Juzi katika Kongamano la kumuenzi Mwalimu Nyerere, viongozi wa zamani akiwapo Jaji Warioba alishauri kuwa vijana tuache kulalamika tuchukue maamuzi na kuamua kutenda nami nakubaliana naye mia kwa mia. Katika nchi yeyote mabadiliko huletwa na vijana ikiwa jamii husika iko tayari au la. Na Tanzania yetu ya leo mabadiliko ya kweli yataletwa na vijana. Ni ukweli uliodhihiri kuwa maendeleo ya Tanzania hayawezi kuja chini ya CCM lije jua au mbalamwezi. Mtoto aliyelelewa kifisadi atafikiri kifisadi na kutenda kifisadi ndio maana wanarithishana majina yale yale tazama kuna J. Makamba, N. Mnauye. H. Mwinyi, Kipi Warioba,R. Kwikwete n.k.Hawa wote ni mvinyo wazamani kwenye chupa. Hawawezi kuwa na jipya katika kupambana matatizo yetu hawayajui kwanza wamesoma nje hawajui matatizo ya shule zetu kuwa pale mlimani wenzao tulikuwa tunalala mzungu wanne.
Ni ukweli ukombozi wa nchi yetu utaletwa na vijana nishauri vijana wote tuamue kuwa sasa basi kila kijana ahakikishe kuwa anakitambusho cha kupigia kura na kama hana wakati ukitimia wa kujiandikisha kila kijana ajiandikishe na afanye kwa nafasi yake kuelisha umma juu ya madhara ya kuendele kutawalwa na CCM tusiendeleze janga la kitaifa.
Tuachekulalamika tuchukue hatua.
Mungu Ibariki Tanzania