Vijiji vya Ujamaa vilivyokufa ni vipi?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Baada ya kushindwa kwa sera ya Azimio la Arusha ya Ujenzi wa Vijiji vya Ujamaa vijiji vingi vya ujamaa vilikufa na wananchi wakarudia maisha yao ya jadi. Hii yote inasadikika ni jinsi gani Mwalimu Nyerere alishindwa katika uongozi. Najua wengi hapa mmewahi kupita maeneo mbalimbali ya tanzania je kuna mtu yeyote anayeweza kukumbuka kilichokuwa kijiji cha Ujamaa ambacho baada ya sera ya Azimio kushindwa kilikufa na wananchi kurudia maisha yao ya jadi?

Ninavyovifahamu mimi:

Kijiji cha Ujamaa Ndulungu (Singida)
Kijiji cha Ujamaa Geza Ulole (Dar)
Kijiji cha Ujamaa Litowa (Songea)
Kijiji cha Ujamaa Kagera (Kigoma)
Kijiji cha Ujamaa Matetereka (Songea)
Kijiji cha Ujamaa Buyuni (Dar)

N.k
 
I'm also curious to know mkuu. Isije ikawa kuna baadhi ya wananchi bado wana fikiria mpaka leo kuwa kuna such a thing as vijiji vya ujamaa.
 
Kuna vijiji viwili niliviona, kimoja Sengerema na kingine Biharamulo - Vile vijiji havikupewa majina maana vyote viliitwa vijiji vya Ujamaa, lakini ukienda hata leo pana magofu ya vijiji na wao wanavijiji waliohama wanaviita "mahame" vimebaki magofu tu!

Of course majumba yameezuliwa na kuaharibiwa sana - sijui ni makusudi au ni wizi.
 
Asante MWANAKIjiji, baadhi ya maeneo vijiji vilivyoanzishwa na Ujamaa bado vinaendelea kama vifuatavyo vipo Mbeya Vijijini vilianzishwa kufuatia presidential decree ya vijiji vya Ujamaa mfano wake ni Nsongwi Juu(Sogeza) kiliitwa Sogeza kutokana na ile kuwasogeza watu toka maeneo yao ya asili, nsongwi mantanji, nsongwi(ituha), ijombe juu(ntangano), shibolya, tembela(idunda), hatwelo,ilembo usafwa, galijembe nadhani hata simambwe ni kijiji cha ujamaa. pia vipo vijiji vingine watu nusu wali adopt hivyo vijiji vya ujamaa wengine wakashindwa hivyo kufanya mtaa mmoja kuwa mbali na kijiji halisi mfano kijiji cha iwalanje kina mtaa uliojitenga na upo mbali na kijiji halisi unaitwa syema unaweza dhani ni kijiji ila utajua kuwa mtaa kwa idadi ndogo ya watu hazizidi kaya 50
 
Last edited by a moderator:
Mwanakijiji naona unawapa raha wapinzani wa Ujamaa. Ombi langu mimi ni moja: Muangalie na Vijiji vya Ujamaa ambavyo vilianzishwa kwa hiari kabisa tena kabla ya kutangazwa kwa Azimio la Arusha na kuja kwa Operesheni Sogeza n.k. Hivyo ndio msingi wa Ujamaa halisi na Muasisi wake sio Mwalimu ila ni huyu Mzee hapa chini.

Rediscovering Tanzania's Ujamaa –
Tribute to the Great Ntimbanjayo Millinga and the Ruvuma Development Association
Sunday 8 February 1.30-5.30pm, VENUE: Bolivar Hall Venezuelan Embassy
You may remember that we held an event in June 2007 with Madaraka Nyerere. That occasion relaunched the Arusha Declaration by President Julius Nyerere and publicised his enormous contribution to peace, justice and recognition of women's unwaged work as basic to survival and to development.
Since then the Global Women's Strike has continued researching and publicising the achievements of the Ruvuma Development Association (RDA), which successfully built the ujamaa movement, President Nyerere's central strategy for building African socialism. Ntimbanjayo Millinga, the founder and inspirational leader of the RDA, tragically died last year. On 8 February we are holding a memorial, celebrating his life and work: Rediscovering Tanzania's Ujamaa – Tribute to the Great Ntimbanjayo Millinga and the Ruvuma Development Association – see details below. Few know about what rural people in Tanzania in the 1960s collectively created despite lack of material resources. They built an extraordinary rural society based on equity between women and men, young and old, with and without disabilities, achieving a harmony most of us have never known and which, we're always told, ‘human nature' prevents us from achieving.
We are very fortunate that we will have the participation and first-hand experiences of Conrada Millinga, Ntimbanjayo Millinga's wife; Suleman Toroka, headmaster of the RDA's remarkable school from which young people and all concerned with education can learn a great deal; Noreen and Ralph Ibbott who, at invitation, lived with their children in his village – Noreen working with the women, and Ralph as a dedicated and skilled technical adviser. We are planning to publish his unique account of what RDA achieved and how, and its destruction.
This event is part of an International Gathering, The Struggle Against Poverty, War and Occupation, 31 January to 8 February, in which women and men from our international network are participating – please see details below.
We hope that you will be able to attend the tribute and any of the other events. Bring your friends and relatives, and please circulate this invitation widely, through your workplace, email, facebook, religious institutions and networks, etc.
Also much needed are donations towards the costs of organising the event including air fares – it is entirely unfunded and organised by volunteers. Cheques of any amounts payable to the Global Women's Strike can be sent to the address below.
Looking forward to seeing you there.

Rediscovering Tanzania's Ujamaa – Tribute to the Great Ntimbanjayo Millinga and the Ruvuma Development Association
In the 1960s, a great anti-imperialist movement swept the world. President Julius Nyerere urged Tanzanians to reject capitalist exploitation, and build a society based on African communalism. Ntimbanjayo Millinga with a few others and hardly any funding put these views into practice and built an extraordinary rural society based on equity between women and men, young and old. By 1969, 17 ujamaa villages had formed the Ruvuma Development Association (RDA). But the governing party was so hostile to grassroots power that, against Nyerere's will, they closed it down. Tragically, Millinga died in 2008. But the RDA he led is a beacon in our struggle today.

SPEAKERS: ¨ Conrada Millinga, colleague and widow of Ntimbanjayo Millinga ¨ Suleman Toroka, Head-teacher of RDA ¨ Ralph & Noreen Ibbott, British colleagues who helped build RDA ¨ Selma James, who reclaimed RDA for the movement today.

DATE: Sunday 8 February 1.30-5.30pm
VENUE: Bolivar Hall Venezuelan Embassy


MillingaTanzatrip07photo1colfor3email.jpg



 
Na hivyo vipo Companero au navyo vilikufa?

Sijui ndio maana nasema mvitafiti na hivyo. Ila hivi vya Mzee Millinga viliuliwa kwa makusudi na dola iliyokuwa inadai ni ya Kijamaa kumbe ni dola ya Kichama (Party State). Hebu pata dondoo hii uone jinsi wajamaa wa RDA walivyokuwa wamefika mbali na vijiji vyao vya Ujamaa walivyovianzisha wenyewe kwa hiari:

A tribute to a champion of self-reliance
There are two types of heroes/heroines. The sung and unsung. Thanks to conventional history we tend to notice the former over and above the latter. That's just the way it is. Isn't it?

Yes, we praise the likes of Nelson Mandela and forget the likes of Anton Lembede who inspired the anti-apartheid movement in the first place. As the satirical author of ‘Miradi Bubu ya Wazalendo' portrays it, we eulogizes the service of the likes of Mwalimu Julius Nyerere and ignore that of the likes of his ‘messenger' in the formative period of the struggles for Uhuru. In the case of the Bibi Titi Mohammeds, we even privileged ‘his-tory' at the expense of ‘her-story'.

It is not surprising then that the death of one of the pioneering champions of self-reliance, Ntimbanjayo Milinga, on 12 July 2008 has not captured our conventional imagination. In a way conventional history had it sway in suppressing his story during his lifetime. But if it is the people who ultimately make history then conventional history can hardly bury his heroics.

I, for one, did not know Mzee Milinga personally. Our wanazuoni yahoo group had planned to hold a session with him on the then banned Ruvuma Development Association (RDA). The aim was to directly engage the founder of RDA as we revisit this marginalized part of our history.

This aim is broadly informed by the fact that our history is constantly being hijacked if not distorted altogether. Ours therefore is an attempt at rewriting and remaking our history primarily for our own sake. As we probably all know a people with no clear sense of their history have no clear sense of direction. They don't know where they are really coming from let alone where they are going. To put it bluntly, they are simply lost in the wilderness of ‘ufisadi' and so forth.

Concerning the history of RDA, a notable scholar has this to say: "It is a history that is not written and that is not well understood." The onus is on us now to collect bits and bits of this history and come up with a comprehensive history of a successful attempt to implement the policy of self-reliance. That history will be a tribute to the champion of this policy which, despite Mzee Rhuksa's rhetoric against its twin policy of Ujamaa, still looms large in our Constitution.

Interestingly, there are a number of published and unpublished studies that attempt to make sense of RDA. Ironically, they show that before Mwalimu Nyerere proclaimed self-reliance as a part and parcel of our then official policy in 1967, the likes of the then youthful Millinga had already started practicing it. To them self-reliance was not a mere experiment. It was a way of life.

According to the author of ‘Socialist Ideology and the Reality of Tanzania', the seventeen RDA villages undertook the participatory democracy practice of palaver. In "this process they were able to educate themselves through ongoing examination of their own experience." This led them to evolve their own pattern of education system. They even established a primary school "which, unlike the ordinary schools, did not divorce the children from ‘life of the community.'"

They thus achieved "self-sufficiency in food supply; the buying of a maize-mill which was owned by an expatriate so as to process the food they sold; establishing their own dispensary and attempting to send a villager to learn from a local hospital; purchasing a saw-mill from a capitalist for wood processing; and attempting wool processing – washing, cording, dyeing, knitting and weaving – as a form of cottage industry while at the same time keeping sheep."

As the author of ‘Matetereka: Tanzania's Last Ujamaa Village' notes, by the time RDA was prohibited it had "assets of approximately one million Tanzanian shillings. That was in 1969, way before the heydays of ‘vijisenti! Ironically, RDA assets "were confiscated, their staff transferred to new positions throughout the country, and replaced with security officers to complete the destruction of their activities and institutions." RDA had become too self-reliant!

Many theories, including conspiracy theories, abound on why Mwalimu Nyerere, the self-proclaimed champion of self-reliance, dissolved RDA. This is the same Nyerere who gave RDA a grant to buy the then only maize mill in Songea. Yes, this is the same Nyerere who often visited RDA and used it as a model for his then famous policy documents on ‘Education for Self-Reliance' and ‘Socialism and Rural Development'. What really happened then?

Mzee Milinga is no longer there to tell us what really happened. But his close colleagues are still there. Will they rise up to the challenge? Or will they succumb to ‘Silences in African History'? In any case, as long as we are not truly free our unquenched quest for self-reliance will continue!

Source: The Citizen - Rethinking Things Column
 
mkuu mkjj ISANSA kijiji cha ujamaa wilayani Mbozi kilikuwa ni full kijiji cha ujamaa na mfano kwa nchi nzima. Mwalimu alikuwa akikitembelea kijiji hiki mara kwa mara na aliwapa zawadi ya trekta likiwa na zana zote kama majembe, harrows, harvesters etc. Pia aliwazawadia malori 2. Todate it is just a traditional village na more likely with full of "kabailas"
 
mkuu mkjj ISANSA kijiji cha ujamaa wilayani Mbozi kilikuwa ni full kijiji cha ujamaa na mfano kwa nchi nzima. Mwalimu alikuwa akikitembelea kijiji hiki mara kwa mara na aliwapa zawadi ya trekta likiwa na zana zote kama majembe, harrows, harvesters etc. Pia aliwazawadia malori 2. Todate it is just a traditional village na more likely with full of "kabailas"

hicho kijiji kipo au baada ya "kuushindwa" ujamaa watu wakaamu kurudi kwenye miji yao ya asili?
 
Mwanakijiji, hakuna kijiji kilichokufa, kusambaratika au kubaki magofu. Sera yenyewe ya ujamaa ndio iliyokufa. Shughuli za kijamaa hazifanyiki tena ukiondoa misiba, harusi na sherehe zingine kama mbio za mwenge. Ndio maana sasa hivi hati za ardhi zinamilikishwa vijiji hivi. Serikali za vijiji zipo, vitongoji vipo na baadhi ya vijiji hivi sasa ni miji midogo.
 
MMM nimekumbuka kuwa kuna utafiti ulifanyika kuhusu hali ya sasa ya vijiji hivyo ila ni wa zamani kiASI. Tafuta REPORT OF THE PRESIDENTIAL COMMISSION OF INQUIRY INTO LAND MATTERS VOL 1 & 2 utaona orodha na hatma ya baadhi ya hivyo vijiji.
 
Hicho kijiji bad kipo na ni wazee ndio waliorudi kwenye vijiji vya asili , mostly ikiwa ni around kijiji kipya wakiacha watoto wao kwenye hicho kijiji kipya. As of now vijiji vya asiliaround Isansa vimeungana na kijiji cha ujamaa ambayo ni kama centre/ mji mdogo of that area. The good thing ni kwamba ukienda pale todate yo can smell and feel what Mwalimu was dreaming about vjj vya ujamaa!!!
 
Kama wananchi walikaa kwenye vijiji hivyo kwa muda mrefu na huduma muhimu za jamii zikawa zipo, iweje watu warudi kule kwenye vijiji vya asili? Ndio hapo sasa najiuliza huwa tunafikiriri nini maana ni rahisi kufanya kazi ya kuendeleza pale mlipofikia kuliko kuanza tena upya kwenye maisha yale ya zamani.
 
Lets see, what are the reasons Vijiji wether Vijiji vya Ujamaa or Vijiji Asili or Vijiji vya Kisasa dying or falling apart.

Kwanza ni sera mbovu za kilimo na ununuzi wa mazao ya Wakulima. Ikiwa Serikali kupitia vyama vya ushirika na bodi za mazao zilijitwalia mazao kwa bei chee na wao kunona, huoni Mkulima na Mwanakijiji atasema gademu shiti na kuachana na kilimo?

Pili, kufumuka kwa maendeleo ya miji na kupanuka kwa mitandao ya mawasiliano ambayo iliwezesha watu kusafiri na kujionea gibande ingine. Wale wa jamaa wa Ochestra Tomatoma walipoimba Tembea Ujionee usingoje kuambiwa, yule Mzee Mwanakijiji akaondoka kijijini kwao Mntinku, Itelile na kwingineko akaenda mjini. Kufika mjini anakuta nyumba za ghorofa, umeme, simu, maji kwenye bomba na choo cha kuketi. Anakuta kuwa viwanja vya vikao sijui Rose Garden na mengine na mbaya zaidi anaona shule nyingi, hospitali na alipoenda kuomba kibarua, akalipwa ujira mkubwa kuliko aliowahi kuoona. Sasa kwa kuwa yeye hana elimu ya kufikiria vya mbele na anachofikiria ni kinachotokea sasa hivi, anaamua kubaki mjini na kuwapigia wenzie simu ya kopo na kuwaambia jamani Mjini kuna neema, wanatudanganya tukae vijijini.

Kijijini kwetu,ambacho kilikuwa cha asili na watu hawakuhamishwa bali mfumo wa kiserikali uliletwa, mpaka leo watu wanaunga Azimio kwenda kuchota maji mtoni. Hakuna Zahanati, shule ziko, lakini hakuna waalimu, watu wenye umri wa kufanya kazi wamekimbilia mijini na kwenye ajira badala ya kilimo, waliobakia wameridhika na maisha na wanaendeleza maendeleo ya kujikimu.

Tatizo si Vijiji vya Ujamaa au sera ya Vijiji vya Ujamaa, Tatizo ni lile lile la UONGOZI! Tatizo si Wanakijiji kukimbilia mijini, tatizo ni UDHAIFU na UKICHWA NGUMU wa UONGOZI ulioambatana na tabia ya UBWANA, UBWANYENYE na hata UMANGIMEZA na UNDUMILAKUWILI na kuwaona kila mtu asiye na cheo au mamlakakuwa ni MTUMISHI, MTWANA na asiyeSTAHILI maisha bora.

Kwanini tutafutu vijiji vya mikoani? si tuende pale jirani ya Dar Es Salaam ? nenda vijiji vya huku Ubungo, Kimara, Tandika, Mbagala, Pugu, Kisarawe, Bagamoyo, hakuna maendeleo zaidi ya Barabara ya lami kutumikia wenye pesa kutoka mjini kwenda kununua ardhi na kujitajirisha!

Hata pale Manese, Mabibo, Temeke reli, Ilala boma, Kariakoo, Msasani, Kinondoni Shamba, bado kuna umasikini wa hali ya juu na watu wanaishi maisha ya dhiki kuliko walioko Vijijini ambao hawana maji ya bomba.

Ikiwa leo hii pale Dar Es Salaam bado kuna watu wanakaa kwenye nyumba za Udongo, sembuse Ujiji na Wete?

Kama ilivyokuwa Azimio la Arusha, tulianza kujenga Vijii vya Ujamaa, tukapandisha kuta, kisha tukawaambia watu wahamie, lakini hatukumalizia kuta, kuezeka paa wala kuweka milango na madirisha sembuse kusakafia sakafu.

Mnategemea nini kitokee kazi ikifanyika nusunusu?

Watu waache kulaumu Sera na Maazimio yaliyoandikwa ama Kinadharia au hata kisheria, waangalie Utendaji na Ufanisi wa Watendaji.

OUr problem is not policy, program or scheme, our problem is inefficiency, lazyness, greed, procrastination, ineptitude, not taking accountability or acting responsibly and we do not follow through to track and measure any progress or even take time to make thorough and straight forward assesments!

Just remind yourselves whi Kikwete did not jump on a boat to cross river Ruvuma and head to frelimo celebrations. Have you heard what happened to those who invited the President to see the "completed" bridge?
 
Baada ya kushindwa kwa sera ya Azimio la Arusha ya Ujenzi wa Vijiji vya Ujamaa vijiji vingi vya ujamaa vilikufa na wananchi wakarudia maisha yao ya jadi. Hii yote inasadikika ni jinsi gani Mwalimu Nyerere alishindwa katika uongozi. Najua wengi hapa mmewahi kupita maeneo mbalimbali ya tanzania je kuna mtu yeyote anayeweza kukumbuka kilichokuwa kijiji cha Ujamaa ambacho baada ya sera ya Azimio kushindwa kilikufa na wananchi kurudia maisha yao ya jadi?

Ninavyovifahamu mimi:

Kijiji cha Ujamaa Ndulungu (Singida)
Kijiji cha Ujamaa Geza Ulole (Dar)
Kijiji cha Ujamaa Litowa (Songea)
Kijiji cha Ujamaa Kagera (Kigoma)
Kijiji cha Ujamaa Matetereka (Songea)
Kijiji cha Ujamaa Buyuni (Dar)

N.k
Mkuu Mwkjj,

Pamoja na sera ya Ujamaa kutofanikiwa, wananchi wengi waliendelea kuishi kwenye vijiji hivi na ukisikia watu wanasema 'mahame' basi wanamaanisha vile vijiji vya zamani kabla ya 1974. Katika vijiji vipya ziliwekwa huduma hasa shule za msingi ambazo hadi leo zinaendelea kusomesha watoto wetu na kuwafanya wazazi wasiende mbali sana na maeneo yale.

Vitu ambavyo hutaona ni yale matangazo ya 'KIJIJI CHA UJAMAA GEZAULOLE' na mashamba ya pamoja kama 'MFUMAKI' , maduka ya Ushirika, nk. hayo yote yamebaki historia.

Vijiji vya Ujamaa bado vipo isipokuwa Ujamaa wenyewe hatuuoni katika vijiji hivi.
 
Mkuu Mwkjj,

Pamoja na sera ya Ujamaa kutofanikiwa, wananchi wengi waliendelea kuishi kwenye vijiji hivi na ukisikia watu wanasema 'mahame' basi wanamaanisha vile vijiji vya zamani kabla ya 1974. Katika vijiji vipya ziliwekwa huduma hasa shule za msingi ambazo hadi leo zinaendelea kusomesha watoto wetu na kuwafanya wazazi wasiende mbali sana na maeneo yale.

Vitu ambavyo hutaona ni yale matangazo ya 'KIJIJI CHA UJAMAA GEZAULOLE' na mashamba ya pamoja kama 'MFUMAKI' , maduka ya Ushirika, nk. hayo yote yamebaki historia.

Vijiji vya Ujamaa bado vipo isipokuwa Ujamaa wenyewe hatuuoni katika vijiji hivi.

Sorry, How can you account that ujamaa haukufanikiwa? au you meant haukufanikishwa?
 
Wabz,

Watu wengi hawakuelewei, hata kule kwenye suala la Mwinyi na Azimio wewe unauliza role ya mtu mmoja mmoja na si policy.

Umeuliza swali la mantiki na ndilo la kutafakari, je Ujamaa haukufanikiwa au Watu waliokuwa na dhamana ya kkufanikisha na kufanya kazi kufanikisha Ujamaa hawakutimiliza wajibu wao na hivyo kuufanya uonekane haukufanikiwa.

Same tarait you can see now in free market economy tuliyoikimbilia, ni watu watakaosababisha mfumo na sera zishindwe!

I guess kama Nyani Ngabu anavyosema...........tulivyo!
 
Wabz,

Watu wengi hawakuelewei, hata kule kwenye suala la Mwinyi na Azimio wewe unauliza role ya mtu mmoja mmoja na si policy.

Umeuliza swali la mantiki na ndilo la kutafakari, je Ujamaa haukufanikiwa au Watu waliokuwa na dhamana ya kkufanikisha na kufanya kazi kufanikisha Ujamaa hawakutimiliza wajibu wao na hivyo kuufanya uonekane haukufanikiwa.

Same tarait you can see now in free market economy tuliyoikimbilia, ni watu watakaosababisha mfumo na sera zishindwe!

I guess kama Nyani Ngabu anavyosema...........tulivyo!

Wakuu samahani kwa kutoka nje ya mjadala. Rev. nakuomba nipenyezee namba na email address ya Bob Rick. Natanguliza shukrani
 
Kama hivi vijiji vipo na vimeendelea hata kuwa miji midogo na kusababisha huduma mbalimbali za jamii kuwafikiwa kwa wananchi, tunaweza kusema kwa kiasi fulani japo ujamaa wenyewe haupo lakini lile lengo la kuwaleta wananchi pamoja katika operesheni vijijini limefanikiwa?
 
Wabz,

Watu wengi hawakuelewei, hata kule kwenye suala la Mwinyi na Azimio wewe unauliza role ya mtu mmoja mmoja na si policy.

Umeuliza swali la mantiki na ndilo la kutafakari, je Ujamaa haukufanikiwa au Watu waliokuwa na dhamana ya kkufanikisha na kufanya kazi kufanikisha Ujamaa hawakutimiliza wajibu wao na hivyo kuufanya uonekane haukufanikiwa.

Same tarait you can see now in free market economy tuliyoikimbilia, ni watu watakaosababisha mfumo na sera zishindwe!

I guess kama Nyani Ngabu anavyosema...........tulivyo!


Kweli kaka unachosema na mimi najiweka katika mazingira ya kutokueleweka ili mtu aje na convincing argument kuwa kwa nini ujamaa haukufanikiwa, haishii tu kusema ''ujamaa haukufanikiwa' then what?

Kumbuka kwenye thread ya AD, I mixed my argument ya kuwa Mwinyi anaonewa kabisa kuhusu AD. Hajui lolote kuhusu AD, hivyo huyu mtu hapaswi kuhukumiwa kuhusiana na AD, yeye maadamu aliuleta ubepari, tunampa sababu kwa nini alichokileta kilikuwa na makosa na hakikutufaa. So tunapomwangalia individua naye tutam-evaluate failure yake na success yake individually

Ikija policy tutaiangalia Policy kama ilivyo. Personally I think here JF is a place to learn more than in school! just imagine 'unakuwa na discussion group' ya watanzania wasomi waliko dunia nzima! it is amazing! so I think mtu anapokuja kusema lolote awe tayari kuulizwa lolote ili na sisi wengine tufumbuke macho.

Ndiyo maana nimemuuliza mkuu afafanue;

sijajua atafafanua vipi, I think we might have other reasons angalia kipande hiki;

''In 1960s, the 'decade of development', many third world countriesnations failed to make their entry into the modern world, sliding backwards into trabalism and ethnic conflict.Nwely liberated from colonialism, these eerging countries were said to be 'hollow shells, lacking the insitutional structures which make a nation a viable and effective socio-political and economic enterprise; (Inkeles and Smith 1974)

Inkeles, A. and Smith, D.H (1974) Becoming Modern:Indivual Cahnge in Six Developing Countries, Cambrideg,MA:Havard University Press. Kipande hiki kipo pia kwenye kitabu cha John Hannigan -'Environmental sociology' page number 4)

Ukisoma hizo argument za Inkeles and Smith unaona kabisa Tanzania hatumo HUMO! hatumo katika mataifa ya Afrika ambayo hatukuwa na structure, we had institutional structure, hatukuwa na matatizo ya ukabila n.k. This is my kudos to JKN!

In Short, we were perfect country with perfect system etc.

Sasa nilitaka jamaa anaposema umeshindwa atoe sababu ni nini?

'Hollow shell' hiyo Idiom wana maana tulikuwa taifa lakini hatuna uhai ndani yake! damn! Tanzania was a different case.

so my worries are either;

1. Hatukuusimamia vizuri ujamaa (hii ndiyo kisa cha kumlaumu JKN kwa upole, na kumuopoa Mwinyi kuwa alikuwa hajui chochote!)

2. Either tulichelewa kuuanza? yaani pengine tungepata huru miaka ya 50s na kuanzisha ujamaa?

3. Au JKN aliondoka mapema sana, angetakiwa kubakia mpaka 1990, (demokrasia kwa mtoto anayetambaa haipo!)

4. Je, tuna matatizo ya asili ambapo pamoja na hizi social system still we need to deal with our nature?

5. Je kulikuwa na external reasons kutoka mataifa ya nje (I can certainly believe this! but lacking some concrete points), maana hiyo issue ya 'hollow shell' ina maelezo mengi? they gave us freedom while they knew for sure we can not go further! why wao ndio wliokuwa regulators wa soko la dunia n.k walitubania hapo pia!


Kuna ndugu Kyoma nilimuuliza sababu ya kuwa anafikiri Mwinyi angekabiliana vipi na mashart ya IMF na WB ambayo JKN aliyakataa kupitia ushauri wa Mtei? hajanipa jibu, RUDI point number 3 hapo juu, I believe and strongly convinced kuwa JKN angeendelea na msimamo wake wa kukataa haya mashart leo tungekuwa mbali kimaendeleo why!

Tungeteseka sana, lakini katikaakipindi kile cha kuteseka ndiyo tungejifunza mambo mengi.

1. Kuchagua viongozi bora
2. Innovation
3.Utaifa
4. Elimu inayokabili mazingira
5. Laws and effective system za kusuma maisha yetu ya kila siku

Mwinyi alitukwepesha kutupitisha kwenye hii ''REFORMATION MUHIMU SANA YA TAIFA' ya kuteseka kwanza kuwekana sawa! so issue za kula ugali wa njano was none comparing to the future glory that country we heading to!

Today we need to start are fresh, na ndiyo nika -pose challenge kwa wote waamini wa AD kuto mlaumu yeyote, hakuna atakayewaelewa! kaeni chini, piga buku, fanya modification lets move foward....

The suddenly change of system from Nyerere's to Mwinyi's imeua taifa !

Hatuna nchi leo, sad to write this, we are doing election , but there is none! none at all, mpaka msingi ya taifa hili itikiswe na kuwekewa drip za kulikoa!

Nadhani umenielewa mkuu nawaza nini,

By the way I am learning, mimi ni mhandisi haya mambo na sisi na mbali mbali sana , But I have.....................see my signature.
 
Back
Top Bottom