VIJANA WASOMI 'watanunuliwa'

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,800
Chama cha Mapinduzi kimeapa kuwa kitafanya kila kiwezalo kuwanunua vijana ndani na nje ya vyama vya upinzani ili kubaki madarakani. Katika ujumbe mfupi niliopokea leo kama 'Mwana-propaganda Mbobezi' chamani, kila mmoja wetu(sisi ambao tuna ushawishi wa kutosha) ahakikishe kuwa ananunua hata vijana wasomi kumi nchini Tanzania kutoka vyuoni na shuleni. Hii itafanya CCM ionekane ni sehemu iliyosheheni wasomi wengi.

Mkakati huo unaratibiwa na viongozi wa juu wa Chama cha Mapinduzi wakioongozwa na Katibu Mkuu Wilson Mukama aliyeubuni. Ujumbe huo pia unaeleza kuwa itakaposhindikana kuwanunua wapya,waliopo wapandikizwe kwenye vyama vya siasa vyenye nguvu ili watwae nafasi za maamuzi ya kukwamisha vyama hivyo.

TAARIFA YA NYONGEZA (Kwenye ujumbe huohuo): Mkutano wa kwanza wa Kamati Ndogo ya Kuratibu Uchaguzi wa Sumbawanga Mjini utafanyika siku ya Jumatano ijayo tarehe 17/10/2012 katika Ukumbi uleule wa Mikutano wa Siku zote kuanzia saa tatu asubuhi.Wajumbe mfike bila kukosa mkiwa na mawazo yenu ya kujenga chama.

Nakala kwa: Mzee Tupatupa (nadhani ujumbe huu utakuwa umeshamfikia). Funguka Kamanda Mzee Tupatupa
 
Ni kweli kabisa Mkuu. Kumbe Mashushushu tupo wengi ndani ya CCM? Basi wao wameshachelewa sana.Sina shaka na thread yako. Kazi nzuri. Unaujua Ukumbi 'uleule'? Ngoja niku-pm.
 
Utanunua mwili wa mtu sio roho na ufahamu wao. Vizuri sana mimi mmoja wao nipo hapa njooni mmninunue. Nataka nyumba gari na m50 bank.
 
sasa kama ccm wana hizi hela zote kwa ajili ya kuwanunua hawa vijana kwa nintu isifanye ambo ya maana dhen hawa vijana wakaipenda kwa ufanisi wake wa kisiasa katika kuleta maennndeleo.
yani nikiiwaza hii ccm hua nahisi TZ tuna bahati mbaya kweli. yan hi ndo altenative ya jinsi ya kukikomboa chama chao?? sasa jiulizeni je altenative ya kuleta maendeleo kwa nchi ni ipi??
 
Tutafanya kama igunga wanaleta pesa tunakula ccm tunalala cdm watakiona 2015,na watakao pata nafasi za kusimamia uchaguzi kwa wale wa vijijini watusaidie kitu kimoja kwawale ambao awajui kusoma na kuandika kura zetu zile kwa cdm,walio wahi kusimamia watanielewa naongelea nini,ya tutakaba kila kona kuakikisha cdm tunaiweka madalakani.
 
msomi mtu gani?asiejitambua,asietumia usomi wake manufaa kwa jamii,mwenye mtazamo hasi ? hapa sio chama,bali ni upeo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom