Vijana Wa Nyakati Hizi Sijui Wana Matatizo Gani?.

SAYANSIKIMU

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
1,132
260
Siku hizi imekuwa kawaida kwa baadhi ya vijana wanapokuwa mashuleni wanatafuta wasichana baada ya hapo wanawapa mimba na akigundua aliyefanya nae mapenzi ana mimba basi msichana huyo anatelekezwa.Imekuwa ni tabia ya vijana na hata baadhi ya wababa kutia mimba na kutelekeza msichana aliyempa mimba.Tatizo linakuwa kwa hawa watoto wanaozaliwa.Watoto hawa wakati mwingine wanakuwa na maisha magumu wanaishia kula mabaki au makombo kwenye mashule mbalimbali ya serikali.Huwa najiuliza mtu anajua kabisa hana uwezo wa KUTUNZA MTOTO lakini hilo hajali anafanya mapenzi na kupeana MIMBA na huyo mtoto aliyezaliwa anabaki kuhangaika,.Mtu unajua kabisa uwezo wa kulea huna kwa nini sasa ufanye mapenzi? .Kwani usipofanya mapenzi utakufa.Wengine utakuta wanawatoto lakini wapo kwa wazazi wao .Ingekuwa kama kweli wana akili wafanyapo mapenzi wawe wanatumia uzazi wa mpango kuzuia mimba zisizo tarajiwa lakini hawajali hilo wanataka hivihivi.Wahusika mjirekebisha.Najua baadhi yenu wahusika mtauchukia huu ujumbe .Vijana mjerekebishe
 
Kuna kipindi wakati nipo secondary nilishawahi kumuhoji mtoto mmoja anayekula makombo ya wanafunzi .Nili muuliza wewe mtoto mama yako yuko wapi lakini yeye akanijibu NIKIENDA KWA MAMA HUWA ANANIFUKUZA ina elekea mama yake huwa anaishi maisha magumu mpaka anaamua kumfukuza mwanae wa kumzaa na kumwacha mtoto anaishia kula mabaki ya wanafunzi.Wakati mwingine unakuta msichana mwenye mimba nayeye anakula mabaki ya wanafunzi mashuleni sasa sijui mtoto aliye mzaa atakuwa anaishi maisha gani wakati huo aliye mpa mimba kasha mtelekeza.Na nyie wasichana nawashangaa sana hivi kwa nini mnakubali kudanganyika kirahisi namna hii .Hivi kweli kwa akili timamu unatongozwa na mwanafunzi wa sekondari mpaka unafanya nae mapenzi wakati unajua kabisa hawezi kulea mtoto basi hata unashindwa kutumia uzazi wa mpango .Mambo haya ndo yanasababisha kuongezeka kwa watoto wa mitaani ,na kuongezeka kwa wanawake wanao TUPA WATOTO WAO kwa kushindwa kuwatunza.Kwa kweli inasikitisha wahusika mjirekebishe basi.
 
Wasuburie watoke makanisan hao vijana.
Sis wazee tumepita long time hku
 
Mkuu hiyo shule ni Mz nini?
 
Nikweli kabisa hata mimi nimeshuhudia hali hiyo hiyo nikiwa A level same sec.. Kwakweli wale watoto wanatia huruma.
 
Back
Top Bottom