Vilaza ndio watu wa aina gani?

Kilaza ni neno lilokuwa linatumika University of Dar es Salaam miaka ya 90s na kuendelea (sina hakika na miaka ya nyuma zaidi) kumuidentify mwanafunzi mwenye uwezo mdogo darasani. Kinyume chake ni Kipanga.

Solidarity forever, and DARUSO members are strong!

Thank you ! Hujasema kinyume cha Kilaza ni Kiranga
 
"Kilaza" ni tafsiri SISISI ya neno la kiengereza "lay man" lenye maana - mtu wa kawaida, asiyekuwa mtaalamu.
Neno hilo limepanuliwa kimatumizi ili kukidhi haja ya watumia lugha kama watangulizi walivyoeleza maana yake.
Hivyo ukisema Malariasugu ni kilaza ina maana sio mtaalamu (hasa katika jambo analoliongelea).
Zaidi neno linaweza kuwa na maana kutokana na muktadha wa mazungumzo na kusudio lake!
 
Naomba mwenye kujua asili ya hili neno na historia yake atudadavulie sisi tulioliona jua juzi kati!
 
waliosoma Mlimani wanajua miaka ya 70s ( Kipanga Vs Kilaza) Kumbe mwalitumia bila kulijua. Je mnajua ni release ya MZEE PUNCH ya lini hehee. Muulize Mzee prof, Mukandara niye VC wa UDSM anajua au KIPANGA BANA!!
 
Jana luninga nyingi zilinukuu sehemu ya hotuba ya Rais anapotamka neno "kilaza".Azam Tv ilikuwa na muhutasari wa habari unasema "VILAZA MARUFUKU CHUO KIKUU",na ITV nao walikuwa na sehemu hiyo inayomnukuu Rais katika kuelezea uchungu wake wa vilaza kujiunga chuo kikuu,TBC nao hawakubaki nyuma,nao walielezea kwa undani hotuba ya Rais bila kuacha eneo alilowashutumu "Vilaza" wa UDOM.


Wanasema hii ndio asili ya neno "Kilaza",kwamba lilitokana na ushindani wa Wanamuziki kupiga gitaa,yule aliyejitamba kuwa anaweza kuliko mwenzake ndio alionekana hawezi kuliko.Tangu hapo neno "kilaza" likaasisiwa na kuchukua nafasi ya kumaanisha mtu mwenye uwezo wa chini.Miaka ya 1970 neno hili lilihamia katika viunga vya Chuo Kikuu Dsm(UDSM) na baadae kuhamia maeneo ya vyuo vikuu vingine Tz,na hatimaye neno "kilaza" likaingia katika msamiati wa kumaanisha "mtu asiye na uwezo wa kufanya jambo fulani".Bila shaka TUKI na BAKITA watalichukuwa na kuwa neno rasmi la Kiswahili maana hata Mkuu wa nchi amelitumia katika hotuba zake rasmi na litabaki katika kumbukumbu za hotuba zake.

Ama hakika Lugha huzaliwa,hukuwa na kufa.Hivi ndivyo Lugha inavyoendelea kukuwa na hakika kuna lugha nyingine hufa(dead language).Mfano wa "Lugha Mfu" ni Kilatini,japo kinaendelea kutumiwa kama Lugha ya "Kanisa Katoliki".Misamiati mingine ambayo imekuwa maarufu kutokana na majina ya waliofanya hayo matukio ni kama "Kihiyo"..."Masa..buli" na "Kitwanga"

Huku kwetu kuingia Bar na kuomba "Kitwa..nga" mbili za baridi imekuwa jambo la kawaida.Ama hakika Lugha hufa,hukuwa na kufa.Asante Mh Rais kwa kuendelea kukuza lugha ya Kiswahili
image.jpeg
 
**** jamaa mmoja alikuwa anaitwa Christopher juma kilaza ....alishindwa katika mashindano miaka ya 70.....ndo ikwa kilaza kilaza mpaka leo
 
Safi barafu umedadavua vema. Nilikuwa hasa namtafuta Juma Kilaza!
 
Back
Top Bottom