Na hapo ndo kwenye shida ya vijana na watu wengi miongoni mwetu. Mtu kaiba mali anaendesha gari ya thamani na kuishi maisha ya kifahari basi anaitwa mtu mwenye mafanikio ktk jamii.
Angalieni mchango wa mtu kwenye kusaidia jamii kuondokana na matatizo. Akifanikiwa ktk hilo ndiyo useme huyu jamaa ndiye mtu mwenye mafanikio ktk jamii ya watanzania.
'Mitanzania ndivyo tulivyo'
Patrick Ngowi mbona sijamuona wakati ni billionea?
Napata shida sana kujua ni nini maana ya mafanikio. Hivi mtu anayepata kula kwa kutegemea ujira wa kumtumikia mtu mwingine ndio utamwita mwenye mafanikio? Huyo Mange mi nilishasema kitambo kuwa siyo mzima kiakili. Kwangu mimi mtu aliyefanikiwa kujiajili mwenyewe na kutengeneza ajira kwa wengine ndiye mwenye mafanikio. Na mtu anayetumia kipaji chake ama elimu yake kwa kusaidiz jamii kama mwanasheria, daktari, engineer, na wengineo.
Kama suala ni vijana, wapi shigongo?, wapi mohamed dewji? Na wengineo?
Mkuu patrick ngowi yupi huyo unayemzungumzia?
Huyu Hapa Billionea mtanzania anauza solar power.
Forbes Millionaire $(kwetu ni billionea) under 30
Patrick Ngowi Young African Millionaire on Forbes list under 30
Patrick Ngowi ubilionea upi alio nao, tunavyojua ana ubilionea wa umaarufu,hela aliyo nayo patrick haifiki kokote,amejitahidi kucheza na vyombo vya habari tu ila tunafahamu vizuri.
Sioni umuhimu wa hii mada hapa na moja na sababu kubwa ni kwamba ni research gani imefanyika ikaonyesha kwamba wao ndio vijana waliokuwa na mafanikio zaidi mwaka 2011 huo ni upuuzi, unajua kwamba kuna vijana waliopata mafanikio makubwa sana kwa mwaka 2011 na bado wako kimya hawana kelele wametulia. wewe ulitoa mada huko uliko itoa na huyo aliyeianzisha nyote ni OVYO. samahani kama nitakuwa nimekuudhi.