Vijiji vya Ujamaa vilivyokufa ni vipi?

Mkuu Mushi,

Hapo kwenye maneno niliyopigia mstari naomba nitofautiane na wewe. Ina maana wakulima wetu walipokuwa wanalima mazao ya biashara [pamba, mkonge, tumbaku, kahawa, chai, na pareto] walikuwa wanalima ili watumie wenyewe? Ni kwa vipi Ujamaa una-discourage export?

Kwanini shirika kama GAPEX na Vyama vya Ushirika vilianzishwa? GAPEX ilikuwa ina deal na exports za sector ya kilimo kama sikosei.

Ujamaa hauna uhusiano wowote na closed or open economy. nchi inaweza kuwa ya kibepari na bado ikawa closed. Kinacho-close/open economy ni tariffs pamoja na urasimu mwingine ndani ya nchi, na huo urasimu sio lazima utokane na Ujamaa. Marekani na Nchi zilizoendelea kila siku wakienda kwenye WTO nchi masikini zinalia kwamba hazina fair competition kwenye mazao yao ya kilimo kwa kuwa nchi tajiri zinatoa ruzuku kubwa kwa wakulima wao na hivyo wakienda kwenye soko la dunia wanavuruga bei na nchi masikini zinaishia kuuza kwa bei ya chini while wananunua pembejeo kwa bei kubwa sana, at the end of the day wakulima wa nchi masikini wanapata hasara.

Ninadhani tatizo kubwa liko kwenye marketing system ya mazao yetu. Wakati tunapata Uhuru, mkoloni aliacha marketing system ambayo ilikuwa ina-function vizuri. Wakati huo mazao ya biashara yalikuwa ni Kahawa, Chai, Mkonge, na Pamba; yalikuwa yanalimwa kwenye mashamba makubwa (plantations) ambayo yalikuwa yanamilikiwa na kampuni za nje. Kampuni hizo za nje ndizo ambazo zilikuwa zinafanya biashara ya ku-export hayo mazao, na kama kulikuwa na wazawa ambao walikuwa na vishamba vyao basi walikuwa wanaunza kwenye vyama vyao vya Ushirika kama KNCU, Nyanza, Ngoni-Matengo na vinginevyo, then hivyo vyama vya ushirika viliuza kwa hizo kampuni za wazungu.

Azimio la Arusha lilipokuja lilivunja hiyo marketing system na ku-introduce a new marketing system ambayo iliishia kuwaumiza wananchi kwa kuwapunja bei za mazao. GAPEX, Mamlaka za Mazao, Vyama vya Ushirika chini ya Ujamaa viligeuzwa kuwa miradi ya ulaji. Kuna kipindi Nyerere alivunja vyama vyote vya ushirika sababu ya huo ulaji na baadaye tena akaja kuvirudisha lakini vikawa chini ya CCM kama Jumuiya ya Chama [WASHIRIKA]. Kwa hiyo ni CCM ndiyo ambayo ilikuwa ina-impose viongozi wa hivyo vyama vya ushirika. Sasa kama CCM ndiyo ime-impose viongozi, je, viongozi wanawajibika kwa nani? Kwa CCM ama kwa wanachama wa chama cha Ushirika?

Baada ya kuanza kufuata mfumo wa soko huria [kama siyo soko holela], serikali imeshindwa kuweka marketing system ambayo inaweza kumpa mkulima bei nzuri. Ukifika msimu wa kuuza mazao inabidi serikali iweke masharti kibao as if wao walikuja kukupa pembejeo za bure. Mahindi nilime mimi, ikifika wakati wa kuvuna serikali inasema hakuna kuvuna mahindi mabichi, na hakuna kuuza mahindi nje ya Tanzania.

Nenda Karagwe, ukivuka mpaka ukaingia Uganda unakutana na bei nzuri ya kahawa kuliko ile ambayo unapewa na wanunuzi wa Tanzania. Mwaka 2003 nilikuta FFU wametanda mpakani kuzuwia kahawa isiuzwe Uganda, wakati huo vyama vya ushirika vya Karagwe na Bukoba vilikuwa hoi vikiwa havina hela na vinaomba mkopo toka CRDB ili vikanunue mazao hayo, na CRDB walikuwa wamegoma kutoa mkopo kwa kuwa hivyo vyama vya ushirika vilikuwa ni wadeni sugu na collateral walizokuwa nazo hazikuwa zina-qualify kupewa mkopo mwingine.

Je, ina maana Uganda wao huwa wanauza kwenye soko gani hiyo kahawa yao? Wakulima wakiacha kulima mahindi ama kahawa, utawalaumu? Je, exports za mazao zikipungua bado utasema ni sababu ya Ujamaa kwamba una discourage exports?

Keil,

Leo umeamsha munkari wangu.

Nitamuomba samahani Mzee Mwanakijiji kwa kutoka nje ya mada kidogo, kusogoa na Keil.

For the past 6 weeks I have been having a self debate about role of Party (TANU-CCM) and Government of Tanzania in solidifying poverty in Tanzania.

Mfano swali moja ambalo najaribu kuliundia hoja na hata kuanzisha thread ni kuhoji mfumo wa mapato ya serikali ya Tanzania.

Ukiangalia majedwali ya BOT hata bajeti, unakuta Serikali inaongea kwa HERUFI kubwa kuhusu mauzo ya mazao kama pato la Taifa. Lakini swali langu ni hili, ni kwa kiwango gani kipato hicho kwa uhalisi kinaenda kwa aliyevuja jasho? nikiwa na maana Mkulima?

Mpaka leo hii Mkulima wa Tanzania anapokea kama mapato si zaidi ya 15%-20% ya bei ya mazao yake. Kuna Serikali za vijiji, vyama vya ushirika, bodi za mauzo, wizara mama na serikali kuu ambazo kila moja inanyofoa shilingi zake kutoka bei ya Korosho.

Jiulizeni kama Mkulima angekuwa na uwezo kamili wa kujitafutia soko na kuuza anakotaka leo hii watu wa Vijijini wangekuwa wapi kimaendeleo?

Sasa hapa nitamjibu Zakumi na swali lake kuuliza tuonyeshe Mizania za Vijiji (balance Sheet).

Ikiwa Serikali inanyakua faida yote ya mazao na mkulima akija kupewa pesa yake kila mara he is breaking even (uwiano wa gharama za yeye kuzalisha na mapato ni sawa bila kuwa na faida ya kutosha au ziada), jitihada zake kusonga mbele zinabakia pale pale, ungetegemeaje yeye ajenge nyumba ya bati, achangie dawati au kuungana na kujenga hospitali?

Hivyo pamoja na kuwa tulipiga vita Unyonyaji, tuliruhusu unyonyaji wa Dola kupitia Chama cha Kisiasa na Serikali kuwa mmiliki na mnufaika mkuu wa mapato kwa kisingizo cha kujenga nchi (si kujenga Taifa, those are two different things)!

Ndio maana ukiwasoma CHADEMA na sera yao ya Majimbo wanadai kuwa kila wilaya itarejeshewa kwa kiwango kikubwa fedha za makusanyo ya kodi na mauzo ili wilaya zijiendeleze.

Nitajitahidi kufungua mada maalumu, kuchangua Serikali ya Tanzania na mfumo wake wa mapato hapo baadaye.
 
Mkuu unatakiwa uone aibu. Vitu vyote ulivyotaja hapo juu vilikuwa vinawezwa kuwa achieved na effort ya mtu mmoja tu. So what is the point of putting people together?

wool processing – washing, cording, dyeing, knitting and weaving: Hii ni sayansi kimu tu ambayo haina value yoyote katika industrial age.

Don't evade the point! The point is: Umeudanganya Umma! Apologize to the public!
 
Keil,

Naomba usome hii habari kutoka Raia Mwema. Angalia ni jinsi gani watu wanatoka jasho halafu wanawekewa vikwazo kunufaika kisa Serikali na wakala wake hawana uwezo! Let them find market and dictate the prices!


SafeRedirect.aspx

John Bwire
Machi 24, 2010​
SafeRedirect.aspx

Hilo ndilo swali mbalo tunaamini Watanzania wengi wanajiuliza, hivi sasa, baada ya wiki iliyopita, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, naye kujiunga na mlolongo wa wananchi wanaokerwa na hatua ya Serikali ya kuendelea kupiga marufuku wakulima kuuza mazao yao nchi jirani; ilhali yenyewe imeshindwa kuyanunua yote.
Akizungumza Alhamisi iliyopita wakati akifungua mkutano wa watafiti wa sekta ya kilimo, mjini Dar es Salaam, Waziri Mkuu alionyesha wasiwasi wake kwamba hali hiyo itawakatisha tamaa wakulima.
Pinda alisema hivi: “Kama soko tunalolitegemea ni hili la Hifadhi ya Taifa ya Chakula (SGR), wakulima watakata tamaa na hawatatuamini na lengo letu la Kilimo Kwanza. Lazima tufike mahali tuwaruhusu wauze mazao kokote watakakopata soko.”
Lakini pamoja na maneno hayo mazuri ya Waziri Mkuu, Serikali bado haijaruhusu wakulima kuuza mazao yao nje, na kwa sababu hiyo, zaidi ya tani 2,000 za mchele zimelundikana katika maghala ya Mbarali peke yake kwa kukosa soko; maana SGR haina uwezo wa kununua kiasi chote kilichozalishwa.
Kabla ya Waziri Mkuu kutoa kauli hiyo, viongozi kadhaa mikoani tayari walishatoa matamko ya kuisihi Serikali iruhusu wakulima kuuza mazao yao nchi jirani. Wa hivi karibuni kutoa kauli hiyo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Daniel ole Njoolay wakati wa mkutano wa Pinda na wakuu wa mikoa, mjini Dodoma.
Lakini ni kauli hiyo ya Waziri Mkuu ambayo imewashangaza zaidi wananchi. Imewashangaza, kwa sababu Waziri Mkuu hakutarajiwa naye awe ni mtu wa kulalamika. Yeye ni mtu wa kutenda.
Kama wakulima wanalalamika kutoruhusiwa kuuza mazao yao nje, kama wakuu wa mikoa, pamoja na waziri mkuu wao, nao wanalalamikia hali hiyo hiyo, ni nani sasa katika Serikali anayepaswa kukisikiliza kilio chao na kuwasaidia?
Tunajua kwamba Serikali ya Awamu ya Nne imekuwa na mapungufu mengi ya kiutendaji, lakini hatukutarajia kwamba ingefikia hatua hiyo ya viongozi kulalamika tu badala ya kutenda.
Kama Waziri Mkuu Pinda hawezi kusimamia kuondolewa kwa pingamizi hilo la wakulima kuuza mazao yao nchi jirani, basi, wakulima nchini wana haki ya kufahamishwa ni nani hasa anayekwamisha pingamizi hilo kuondolewa.
Ni matarajio yetu kwamba Rais Kikwete na baraza lake la mawaziri wataliweka sawa suala hili haraka iwezekanavyo; kwa maana ya kuondoa haraka pingamizi hilo.
Kwa hakika, kuwahimiza wakulima walime kwa bidii, na kisha kuwazuia wasiuze mazao yao nje ya nchi wakati Serikali haina uwezo wa kuyanunua yote, ni kuwafanya wawe masikini zaidi.
Ndiyo maana tunawaunga mkono wakulima wetu katika kilio chao hicho. Hoja yao ni nzito, na hivyo tunaishauri Serikali kuondoa haraka pingamizi hilo waweze kuuza mazao yao nchi jirani ili wafaidike vyema na jasho lao.
 


President Julius Nyerere urged Tanzanians to reject capitalist exploitation, and build a society based on African communalism. Ntimbanjayo Millinga with a few others and hardly any funding put these views into practice and built an extraordinary rural society based on equity between women and men, young and old. By 1969, 17 ujamaa villages had formed the Ruvuma Development Association (RDA). But the governing party was so hostile to grassroots power that, against Nyerere’s will, they closed it down. Tragically, Millinga died in 2008. But the RDA he led is a beacon in our struggle today.




MillingaTanzatrip07photo1colfor3email.jpg


Najaribu kuipitia hii phase over and over.
 
Butiama hakikuwa kijiji cha ujamaa?If so then sera yote haikuwa sahihi...you start from home

Butiama kilikuwa kijiji cha ujamaa na kilikuwa mbele sana kwenye utekelezaji wa sera hii. Kilimiliki mali nyingi kijamaa ikiwemo karakana ya kisasa kabisa ya zana za kilimo, malori ya kusomba mazao na mbolea, mashamba makubwa tu ya kijamaa, walijenga community centre nzuri sana,....Kilichoua miradi ya vijiji hivi ni uhasibu mdogo sana wa miradi hii, ufisadi na uongozi hafifu mno. Vijiji vyenyewe bado vipo na ukienda pale Butiama utaona baadhi ya alama za ujamaa.Kilichonishangaza mimi ni jinsi mashirika ya UMMA yalivyokufa tena yakiongozwa na yale yaliyokuwa yanamilikiwa na TANU/CCM kama SUKITA, MECCO,....
 
Butiama kilikuwa kijiji cha ujamaa na kilikuwa mbele sana kwenye utekelezaji wa sera hii. Kilimiliki mali nyingi kijamaa ikiwemo karakana ya kisasa kabisa ya zana za kilimo, malori ya kusomba mazao na mbolea, mashamba makubwa tu ya kijamaa, walijenga community centre nzuri sana,....Kilichoua miradi ya vijiji hivi ni uhasibu mdogo sana wa miradi hii, ufisadi na uongozi hafifu mno. Vijiji vyenyewe bado vipo na ukienda pale Butiama utaona baadhi ya alama za ujamaa.Kilichonishangaza mimi ni jinsi mashirika ya UMMA yalivyokufa tena yakiongozwa na yale yaliyokuwa yanamilikiwa na TANU/CCM kama SUKITA, MECCO,....

Mimi nimewahi kufika Butiama,na zijaona haya....vitu impressive pale ni vile vya Mwalimu na familia yake...sasa kama watu waliweza kuuwa kijiji cha muasisi mwenyewe then there were more than problems in the policy....
 
Vijiji vya ujamaa bado viko mkoa wa Kilimanjaro katika wilaya za Same na Mwanga, kule kando ya ziwa Jipe, vijiji kama Kigongo nk ni vya ujamaa. Maeneo ya lower Moshi kuna vijiji kama Mvuleni, Newland vyote vya ujamaa na vipo hadi leo.
 
Vijiji vya ujamaa bado viko mkoa wa Kilimanjaro katika wilaya za Same na Mwanga, kule kando ya ziwa Jipe, vijiji kama Kigongo nk ni vya ujamaa. Maeneo ya lower Moshi kuna vijiji kama Mvuleni, Newland vyote vya ujamaa na vipo hadi leo.

Vipo kwa majina au vina operate kama VvU?
 
Back
Top Bottom