Vijana wote tushirikiane kwa hili

Gwota

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
205
92
Nimefanikiwa kufanya utafiti (usio rasmi) kwa watu wa rika mbalimbali wenye elimu chini ya form 4 na wa chache wenye f4 failuire ktk mikoa ya kigoma,pwani, morogoro na dar, Kikubwa nilichokuwa nataka kujua ni kwanini wengi wao hawakupiga kura?
Walio wengi walijibu hata ningepiga mimi mmoja nisingefanya CHADEMA ishinde,Nilipowauliza km wanafahamu kura yao ina faida hata km Slaa asingeshinda wote walisema hawajui na wanachokifahamu wao baada ya kupiga haina faida tena.
Nilipowaelezea faida ya hiyo kura yao, kuwa kila chama kinapata gawio kubwa la ruzuku kutoka serikalini kila mwezi kutokana na idadi ya kura kilichopata ktk uchaguzi mkuu, Nikazidi kuwaelimisha kwa kuwapa mfano kuwa ruzuku ya CCM imeshuka kutoka miliion 1200 kwa mwezi hadi million 800 na nyingi zimehania CDM na ndo maana CDM wanapata pesa ya kutosha kuzunguka nchi nzima hadi wilayani kutoa elimu na kuwaeleza haki zenu namna zinavyopindishwa wailijilaumu kwann hawakumpigia Slaa kura yao, mmoja wa hao alikuwa ni mama wa Ngerengere akaniambia atafurahi km CDM watafika Ngerengere.
Ninchowaomba vijana wenzangu hasa wale wa CDM Tutumie muda wetu mwingi kuwaondoa mawazo haya mabovu hawa wenzetu wasio na elimu ili tujiongezee mtaji wa kura hapo 2015, Tukifanikiwa kulinasa hili kundi ushindi upo nje nje na hatuna sababu ya kushindwa,tuwafafanulie kwa undani km nilivyofanya mm na hadi leo hao nilioongea nao huwa wananipigia simu kuniuliza maendeleo ya CDM na bila shaka hao tayari ni wetu 2015,
Kwa wale wenye kufanya kazi hasa za mkusanyiko wa watu km mashuleni wasiache kutumia nafasi hizo kuwaelimisha wanafunzi especially O level na A level.

pamoja Tunaweza...............pipoooz pawaaaa
 
Hilo litafanyika katika opereshani mojawapo zinazo kuja,kuelimisha kuhusu faida za kupiga kura,kujiandikisha na kujitokeza kupiga kura bila kukosa na matatizo mengine kama kuuza shahada na kupiga kura kwa kurubuniwa na vijizawadi.
Kwa sab katika ambao hawakupiga kuna ambao hawajawahi kupiga kura kabisa maishani mwao,wengine walishapiga mara nyingi na labda hawakuona jinsi kura inavyoweza kubadili maisha ya mtu
 
The best groundswell movements render the existing power structure irrelevant, because the new belief system adopted by the masses overwhelms the capacity of the elite to maintain control over the former mass delusion over which they presided.
 
Elimu ya mpiga kura na uraia kwa ujumla inahitajika kwa watanzania wengi sana, naona umezungumzia form four wakati kuna watu vyuo vikuu na wala hawatambui umuhimu wa kupiga na wengi hawakupiga kura kwa hoja ya kutoamini ya kwamba kura yake itamsaidia. Hivyo basi wote wanapaswa kupata elimu ya uraia katika kuhakikisha watu wanatambua haki zao.
 
Back
Top Bottom