Vijana wamsimamisha Kikwete Mwanjelwa; wazomea "fisadi fisadi"

RFA wanatangaza sasa hivi katika taarifa ya habari kwamba Rais Kikwete amewaambia vijana wateue wawakilishi wao na amekubali kukutana nao na wameeleza hayo na ufisadi na kulala chini. Haya mliozoea kusikiliza habari za 'kweli', subirini redio zenu na magazeti yenu kutoka ile familia ya TBC na Uhuru na RAI (Rostam Aziz International)

Hahahahah

Tunashukuru sana gottee kwa kutuhabarisha. Wawakilishi binafsi hasa huko mikoani ni wa muhimu sana sana. Tafadhali endelea kuwa jicho letu huko uliko. Hata habari za kusikia tu ziletwe tuzichambue, maana hakiharibiki kitu hapa jamvini.

JamiiForums inapata members wapya kila kukicha, takribani watu 9 kwa siku. Ninyi mlioko mikoani ni wa msaada mkubwa sana, hata sijui nisisitize vipi hili. "Mpaka kieleweke", wandugu!

.
 
Wewe UJUAVYO, huwezi kujua yote katika dunia hii MKUU adhawaizi unajipachika NGUVU za UMUNGU!!! Taarifa za uhakika JK yupo Mbeya tangu jana jioni! Amelala pale Mbeya Mjini na leo asubuhi ameelekea Rungwe (ndipo alipokutana na 'kikaango' kile) ambapo atalala huko na kesho kuelekea Kyela. Nadhani this time source wako hayuko SAHIHI. Habari za kuzomewa JK sina mashaka nazo kwa sababu mpasha habari wangu alikuwepo kwenye eneo la tukio na kwa taarifa yako kwa kutumia simu ya mkononi nimezisikia zile 'SHAMRASHAMRA'

Kama una jamaa zako Mwanjelwa waulize, tukio hili halikufanyika chumbani, lakini kwa sasa HA HAA HABARI NDIYO MKUU!

Gottee,

Ni kweli JK kafika Mbeya jana na leo ndio kaelekea Rungwe. JK hana ziara ya wilaya ya Mbeya mpaka Jumatatu. Sasa hii ya kuzomewa inatoka wapi?

Msafara wa rais unapopita barabarani watu wanajipanga na kila mtu kuongea la kwake. Sasa kama huko ndio kuzomea, basi kazi ipo. Vipi na wanaoshangilia mbona hukuelezea?

Ulivyoandika ilikuwa inaleta impression kwamba rais alikuwa anazomewa kama walivyofanyiwa wale mawaziri mwaka jana kitu ambacho sio kweli. Vijana walikuwa wanatoa dukuduku zao kama ambavyo wanatoa sehemu mbalimbali ambako JK anapita.
 
Sasa sijui mtu anayebisha atatuthibitishia vipi kwamba hakuzomewa? Dunia haiko wala haita zunguka kama watu wengine mnavyotaka!
 
Gottee,

Ni kweli JK kafika Mbeya jana na leo ndio kaelekea Rungwe. JK hana ziara ya wilaya ya Mbeya mpaka Jumatatu. Sasa hii ya kuzomewa inatoka wapi?

Msafara wa rais unapopita barabarani watu wanajipanga na kila mtu kuongea la kwake. Sasa kama huko ndio kuzomea, basi kazi ipo. Vipi na wanaoshangilia mbona hukuelezea?

Ulivyoandika ilikuwa inaleta impression kwamba rais alikuwa anazomewa kama walivyofanyiwa wale mawaziri mwaka jana kitu ambacho sio kweli. Vijana walikuwa wanatoa dukuduku zao kama ambavyo wanatoa sehemu mbalimbali ambako JK anapita.

Wacha habari za "IMPRESSION" bana! Itaku-cost nini wewe kumuuliza maswali mleta hoja? Watu wamekaa darasani kufunzwa namna ya kuripoti habari. Kwa nini utegemee kila mtu aweze hilo?

Eleza wasiwasi/dukuduku lako politely. Please!
Inakuwa kama mtoa habari kafanya kosa. Ninyi ndiyo mnawafanya wengine hata wasijiunge humu. Kuna waliojiunga lakini hawathubutu kuandika hata mstari mmoja.

.
 
Wacha habari za "IMPRESSION" bana! Itaku-cost nini wewe kumuuliza maswali mleta hoja? Watu wamekaa darasani kufunzwa namna ya kuripoti habari. Kwa nini utegemee kila mtu aweze hilo?

Eleza wasiwasi/dukuduku lako politely. Please!
Inakuwa kama mtoa habari kafanya kosa. Ninyi ndiyo mnawafanya wengine hata wasijiunge humu. Kuna waliojiunga lakini hawathubutu kuandika mstari mmoja.

.

Mkuu,

Hapo umefanya vyema,kula zako tano mkuu.Kuna watu wanaotaka kujifanya wao ndiyo wanajua kila kitu,HAKUNA Dunia haitaenda jinsi tutakavyo
 
Gottee,

Ni kweli JK kafika Mbeya jana na leo ndio kaelekea Rungwe. JK hana ziara ya wilaya ya Mbeya mpaka Jumatatu. Sasa hii ya kuzomewa inatoka wapi?

Msafara wa rais unapopita barabarani watu wanajipanga na kila mtu kuongea la kwake. Sasa kama huko ndio kuzomea, basi kazi ipo. Vipi na wanaoshangilia mbona hukuelezea?

Ulivyoandika ilikuwa inaleta impression kwamba rais alikuwa anazomewa kama walivyofanyiwa wale mawaziri mwaka jana kitu ambacho sio kweli. Vijana walikuwa wanatoa dukuduku zao kama ambavyo wanatoa sehemu mbalimbali ambako JK anapita.

Mimi nimeambiwa Rais kazomewa, kama wewe umeambiwa kashangiliwa na wewe andika hivyo adhawaizi huhitaji kunitilia maneno yako mdomoni mwangu! Sasa kama wewe unataka 'kupimanisha' mawaziri wa JK walivyozomewa na Bosi wao hilo ni lako! Hivi wewe Mtanzania unapata impression gani hata kama Rais wetu alikuwa anashangiliwa kwa watu kutamka 'MAFISADI'

Nataka nikwambie mimi sina chuki yoyote na JK lakini siwezi kusema uongo tu kwa kuwa yeye ni Rais! Ishara ya LEO huko Mbeya na ukichukulia hali TETE kule Tarime kwa mwenye kuitakia nchi hii mema lazima AJIULIZE mara mbili mbili. SIFA za UONGO hazitamsaidia JK! HALI NI TETE MKUU!
 
mimi nimeambiwa rais kazomewa, kama wewe umeambiwa kashangiliwa na wewe andika hivyo adhawaizi huhitaji kunitilia maneno yako mdomoni mwangu! Sasa kama wewe unataka 'kupimanisha' mawaziri wa jk walivyozomewa na bosi wao hilo ni lako! Hivi wewe mtanzania unapata impression gani hata kama rais wetu alikuwa anashangiliwa kwa watu kutamka 'mafisadi'

nataka nikwambie mimi sina chuki yoyote na jk lakini siwezi kusema uongo tu kwa kuwa yeye ni rais! Ishara ya leo huko mbeya na ukichukulia hali tete kule tarime kwa mwenye kuitakia nchi hii mema lazima ajiulize mara mbili mbili. Sifa za uongo hazitamsaidia jk! Hali ni tete mkuu!

hali ni tete wapi tanzania nzima au huko mbeya na tarime peke yake ?
 
Mkuu,

Kuna watu wako hapa kumrushia maneno mabaya Salva Rweyemamu anavyompamba Rais,lakini wao ndio worst of all.Wantaka eti uje na kichwa cha habari "JK apokelewa kama mfalme",
"Au JK aiteka Mbeya", Au "Kikwete Funika mapokezi ya Nyerere Mbeya" au ..........Wakuu wengine hebu malizieni mje na heading za kuwatuliza watu wengine moyo
 
mimi nimeambiwa rais kazomewa, kama wewe umeambiwa kashangiliwa na wewe andika hivyo adhawaizi huhitaji kunitilia maneno yako mdomoni mwangu! Sasa kama wewe unataka 'kupimanisha' mawaziri wa jk walivyozomewa na bosi wao hilo ni lako! Hivi wewe mtanzania unapata impression gani hata kama rais wetu alikuwa anashangiliwa kwa watu kutamka 'mafisadi'

nataka nikwambie mimi sina chuki yoyote na jk lakini siwezi kusema uongo tu kwa kuwa yeye ni rais! Ishara ya leo huko mbeya na ukichukulia hali tete kule tarime kwa mwenye kuitakia nchi hii mema lazima ajiulize mara mbili mbili. Sifa za uongo hazitamsaidia jk! Hali ni tete mkuu!

gottee;

ujumbe wako umefika na mwenye wake aanzishe thread yake, focus yako pia imeeleweka, thanks saaana for keeping us posted na wahusika wafanye kazi
 
Wakuu,kuna watu wanataka kulazimisha mambo.Wameshaambiwa waanzishe thread yao lkini utawakuta wanalazimisha na kung'ang'ania hapa tu.
 
Hahahahah

Tunashukuru sana gottee kwa kutuhabarisha. Wawakilishi binafsi hasa huko mikoani ni wa muhimu sana sana. Tafadhali endelea kuwa jicho letu huko uliko. Hata habari za kusikia tu ziletwe tuzichambue, maana hakiharibiki kitu hapa jamvini.

JamiiForums inapata members wapya kila kukicha, takribani watu 9 kwa siku. Ninyi mlioko mikoani ni wa msaada mkubwa sana, hata sijui nisisitize vipi hili. "Mpaka kieleweke", wandugu!

.

Mkuu LD,

Binafsi yangu mimi huwaogopa sana watu WANAOJUWA KUWA HAWAJUI lakini WANAJIFANYA WANAJUA KUWA WANAJUA wakati sisi TUNAJUA KUWA HAWAJUI!

Hivi mtu anatoka huko alikotoka na na kusema NINAVYOJUA MIMI RAIS ANAANZA ZIARA tarehe KADHAA huko KADHAA wakati SI KWELI! Rais yupo MBEYA tangu jana jioni na alikuwa anakutana na watu wengi tu jana pale Ikulu Ndogo! Jamaa zangu wamekula chakula naye jana usiku! Rais ameelekea Rungwe leo akiwa njiani pale Mwanjelwa ndipo akakutana na 'msaragambo' ule. Watu wamelala njiani! Msafara wa Rais ukasimama! Akajitokeza kuwaamkua wananchi! Wakamuamkua! Nimeambiwa hakukuwa na tukio lolote la kurusha mawe au kitu cha aina yeyote ila watu walikuwa 'wakishangilia' kwa kusema neno 'mafisadi' Mimi nimesema kwamba hizi taarifa nimeambiwa na source wangu! Binafsi NINAMUAMINI! Lakini silazimishi Mtanzania naye AMUAMINI ila namuuliza Mtanzania yeye AKIJUA KITU ndio JF wote wanajua??? Na yeye AKIJUA KITU, wana JF wana UHAKIKA gani kwamba anachokijua kina ukweli?

Masikio ya Mtanzania yanataka kusikia tu, 'JK apokewa kwa nderemo!', 'Msafara wa JK washindwa kupita Mwanjelwa kwa sababu watu walilala chini kushinikiza JK amuadabishe Kubenea!' Wananchi wamwambia JK, hakuna Rais kama wewe, 'Mwandosya ampa tafu JK', 'JK asema mkinichagua tena hakyanani nampa Uwaziri Mkuu Mwandosya na Mwakyembe Unaibu Waziri Mkuu na Mwakyusa Urais wa Zanzibar!

Mimi namshauri Mtanzania asubiri TBC One, na TBC Taifa, na TBC Nanihii na RAI Hoja ya Nguvu, na Makamba na Pius Msekwa na Nchimbi na Mwakipesile na yeye mwenyewe. Hao watampa taarifa anazozipenda!

Nawakilisha!
 
Wakuu,kuna watu wanataka kulazimisha mambo.Wameshaambiwa waanzishe thread yao lkini utawakuta wanalazimisha na kung'ang'ania hapa tu.

Sijathibitisha lakini naambiwa Mwanjelwa ilikuwa 'Trela' senema yenyewe ilikuwa Uyole!
 
Hebu Watz tuwe na utamaduni wa kukiri tunapokosea. Mimi nilishuhudia msafara mpaka maeneo ya Ikulu ndogo ya Mbeya. JK hakuzomewa! Labda atazomewa siku nyingine lakini jana haikuwa. Mzee gottee, tunatengeneza story hadi JF?

Kila eneo lililokuwa na mkusanyiko wa watu wengi kulikuwa na ulinzi wa kutosha kuanzia uwanja wa ndege hadi alipofikia. Gari yake ilikuwa imefungwa vioo muda wote.

Kwa bahati mbaya tulioshuhudia tunatakiwa kuamini maneno ya mtu 'aliyesimuliwa' akiamini alichoambiwa ni sahihi.

NN.
 
Mkuu LD,

Masikio ya Mtanzania yanataka kusikia tu, 'JK apokewa kwa nderemo!', 'Msafara wa JK washindwa kupita Mwanjelwa kwa sababu watu walilala chini kushinikiza JK amuadabishe Kubenea!' Wananchi wamwambia JK, hakuna Rais kama wewe, 'Mwandosya ampa tafu JK', 'JK asema mkinichagua tena hakyanani nampa Uwaziri Mkuu Mwandosya na Mwakyembe Unaibu Waziri Mkuu na Mwakyusa Urais wa Zanzibar!

Mimi namshauri Mtanzania asubiri TBC One, na TBC Taifa, na TBC Nanihii na RAI Hoja ya Nguvu, na Makamba na Pius Msekwa na Nchimbi na Mwakipesile na yeye mwenyewe. Hao watampa taarifa anazozipenda!

Nawakilisha!

HAhahahh kwi kwi kwi kwi Ijumaa imeanza wikienda hiyooooooooooo!!
 
Mkuu LD,

Binafsi yangu mimi huwaogopa sana watu WANAOJUWA KUWA HAWAJUI lakini WANAJIFANYA WANAJUA KUWA WANAJUA wakati sisi TUNAJUA KUWA HAWAJUI!

Hivi mtu anatoka huko alikotoka na na kusema NINAVYOJUA MIMI RAIS ANAANZA ZIARA tarehe KADHAA huko KADHAA wakati SI KWELI! Rais yupo MBEYA tangu jana jioni na alikuwa anakutana na watu wengi tu jana pale Ikulu Ndogo! Jamaa zangu wamekula chakula naye jana usiku! Rais ameelekea Rungwe leo akiwa njiani pale Mwanjelwa ndipo akakutana na 'msaragambo' ule. Watu wamelala njiani! Msafara wa Rais ukasimama! Akajitokeza kuwaamkua wananchi! Wakamuamkua! Nimeambiwa hakukuwa na tukio lolote la kurusha mawe au kitu cha aina yeyote ila watu walikuwa 'wakishangilia' kwa kusema neno 'mafisadi' Mimi nimesema kwamba hizi taarifa nimeambiwa na source wangu! Binafsi NINAMUAMINI! Lakini silazimishi Mtanzania naye AMUAMINI ila namuuliza Mtanzania yeye AKIJUA KITU ndio JF wote wanajua??? Na yeye AKIJUA KITU, wana JF wana UHAKIKA gani kwamba anachokijua kina ukweli?

Masikio ya Mtanzania yanataka kusikia tu, 'JK apokewa kwa nderemo!', 'Msafara wa JK washindwa kupita Mwanjelwa kwa sababu watu walilala chini kushinikiza JK amuadabishe Kubenea!' Wananchi wamwambia JK, hakuna Rais kama wewe, 'Mwandosya ampa tafu JK', 'JK asema mkinichagua tena hakyanani nampa Uwaziri Mkuu Mwandosya na Mwakyembe Unaibu Waziri Mkuu na Mwakyusa Urais wa Zanzibar!

Mimi namshauri Mtanzania asubiri TBC One, na TBC Taifa, na TBC Nanihii na RAI Hoja ya Nguvu, na Makamba na Pius Msekwa na Nchimbi na Mwakipesile na yeye mwenyewe. Hao watampa taarifa anazozipenda!

Nawakilisha!

Gottee,
Hapo umenena.Kama hawataki kusikia hilo basi,wabongo wengine bwana.Duh!
 
Mtanzania ili aende Kyela au Rungwe ambako ndiko ziara yake kwa siku ya leo na kesho haimpasi JK kupita maeneo kama Mwanjelwa?

Mbona unakuza mambo pasipo kuwa na hoja ya msingi dhidi ya Gotee.
 
Kazomewa kashangiliwa anapaswa awe amejua by now kuwa upepo hauelekei upande wake!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom