Vijana walia na rafu za UVCCM

kupelwa

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
1,087
450
na Mwandishi wetu

BAADHI ya vijana wanaowania uongozi kwenye Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wamelalamikia vitendo vya kuwabeba baadhi ya wagombea.

Wakizungumza na Tanzania Daima kwa masharti ya kutotajwa majina yao walisema miongoni mwa rafu hizo ni kampeni zilizoanzwa kufanywa na wenzao kinyume cha taratibu za umoja huo.

Walisema walianza kampeni hizo kwenye sherehe za Idd Pili zilizoandaliwa na Mbunge wa Ukonga, Eugene Mwaiposa (CCM) aliyewaalika baadhi ya wajumbe kwenye fukwe moja iliyopo Kawe jijini Dar es salaam.

Walisema katika sherehe hiyo wagombea hao (majina tumeyahifadhi) ambao wanawania uenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ilala na unyekiti Mkoa wa Dar es Salaam walimwaga sera zao wakiomba wajumbe watakaoingia kwenye vikao vya maamuzi mkoani na wilayani wapitishe majina yao.
 
huwezi kupanda boga ukavuna zabibu, Mtoto wa nyoka ni nyoka tu, hizi mbinu wanaiga kwa baba zao magamba
 
huwezi kupanda boga ukavuna zabibu, Mtoto wa nyoka ni nyoka tu, hizi mbinu wanaiga kwa baba zao magamba

uchaguzi huo kiini nacho sababu ya makundi ya walionacho na wasiokuwanancho na hapa ccm itataka iweke viongozi wao uvccm na si viongozi wa wanachama wa uvccm
 
Huwezi kupata uongozi ccm bila kutoa rushwa,anyway acha wafu wazikane.
 
Huwezi kupata uongozi ccm bila kutoa rushwa,anyway acha wafu wazikane.

Hao UVccm Wanaolalamikia ni wajinga kwa sababu wanajua wazi mbinu zote ndani ya gujichama lao.MSOMI KIJANA KUWA CCM ANAAKILI YA MAITI.
 
huwa nawashangaa sana vijana wanaoishabikia CCM

kwa miaka 50 CCM haijamkomboa Mtanzania labda kama wazazi walo ni mafisadi
au walifaidika na ufisadi,
 
Kwa hiyo kuja kulalamika huku jf kunawasaidia nini?kwanini na wao wasifanye siasa?hawana ujasiri ndio mana wanaogopa hata kutaja majina yao
 
Kwa hiyo kuja kulalamika huku jf kunawasaidia nini?kwanini na wao wasifanye siasa?hawana ujasiri ndio mana wanaogopa hata kutaja majina yao

hawajalalamika jamii forum, bali ni tafiti za gazeti la tanzania daima na taarifa alizoletewa mwadishi kuwa kuna viongozi ndani ya ccm wanapanga safu yao ua uvccm iliwapate kuiendesha wanavyotaka.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom