Mimi ninashindwa kuelewa hivi kila mtanzania ni lazima aipende Chadema? Maana nimeona post zote mtu akiwa tofauti na Chadema basi atashambuliwa kwa matusi,kebehi na kila neno la dharau jamani wanabodi mfumo wa vyama vingi unaturuhusu kutofautiana kwa hoja bila kupigana,hivi mtu akieleza hisia zake kuwa anaipenda CCM basi liwe ni kosa? Tujifunze kuwa wavumilivu ikiwa mmoja wetu hapendi kile wanachokipenda watu wengine! Na hakuna haja ya kuitana majina yasiyofaa inaonekana watu hawako tayari kufanya siasa za kiustaarabu tujirekebishe.
hao wasomi inaonekana hawajielewi
Ritz lazima atapost,"maandamano mabukwa ya kumpongeza jk vyuo vikuu"
Inatia aibu kwa kweli...
kuna kama vijana kumi hivi wameandamana eti kuunga mkono jitihada za serikali za JK kupangua baraza la mawaziri na kupokelewa na Vuvuzela la ccm Nape
Kwa harakaharaka ukiangalia ni kama kichekesho lakini vilevile ni aibu kwa vijana kuandamana kupongeza wajibu wa mtu! hawaoni kama huyo Jk ndiyo kikwazo kwa utendaji na ustawi wa nchi hii na ni aibu kwa yeye kuteua watu ambao mwisho wake wanakuwa waizi wa rasilimali za nchi hii!
Shame on you vijana kama kmi mlioandamana!
Leo mchana nape amepokea maandamano ya wale wanaojiita Wana cccm wa vyuo vikuu,lengo Lao ni kupongeza Kamati kuu.(source Chanel ten)
Haiwezekani na ni vigumu kuamini kwamba bado kuna wasomi vyuoni ambao wanaweza kupoteza muda wao kwa ajili ya kuunga mkono ubadhirifu unaofanywa na mawaziri wa jk,
Watakuwa wanafunzi wa imani ya wala tende, halua na ubwabwa.
Madogo wamepewa shilingi elf5 na Tshet basi wame'respond.