Vijana wasomi wa aina ya Mwigulu Nchemba wana 'Significant Contribution' kwa TAIFA?

sidimettb

Member
May 17, 2011
42
14
Sina shaka yoyote kuhusu vyeti vyake vya darasani,ila wasiwasi mkubwa ni unafiki/kutokujiamini kulikopitiliza kunakompelekea kujipendekeza kwa kiwango cha juu sana kwa watawala na in a way kuwa mzigo kwa wenzake wasiobahatika kufika kiwango kikubwa cha elimu ya darasani katika mazingira anamoishi. Ananikumbusha zamani kidogo ambapo vijana pamoja na kusoma walikuwa na uhuru na confidence kidogo sana, badala yake wanaishia kujipendekeza kwa makada wa ccm ili wapate nafasi Fulani ndani ya serikali.

Hizo styles zimepitwa na wakati, kwa hiyo wakati watu wenye umri mkubwa kama kina Dr.Slaa, Mwanakijiji etc wanapigana usiku na mchana kulitoa gizani taifa hili, ni aibu na ni usaliti kwa vijana wasomi wa aina ya Mwigulu kuwa sehemu ya kurudisha nyuma hizi juhudi i.e Kama hana mchango chanya ni bora akakaa kimya na uhazini wake ndani ya Taasisi iliyomwajiri(CCM), kwa maana historia itakuja kumhukumu kwa usaliti anaoufanya dhidi ya maskini waliowengi nchii hii!

Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu mwenendo wa huyu jamaa ni kichefu chefu kwa kweli. Kwamba, wakati vijana wengine wasomi wakipigania kujinasua na mfumo uliooza wa sisi m, kama walivyofanya vijana wa enzi hizo e.g JKN dhidi ya mfumo dhalimu wa kikoloni, yeye sifa kubwa kwake ni kusikika kuwarudisha kwenye giza watu wengine,bila shaka kwa gharama kubwa tuu. Inasikitasha kuona kuna watu bado wanafikiria kumrudisha mtu fulani kwenye chama mfano diwani,wakati dunia inadili na falsafa na dhima nzima ya kuweka mfumo utakaofaa wote.

Kwa upande mwingine nina imani kubwa kwamba ndani ya nafsi yake kijana kama NAPE bado ni silaha muhimu sana ya upinzani ndani ya Chama Cha Magamba, japo hawezi kijionyesha wazi kwa sasa!

Ni imani yangu kuwa sijamshambulia yeye personally,ila aina ya dhamira anazoziwakilisha!

Nawasilisha

Mwigulu anafadhari anaongea anapotakiwa livingstone lusinde huyu jamaa ni wa mtera yeye ni mchekeshaji na hajui kujenga hoja kwa umbile na umri wake huwezi amini anayo yafanya nia aibu kwa kweli full kujikomba...................................
 
wameenda shule ila hawakuelimika

Yupo mbunge kilaza kuliko wote yule wa MTERA

Mkuu you are very right. To be schooled is not the same as to be educated, kuna watu wamesoma lakini ni wezi kuliko ambao hawajasoma, Kwa system tuliyonayo Tanzania usomi si kigezo cha mafanikio. elimu si kigezo cha mafanakio, lakini kujuana na fitna ndio misngi wa maendeleo binafsi.
 
Anatetea ugali binafsi. Suala ni ccm ishinde ili aneemeke hilo swala la kukomboa watu nafikiri in magamba it is an old story, isuue naona wanapigana kunasua chama kisianguke lkn sijui historia hawaikumbuki? vyama vingi kama sio vyote duniani vya aina ya CCm vimeshaanguka tatizo kubwa ikiwa kujisahau na kuconcentrate kushinda uchaguzi, siku hizi wa TZ hata kama hawajaenda shule lazima waevaluate matendo yako ndo wakupe uongozi. Victory is coming soon.
 
Whether umesoma au la, ukifika kwenye lango la ccm unatakiwa ukabidhi akili zako zooote na kuchukuwa ubongo wa kijani. Kwa mambo ya maslahi ya Taifa na vitu vya namna hiyo hawawahusu hawa watu, kazi ni moja tu - kuiba! Na ukijidai kufanya kazi watakushuhulika kama walivyofanya kwa Magufuli, waziri mkuu atapanda ndege kwenda kwenu ili akunyuke mbele ya jamii yako. Mazingaombwe!
 
Wanaiabisha sana Singida. Inaonesha bado kuna kazi kubwa kuitoa Singida yetu kwenye umasikini kama aina ya viongozi wanaotuwakilisha ni wa type hii.
 
Utakuwa unajidanganya ukidhani wapinzani wana jema na nchi hii, wengi ni wachumia tumbo tu, basi tu hawajapata nafasi ukayaona makucha yao halisi. CCM tunaweza kuona vizuri make ndo wenye nchi sasa.

Mfumo wa siasa zetu kwa sehemu kubwa watu wazuri kupenyeza ni ngumu sana, ndo maana utaona kina "Prof" Maji marefu (mganga wa kienyeji) au Sugu (mtukana ovyo) wanapita wakati kuna watu makini sana kwenye majimbo yao wanapigwa chini.

Dont be too naive na hizi bla bla za vyama. Kama we unaweza ingia ukomboe nchi.
 
Lusi nde?ya!nadhani naye anatakiwe awe na bend yake ya mipasho in campaign kama yule Kilaza wa Mbinga katibu wa kusinzia mjengoni.
 
jamaa alikuwa kiranja ilboru alikuwa mnoko na anaboa sana.sema ni kiongozi ambaye hasaidii kuleta maendeleo.yuko yuko tu.sema ni kakikongwe kiasi.
 
Utakuwa unajidanganya ukidhani wapinzani wana jema na nchi hii, wengi ni wachumia tumbo tu, basi tu hawajapata nafasi ukayaona makucha yao halisi. CCM tunaweza kuona vizuri make ndo wenye nchi sasa.
Mfumo wa siasa zetu kwa sehemu kubwa watu wazuri kupenyeza ni ngumu sana, ndo maana utaona kina "Prof" Maji marefu (mganga wa kienyeji) au Sugu (mtukana ovyo) wanapita wakati kuna watu makini sana kwenye majimbo yao wanapigwa chini.
Dont be too naive na hizi bla bla za vyama. Kama we unaweza ingia ukomboe nchi.

Tunachozungumzia ni kwamba mfumo uliyosimikwa na kulelewa na ccm umefika beyond repair.Hauwezi kufiti kwa muda huu,na lazima tuubadilishe.Hata waliokuwa wanam support Kiwete baadae walimgeuka baada ya yy kuto deliver ilivyo tarajiwa, 'partly' due to his own weakness and mainly due to deep rooted corrupt system where he immersed completely na ama akashindwa au akaamua kutopiga mbizi.

Ni katika mtazamo huo tunaona tuwe na mfumo mpya,ambao kwa bahati mbaya uwepo wa ccm madarakani utakuwa kikwazo kikubwa kwani wenyewe wanaulinda vilivyo kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Ni kweli hata huko upinzani kuna wanaochumia tumbo tena wanaweza wakawa wengi,miongoni mwao kuna wanajisahihisha lakini pia wengi wanapukutika on the way kwa sababu hawana pa kujishika kwani matawiwaliyoyategemea hayapo huko e.g imadiwani wa arusha, and Shibuda's type to follow!) bali wachache wenye dhamira ya kweli tangu mwanzo watatuvusha kwa kuwa wanasuport yetu as long as hawajatoka nje ya mstari mpaka hapo.
 
Kwa hiyo lengo lako ni nini? Watanzania wote wawe na mawazo kama ya Slaa na Mwanakijiji?
Absolutely NO!.Kuna tofauti kubwa kati ya kutofautiana namna/mbinu ya kupigana na adui,na kuhusu adui ni yupi hasa!
 
Kwa hiyo lengo lako ni nini? Watanzania wote wawe na mawazo kama ya Slaa na Mwanakijiji?
Tunataka elimu ya ukombozi wa kifikra kwa watu wetu wote, sio aina ya magamba walio na fikra mgando za kuombaomba pekee. Kikundi kinachowaza kushinda uchaguzi at any cost ni hatari zaidi ya mabomu ya maangamizi.
 
Utakuwa unajidanganya ukidhani wapinzani wana jema na nchi hii, wengi ni wachumia tumbo tu, basi tu hawajapata nafasi ukayaona makucha yao halisi. CCM tunaweza kuona vizuri make ndo wenye nchi sasa.
Mfumo wa siasa zetu kwa sehemu kubwa watu wazuri kupenyeza ni ngumu sana, ndo maana utaona kina "Prof" Maji marefu (mganga wa kienyeji) au Sugu (mtukana ovyo) wanapita wakati kuna watu makini sana kwenye majimbo yao wanapigwa chini.
Dont be too naive na hizi bla bla za vyama. Kama we unaweza ingia ukomboe nchi.
Kazi ipo, halafu utadai umesoma!! Unajadili watu, ndio elimu uliyoipata, kujadili watu. Kwa uelewa wako finyu mtu mzuri ni yule aliyevaa joho pale mlimani na sehem kama hiyo, asiyepita pale si mtu mzuri? Ama uzuri wa mtu ni aina ya kazi yake, na si mchango wake? Kwa aina ya watanzania wenye fikra potofu kama zako nchi haina maisha marefu. NI WAZALENDO WACHACHE WENYE MOYO NDIO WATAITOA NCHI HII UTUMWANI.
 
Wanaiabisha sana Singida. Inaonesha bado kuna kazi kubwa kuitoa Singida yetu kwenye umasikini kama aina ya viongozi wanaotuwakilisha ni wa type hii.

Singida si ndio anatoka Nape? Nape na Mwigulu, they are all alike!
 
Kuna wakati inabidi ujue unafanya siasa na sioni tatizo kwa Mwigulu kwa yeye kufanya kile anachotumwa na chama chake suala hapa ni kujenga hoja za kuwaondoa ccm na mfumo mzima madarakani siyo mtu binafsi kama Mwigulu na sidhani kama anayafanya hayo kwa sababu ya njaa maana jamaa kazi aliyokuwa nayo ni nzuri ni mtu kama wa 12 kama sijakosea kutoka kwa gavana ina masilahi na safari kibao sidhani kama anajipendekeza ila anafanya anachotumwa kama nape na wengine wengi ingawa wanachukia ufisadi so sidhani kama ni busara kumshambulia mtu personal Ma Great Thinkers.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom