasuaji baada ya kifo kilichotokana na kupigwa risasi na majambazi.
Marehemu Jackline aliuawa mwanzoni mwa wiki hii akiwa na ujauzito wa miezi nane ambapo madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Selian walimfanyia upasuaji.
Vilio hivyo vilianza mara baada ya miili hiyo kutolewa nje ya chumba cha maiti na kulazwa nje huku mtoto huyo akiwa pembezoni mwa mwili wa mama yake.
Baadhi ya kina mama ambao ndio wengi waliokumbwa na hali hiyo walisikika wakigugumia na kulia huku wakihoji kwamba mtoto huyo alikuwa na kosa gani hadi auawe wakati hakuwa na hatia.
Mwili wa Jackline ulisafirishwa kwenda nyumbani kwao kwa mazishi katika kijiji cha Rawiya, Marangu Moshi.
Marehemu Jackline akiwa anaingia nyumbani kwake saa 3.30 usiku Jumanne iliyopita akiendesha gari aina Toyota Nadia T 125 AUW alivamiwa na watu wawili waliokuwa na pikipiki ambapo mmoja alimfuata upande wake na kuhoji alikokuwa mumewe Deo Minja ambaye ni mchimbaji wa madini katika mgodi ya Tanzanite Mererani wilayani Simanjiro.
Siku ya pili baada ya tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Basilio Matei, aliwaambia waandishi wa habari kuwa jeshi hilo limefanikiwa kuwaua kwa kuwapiga risasi watu wawili waliohusika na kifo cha Jackline. Aliwataja majambazi hayo kuwa ni Gilbert Charles (32) na Deus Dossa ambao waliuawa baada ya kurushiana risasi na polisi katika eneo la Soweto.
 
Basilio Matei, aliwaambia waandishi wa habari kuwa jeshi hilo limefanikiwa kuwaua kwa kuwapiga risasi watu wawili waliohusika na kifo cha Jackline. Aliwataja majambazi hayo kuwa ni Gilbert Charles (32) na Deus Dossa ambao waliuawa baada ya kurushiana risasi na polisi katika eneo la Soweto.

Hivi kwa nini jeshi la polisi Tanzania kila mara wao wana "shoot to kill" badala ya kuwapiga majambazi risasi sehemu ambazo hazitasababisha kufa kwao ili waweze kuwahoji?

Au kuna mambo wanakuwa hawataki yatoke/ yathibitike hadharani?

Manake ni mara chache sana unasikia eti majambazi yamekamatwa Tanzania!!

Poleni sana wafiwa
 
So sad, jamani cku hizi mwanadamu ni wa kumuogopa kama simba vile, hata wanyama wamekuwa waastarbu kuliko mwanadamu tunaenda wapi? ebu ona sasa mtoto asiye na hatia jamani I cant continue................RIP Jackline and baby.
 
Hivi kwa nini jeshi la polisi Tanzania kila mara wao wana "shoot to kill" badala ya kuwapiga majambazi risasi sehemu ambazo hazitasababisha kufa kwao ili waweze kuwahoji?

Au kuna mambo wanakuwa hawataki yatoke/ yathibitike hadharani?

Manake ni mara chache sana unasikia eti majambazi yamekamatwa Tanzania!!

Poleni sana wafiwa

Ndo hapo sasa tutaaminije kuwa wao ndio waliofanya tukio hilo?

RIP marehemu na pole kwa wafiwa
 
hawa mapolisi ni wahuni kabisa;;
huyu basilio mtei atueleze lile tukio la wiki iliopita
walipiga wezi wakampiga askari mmoja mkono wengine wakauwawa
akaenda kwake akachukua familia akakimbia atueleze yuko wapi??
 
Mhh!!! sijakupata uzuri hapa; yaani nani ailkimbia na familia mwizi ama askari? Waweza rudia hii?

Nimesikitishwa na upotevu wa Maisha ya Jackline na mwanawe! Na nimesikitishwa zaidi na namna wanausalama walivyo handle hii issue! hatutakaa tujue na tutabaki na speculations tu!
 
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi-Amen
Wiliofanya unyama huu wataipata hukumu yao hapahapa duniani.
 
R.I.P Jack, tumesononeka sana hasa kichanga ambacho kilikuwa kimebakiza takribani siku 30 tu kije duniani kwetu, hakina kosa lolote

Jamani kwa upande wa pili - kama haya majambazi hayakuiba gari/ pesa wala chochote kwa marehemu basi hapo itakuwa ni kitu cha kufikiria sana ambocho ni kazi ya police.

kwetu sisi wana jamii tujiangalie mienendo yetu jamani - unaweza kuuingiza familia yako kwenye matatizo makubwa kama unafanya kazi zizizokuwa na kichwa wala miguu (Illegal business zina madhara yake)

ni vigumu sana mtu aje akupige risasi harafu asichukue chochote toka kwako aishie mmhh hapo kidogo utata.
 
Hivi kwa nini jeshi la polisi Tanzania kila mara wao wana "shoot to kill" badala ya kuwapiga majambazi risasi sehemu ambazo hazitasababisha kufa kwao ili waweze kuwahoji?

Au kuna mambo wanakuwa hawataki yatoke/ yathibitike hadharani?

Manake ni mara chache sana unasikia eti majambazi yamekamatwa Tanzania!!

Poleni sana wafiwa
Poleni sana wafiwa.
Polisi mara nyingine wanaua watu ambao wanahisi ni majambazi hata kama si jambazi wanabambikiza tu kuwa walikutwa na silaha na walikuwa wanarushiana risasi na polisi. Kama wanarushiana risasi mbona hatusikii polisi amejeruhiwa. Mbona kesi ambazo wamerushiana risasi polisi nao wanaumia mfano ile ya Ubungo au ile ya njiro arusha?
Kuna jamaa yangu aliibiwa halafu akakamatwa mtu mmoja akaonyeshwa halafu akaambiwa kesho aje amtambue kuwa ni mojawapo wa wale majambazi waliomvamia. Yule jamaa yangu aliwaambia polisi kuwa yeye hawezi kudanganya na wale majambazi waliomvamia alikuwa anawakumbuka sura zao maana hawajaficha nyuso zao. Lakini bado polisi waliendelea kumcharge huyo jamaa kwa kesi ya kumbambikia kumbe tu walikuwa na mgogoro na polisi wenyewe. Polisi wetu hawako makini including hao wanaoitwa ma-RPC. Kama kweli wanauwa majambazi mbona majambazi wasipungue au ujambazi upungue hata kidogo. Naogopa kuwa polisi inawezekana wana attach wrong targets ili kuonyesha kuwa wanafanya kazi.
 
R.I.P Jack, tumesononeka sana hasa kichanga ambacho kilikuwa kimebakiza takribani siku 30 tu kije duniani kwetu, hakina kosa lolote

Jamani kwa upande wa pili - kama haya majambazi hayakuiba gari/ pesa wala chochote kwa marehemu basi hapo itakuwa ni kitu cha kufikiria sana ambocho ni kazi ya police.

kwetu sisi wana jamii tujiangalie mienendo yetu jamani - unaweza kuuingiza familia yako kwenye matatizo makubwa kama unafanya kazi zizizokuwa na kichwa wala miguu (Illegal business zina madhara yake)

ni vigumu sana mtu aje akupige risasi harafu asichukue chochote toka kwako aishie mmhh hapo kidogo utata.

Can you imagine, kama hawakuiba chochote, it means jamaa ndo alikuwa na maishu nao. unaweza kuta alimdhulumu mtu, tena mambo yenyewe ya tanzanite hayo. RIP jACK N BABY.
 
Mhh!!! sijakupata uzuri hapa; yaani nani ailkimbia na familia mwizi ama askari? Waweza rudia hii?

Nimesikitishwa na upotevu wa Maisha ya Jackline na mwanawe! Na nimesikitishwa zaidi na namna wanausalama walivyo handle hii issue! hatutakaa tujue na tutabaki na speculations tu!

...na unaweza ukakuta katika hao majambazi waliouawa hakuna hata mmoja aliyehusika na vifo vya marehemu hao. inawezekana waliohusika sasa ndio wako free kabisa kula nchi kwa raha zao! Inaudhi.
:mad:
 
...na unaweza ukakuta katika hao majambazi waliouawa hakuna hata mmoja aliyehusika na vifo vya marehemu hao. inawezekana waliohusika sasa ndio wako free kabisa kula nchi kwa raha zao! Inaudhi.
:mad:

Ni kweli, waliouawa sio waliohusika na tukio hilo. Huyo mama kauawa na genge la Justin Nyari, ana bifu na familia ya huyo mama. Anselm Minja ndiye ambaye duka lake lilivunjwa na genge la Nyari, na akakomaa nao hadi Nyari akafungwa kifungo cha maisha, lakini baada ya miaka 3 aliachiwa kwa kushinda rufaa. "Nyoka" wake aitwaye Banjoo bado yuko jela. Alipoachiwa alimtumia ujumbe Anselm kuwa lazima amfanyizie. Kwa kumjua Nyari alivyo mbaya, Anselm alifunga maduka yake yote akahama mji. Huyo Deo aliyefiwa mke ni mdogo wake. Yaani ni katika kumpelekea Minja maumivu hadi akome kuchezea 'wasioguswa'. Imesikitisha sana hii hali, lakini watu wanajua. Alikuwa anatafutwa Deo Minja auawe, lakini walipomkosa wakamalizia kwa mkewe ili maumivu yaifikie familia ya Minja.

Hakuna anayethubutu kumgusa Nyari hapa Arusha licha ya uhalifu wake wote kujulikana.
 
...na unaweza ukakuta katika hao majambazi waliouawa hakuna hata mmoja aliyehusika na vifo vya marehemu hao. Inawezekana waliohusika sasa ndio wako free kabisa kula nchi kwa raha zao! Inaudhi.
:mad:

ni kweli walieuwawa sio wao kabisa serikali kupitia jeshi la po;lisi wanawadanganya watu wamewauwa majambazi husika kumbe sio
waliouwa wako huru wanakula kuku zao kwa starehe

walaaniwe nyari familly
 
Back
Top Bottom