Dijina40
JF-Expert Member
- May 17, 2010
- 727
- 242
Nimetafuta nimechoka. Ninaowapata wote wazuri wiki 2 - 4 za mwanzo baadae wanageuka wezi. Wameniibia miaka 2 yote nimekuwa na-invest shambani bila kupata kitu, mayai wanauza, kuku wanauza, vifaranga wakishachangamka wanauza. Shamba ni la wanyama hasa kuku na kanga. Nguruwe niliwaondoa baadae nitaweka tena. Nimejaribu kutoa hadi nyumbani kijijini interior, wakifika wazuri wiki 3 baadae wakishasalimiwa na vijana wa vijiweni wanageuka wezi tena hao ndugu wamekuwa wabaya kuliko watu baki. Vijana wa shamba wanaojituma na kufanya kazi kwa uaminifu wanapatikanaje? Shamba liko nyuma ya Wazo Hill kuleee alikokuwa akikaa marehemu Waziri Mkuu wetu wa zamani.