Vijipu ukeni

Mkomandaa

Member
Mar 14, 2011
58
18
Wana JF nawaslimu. Nimeishi na mke wangu kwa miaka 33 sasa na tumebahatika kuwa na watoto na wajukuu kadhaa. Kama miaka 5 iliyopita mke wangu alianza kupata vipele ukeni hadi kufanya ule mchezo wetu wa faraghani usiwezekane. Tumeenda hospitali tatu tofauti kwa vipimo. Nyakati zote ameambiwa mkojo wake ni mchafu na kupewa dawa. Ingawaje mimi sikuonekana na tatizo nilishauriwa nami nitumie dawa hizo kwa tahadhari na nikafanya hivyo. Miaka mitano ni mingi vipele ikawa siyo vipele tena ila ni vijipu. Mke wangu akisafiri mahala pa kukaa kiasi cha wiki mbili hivi vijipu ukeni vinapotea kabisa. Akinuia tu kurudi nyumbani niliko vijipu vinaanza usiku huohuo kiasi kwamba akifika nyumbani vijipu viko palepale na ile kazi haifanyiki. Nilifanya kama kumvizia akiwa kule mbali nikamkuta ni mzima wa afya. Kama nimefika asubuhi haifiki saa nane tayari vijipu vimeanza.

Nimehangaika hata kienyeji hakuna mafanikio. Naamini hapa jamvini kuna wataalaam wa fani zote. Naomba kujua ni ugonjwa gani huu ambao hauniambukizi mimi?. Na tiba ya ugonjwa huu ni nini?
 
Usijali mzee, nakuita hivyo kwan miaka uliyoishi na mkeo ndo yangu! "tunayaweza yote ktk yeye atutiae nguvu" Mungu haangalii dini wala kabisa ntakuombea na mtarudi tena kwenye furaha yenu.
 
Pole sana lakini usikate tamaa naamini watalaam watakuja halafu ufumbuzi utapatikana
 
Nadhani ni majaribu yakiimani unayapitia, pole sana ila usikate tamaa mtegemee mungu ktk kila jambo,
 
hii kidogo ni kali-kama akiwa mbali na wewe anapona-ukiwepo anavipata-
ngoja wataalamu waje wakupe data za haya mambo-POLE mkuu
 
Mzee chunguza wapi ulikosea uombe radhi km ni binadamu fanya hivyo haraka mzee. muombe Mungu atakuonyesha njia.
 
apo kuna nguvu za binadamu........jaribuni kumtegemea Mungu..jengeni imani iyo ww na mkeo na jaribu ilo mtalishinda...
 
pole sana kwa wakati huu mgumu kwako, labda mungu anakupa majaribu na wewe jitahidi huenda ukashinda
 
:lock1: Kigogo tatizo hili siyo ngoma (Ukimwi) kwani tumepima sote mara tatu tuko hasi (-ve) kabisa. Saidieni jamani nyumba yangu haiko kawaida.
 
Pole sana mkuu,
Wataalam watakupa ushauri, wapo hapa JF kibao.
Usisahau kuwawekea picha kamili, kwani itawarahisishia kazi.
 
kwani una nyumba ndogo? au kama hauna ku8na mtu alikutaka ukamkataa??? pole saNA KIKUBWA piga maombi sana kwa imani
 
Wana JF nawaslimu. Nimeishi na mke wangu kwa miaka 33 sasa na tumebahatika kuwa na watoto na wajukuu kadhaa. Kama miaka 5 iliyopita mke wangu alianza kupata vipele ukeni hadi kufanya ule mchezo wetu wa faraghani usiwezekane. Tumeenda hospitali tatu tofauti kwa vipimo. Nyakati zote ameambiwa mkojo wake ni mchafu na kupewa dawa. Ingawaje mimi sikuonekana na tatizo nilishauriwa nami nitumie dawa hizo kwa tahadhari na nikafanya hivyo. Miaka mitano ni mingi vipele ikawa siyo vipele tena ila ni vijipu. Mke wangu akisafiri mahala pa kukaa kiasi cha wiki mbili hivi vijipu ukeni vinapotea kabisa. Akinuia tu kurudi nyumbani niliko vijipu vinaanza usiku huohuo kiasi kwamba akifika nyumbani vijipu viko palepale na ile kazi haifanyiki. Nilifanya kama kumvizia akiwa kule mbali nikamkuta ni mzima wa afya. Kama nimefika asubuhi haifiki saa nane tayari vijipu vimeanza.

Nimehangaika hata kienyeji hakuna mafanikio. Naamini hapa jamvini kuna wataalaam wa fani zote. Naomba kujua ni ugonjwa gani huu ambao hauniambukizi mimi?. Na tiba ya ugonjwa huu ni nini?

Pole sana mkuu acha tuendelee kusikilizia wazoefu watupe data....
 
Kwanza pole sana kwa hayo matatizo,pili hebu kumbuka kabla ya tatizo,hukua na nyumba ndogo,?kwani nahisi ni mambo ya kibinadamu kwani yaweza ulimuumiza mwanamke uliyekuwa nae,nae akaamua kukukomoa kwa style hy...but zidi kumuomba mungu atakusaidia.
 
Ladyheart naona kama wewe umtabiri wa aina fulani. Nilikuwa na N-ndogo niliyoachana nayo 2008. Sijaonana nayo tokea wakati huo. Hivyo yaweza kweli kuwa kiini cha tatizo. Naomba ufunguke zaidi kuhusu ufumbuzi. Kumbuka mifano uliyopata kuiona au kusikia na kwamba walifanya nini nami nifuate nyayo huenda nikapata afueni. Maombi pia siachi. Ni vigumu kuishi ndani kama mgane.
 
Kwanza pole sana kwa hayo matatizo,pili hebu kumbuka kabla ya tatizo,hukua na nyumba ndogo,?kwani nahisi ni mambo ya kibinadamu kwani yaweza ulimuumiza mwanamke uliyekuwa nae,nae akaamua kukukomoa kwa style hy...but zidi kumuomba mungu atakusaidia.
Ndugu yangu salama? unachoelezwa na qiote hapa juu ni sahihi kabisa kuna mambo ya nguvu za giza hapa sio bure kwani huoni hakiwa mbali nawewe yuko salama? haujaeleza kama vinamsumbua kwa kumuuma maana naona inawezekana ni kukuzuia wewe usifaidi matunda ya ndoa yako. USHAURI kama unaweza angalia television ya "Emmananuel tv" tafuta kwenye mtandao SCOAN utapata watu ambao walikua na matatizazo kama hayo nao wamepona. KUMBUKA KUTENDA DHAMBI KUSIKUFANYE UMKIMBE MUNGU ILA MKIMBILIE MUNGU YEYE ANAKUPENDA UWE MZIMA. Kwake yeye aliye juu ni kazi rahisi.
 
Acha dhambi mkimbilie Yesu uokoke wewe na nyumba yako,huko ndiko kwenye uponyaji wa
ndoa yako
 
Back
Top Bottom