Vijana wawatoa kamasi wazee Nyanda za Juu Kusini

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Vijana wawatoa kamasi wazee Nyanda za Juu Kusini

lC.gif
Felix Mwakyembe, Mbeya
Novemba 3, 2010
rC.jpg
bul2.gif
CHADEMA yachanga vema karata zake Mbeya Mjini

bul2.gif
Miji mikuu na kata kubwa yakamatwa na CHADEMA

bul2.gif
Ubunge wampa ajira ya kwanza ya mhitimu Chuo Kikuu

Usemi huo unajengwa na jinsi baadhi ya wagombea katika mikoa hiyo maarufu kwa uzalishaji chakula nchini walivyopewa nafasi ndogo ya kushinda kutokana na udogo wa umri na majina madogo katika siasa za nchi lakini hatimaye wameibuka kidedea.
Wagombea hao ni pamoja na CHADEMA, Joseph Mbilinyi aliyeshinda Jimbo la Mbeya Mjini kwa kumwangusha Mbunge wa CCM aliyemaliza muda wake, Benson Mpesya, kijana wa miaka 25 Ernest David Silinde aliyemwangusha Mbunge wa CCM aliyekuwa akitetea jimbo hilo, Dk. Luka Siame na Mchungaji Simion Peter Msigwa aliyemwangusha Mbunge wa CCM Iringa Mjini, Monica Mbega.
Kwa upande wa wagombea wa CCM ni wazi kwamba hakuna aliyemtegemea Chilufi Dickson kunyakua Jimbo la Mbarali akimshinda mgombea wa CHADEMA, Kagwa Kazimoto.
Wengi pia wameshangazwa na anguko la Thomas Nyimbo wa CHADEMA ambaye awali alipewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na umahiri wake katika siasa za nchi hii lakini akajikuta akishindwa na mgombea wa CCM, Lwenge Hosea aliyepewa nafasi finyu.
Kama ilivyochambuliwa katika makala iliyopita, Jimbo la Mbeya Mjini lilitegemea jinsi washindani watavyochanga karata zao za mwisho na ndivyo ilivyotokea na ni CHADEMA walioicheza vema karata yao.
Walijiandaa kwa pigo takatifu la mwisho ambalo mahasimu wao wakuu, Chama cha Mapinduzi walishindwa kulitambua tangu mwanzo, nalo ni kuhitimishia kampeni zao za kitaifa jijini Mbeya.
Ni wazi CCM walichanganywa na Jimbo la Mbeya Mjini, wakahamia huko kuhakikisha haliendi CHADEMA, wakisahau kuwa Jimbo la Mbeya Mjini lilikuwa muhimu kuliko hilo la vijijini kutokana na ukweli kuwa la mjini ni Jiji na ndio taswira ya Mkoa wa Mbeya.
CHADEMA walielewa umuhimu wa kulikamata jiji hilo, hivyo kuhitimishia kampeni zao za kitaifa, ni mkutano huo uliohalalisha kifo cha CCM jimboni humo, kikakolezwa zaidi na hatua ya Jeshi la Polisi kuwapiga mabomu ya machozi wananchi waliokuwa wakitoka kwenye mkutano huo wa kampeni ulioendeshwa na Mgombea Urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa pasipo sababu ya msingi.
Mabomu hayo yalilipuliwa kuanzia uwanja wa ndege eneo la Mafiat hadi CCM Ilomba, ikiwa ni saa moja tangu kumalizika kwa mkutano na Dk. Slaa kupaa, yalilipuliwa hovyo barabarani walikokuwa wakitembea kwa miguu kurudi nyumbani.
Katika vituo vya mabasi, kwenye uwanja wa mkutano ambako watoto walikuwa wakiburudika kwa kucheza muziki, maeneo mengine ya burudani na wacheza bao, kwenye makazi na basi dogo lililokuwa limebeba waandishi wa habari, ilikuwa tafrani kubwa, wananchi wakasikika wazi wakiapa kwa hasira kuishikisha adabu CCM siku ya uchaguzi.
Msanii na muasisi wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa Mr II au Mr Sugu akiwa katika umri wake wa miaka 38 ndiye sasa amekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini
Mbilinyi anakuwa miongoni mwa wabunge kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo wanaoyashikilia majiji makuu ya nchi kwa maana ya Mbeya yenyewe, Mwanza, Arusha na Dar es Salaam.
Mbali ya Jiji hilo la Mbeya, CHADEMA katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini imeikamata Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na miji muhimu kibiashara kama vile Songea mkoani Ruvuma ambako CHADEMA imebeba katazote za pale mjini, Mji wa Tunduma, mpakani mwa Tanzania na Zambia, Mlowo na Vwawa, yote ya wilayani Mbozi.
Ni wazi kwamba katika kanda hiyo CCM imepata pigo kubwa kutokana naukweli kwamba imepoteza nguvu zake katika Jiji la Mbeya pamoja na kunyakua viti 22 vya udiwani dhidi ya 12 vya CHADEMA na viwili vya NCCR-Mageuzi.
Pigo kwa chama hicho ni ushindi mkubwa wa Mbilinyi aliyenyakua kura 46,411 dhidi ya Benson Mpesya aliyekuwa akitetea kiti hicho kwa muhula wa tatu aliyepata kura 24,236 hivyo CHADEMA kuwa na uhakika wa viti maalum vya udiwani vingi zaidi ya CCM.
Pamoja na kuchukua kata nyingi ikilinganishwa na zile zilizochukuliwa na vyama vingine, ni CHADEMA walionufaika zaidi kutokana na ukweli kwamba wamenyakua kata zenye idadi kubwa ya watu katika Jiji hilo ikilinganishwa na zile zilizochukuliwa na CCM, hali inayokifanya chama hicho kuwa na nguvu zaidi sasa kuliko wapinzani wao.
Mbali ya wingi wa watu, kata hizo zilizochukuliwa na CHADEMA jijini Mbeya zina umuhimu mkubwa katika siasa za jiji hilo, kata hizo ni pamoja na Forest, Nsalaga, Sisimba, Mwakibete, Nzovwe, Mbalizi Road, Iganzo na Ilomba, Ilemi na Ruanda Nzovwe, na hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa vyama nje ya CCM kunyakua viti vingi kiasi hicho vya udiwani.
Kivutio kikuu katika uchaguzi wa mwaka huu kwa Mkoa wa Mbeya ni ushindi wa kijana Ernest Shilinde, mvuto huo unatokana na umri wake mdogo wa miaka 29 na kwamba ndio kwanza anatokea Chuo Kikuu alikohitimu mwezi Mei, mwaka huu, hivyo Ubunge kuwa ajira yake ya kwanza katika maisha yake
Silinde, maarufu katika Jimbo lake la Mbozi Magharibi kama Sauti ya Simba ameiteka kabisa miji ya jimbo hilo kama vile Tunduma na Ndalambo kutokana umahiri wake wa kujenga hoja, sifa ambayo inatolewa pia na vijana wenzake aliosoma nao Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao walikuwemo jimboni humo kwa kile walichodai kulinda kura za mpiganaji wao.
Mbali ya Silinde, kivutio kingine ni Mgombea wa CHADEMA katika Jimbo la Mbozi Mashariki, Mtera Mwampamba ambaye naye amehitimu Chuo Kikuu Mei, mwaka huu pamoja na mwenzie wa Mbozi Magharibi, alifanya kampeni kwa 15 tu na kuambulia kura 31, 997 na nusura amnyang'anye kitumbua Mbunge aliyekuwa akitetea jimbo hilo, Godfrey Zambi aliyepata kura 49,095.
Katika kipindi hicho kifupi kijana huyo alivuta hisia za watu, wakamkubali na mwisho wa siku pamoja na kushindwa alikiwezesha chamachake kuikamata miji muhimu katika jimbo hilo, miji ya Vwawa na Mlowo.
Kujiamini kupita kiasi kwa baadhi ya wagombea kama vile mgombea wa CHADEMA katika Jimbo la Njombe Magharibi, Thomas Nyimbo kulichangia kwa kiasi kikubwa anguko lao.
Ni wazi kwamba kwa upande wa CCM hivi sasa watakuwa wakitafuta mchawi wa anguko lao, hususani kwenye miji mikuu na muhimu katika mikoa hiyo, lakini wananchi wao wanaeleza wazi kwamba hawaridhishwi na chama hicho pamoja na kiongozi wake, Jakaya Kikwete.
"Kikwete ana dharau sana, atasemaje hazitaki kura za wafanyakazi, anawadharau wafanyakazi halafu anawakumbatia mafisadi, anasifu eti jembe la zamani, huyu bwana jeuri kwa kweli, ndio maana maisha yamekuwa magumu hatuna tena matumaini," anasema mama mmoja akionyesha hasira yake baada ya kupigwa mabomu ya machozi akitokea kwenye mkutano wa CHADEMA.
Matukio ya wananchi kupigwa mabomu ya machozi yaliendelea hadi siku zakuhesabu kura ambapo kwa Jiji la Mbeya eneo la Chuo cha Uhasibu
ilipokuwapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakikusanya matokeo, mabomu ya machozi yalianza kupigwa saa moja na nusu usiku na kuendelea hadi saa tano.

Mabomu zaidi ya 50 yanadaiwa kulilipuliwa usiku huo huku vijana wenye hasira wakichoma matairi, kupiga mawe askari na kuzuia barabara
kwa mawe na mipira.

Hali ilikuwa hivyo hivyo katika Mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa ambako inaelezwa kuwa zaidi ya mabomu saba ya machozi yalilipuliwa kutawanyawananchi waliokuwa wakidai kutolewa kwa matokeo na wakiamini kuwa yanacheleweshwa ili kumuibia mgombea wa CHADEMA waliyeamini ameshinda.
Hata hivyo Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo hilo, Silvia Siriwa alimtangaza mgombea wa CCM, Haeshi Hilali kuwa mshindi kwa kupata kura 17,324 dhidi ya kura 17,128 za mgombea wa CHADEMA, Nebert Yamsebo.
Wengine walioshinda na majina ya majimbo yao kwenye mabano ni pamoja na Chilufi Dickson (Mbarali), Dk. Harrison Mwakyembe (Kyela), Aliko Kibona (Ileje), Deo Sanga (Njombe Kaskazini, Anne Makinda (Njombe Mjini)
Mgombea Urais kupitia CCM, Jakaya Kikwete alikuwa akiongoza katika majimbo takribani yote ya Mkoa wa Iringa na ule mpya wa Njombe, Mkoa wa Rukwa, Mbeya na Ruvuma.
Hata hivyo maeneo ya mjini mengi bado kutolewa matokeo rasmi ya Rais isipokuwa Iringa ambalo kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi mgombea huyo wa CCM amepata kura 18,857 dhidi ya 14, 864 za Mgombea wa CHADEMA, Dk. Slaa.
Kikwete anaonekana kuongoza pia katika majimbo ya Sumbawanga Mjini,Mbarali, Njombe Magharibi, Njombe Kaskazini, Njombe Mjini na Ileje.
Matokeo kwa majimbo ya Mbeya Vijijini, Kwela, Kalambo, Nkasi Kaskazinina Nkasi Kusini na Lupa yalikuwa hadi jana mchana bado kutangazwa.


Source Raia mwema
 
Back
Top Bottom