Vijana wa mitaani na bajeti ya 2012/2013

Rihanadiya

New Member
Jun 14, 2012
1
0
Nimekuwa nikifatilia maisha ya watoto waishio mitaani kwa muda mrefu sasa na kujikuta nikijiuliza maswali mengi ambayo kwa nyakati tofauti nimekuwa nikikosa majibu juu ya hawa watoto na serikali kwa ujumla. Wimbi la watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu limekuwa likiongezeka siku hadi siku kwa chanzo kinachosemekana ni ugumu wa maisha wanaopata kutoka katika familia zao na wengine ni kutokana na malezi mabaya wanayoyapata toka kwa wazazi wao. Lakini kadiri siku zinavyokwenda wimbi hili la vijana linazidi ongezeka na kwa mtazamo wangu ni kama serikali yetu inatengeneza bomu la nyuklia kwa baadae ambalo likija lipuka litakuwa ni tatizo kubwa sana kwa amani ya nchi yetu. Tumeweza ona wiki chache zilizopita huko zanzibar jinsi vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa wakiongozwa katika kuhatarisha amani ya nchi. Ni siku moja tangu bajeti ya nchi kusomwa lakini katika kusikiliza bajeti hiyo sijaona ni namna gani serikali imepanga kuwasaidia vijana hawa ambao kwa sasa wamekuwa wengi. Ni mahala gani bajeti hii itawasaidi vijana hawa na kuwaondoa katika wimbi la kuishi barabarani. Kwa ujumla vijana hawa tusipowaangalia na kuweza kuwawekea mikakati ya namna ya wao kuweza kuishai japo kwa kiasi kidogo maisha yaliyo bora tutaishia kufukuzana nao barabarani kwa kutuchomolea side mirrow za magari na kuiba hand bag za wakina mama.
Ushauri wangu kwa serikali inabidi kuwafikiria kwani na wao ni part ya watanzania.
 
wazo lako ni zuri sana.ila kwa serikali hii haiwezi kutokea.saizi budget imesomwa lila mmoja wao anawaza atajenga nyumba ngapi,ataninua magari, mangapi, afungue makampuni mangapi,akanyanganye walala hoi ardhi hekta ngai,aongeze magari ya usafirishaji mangapi,azae watoto wangapi,aongeze vumada wangapi na awafanyie mambo mangapi ambayo hawajawahi kufanyiwa maishani mwao.maana viongozi wetu wanpenda kuacha historia.uzalendo sio kujufunza,ila ni utu uliozaliwa nao.bahati mbaya 99%ya viomgozi wetu hawana kabisa hiyo kitu.
 
Tuanze na wwe!Uliyekuwa umemzalisha mmerudiana?Of course ulichoksema ni sahihi,esp.hawa wadogo zetu wa shule za kata,wanaokaa geto.
 
wazo zuri,na hawa vijana kila kukicha ndio wanakuwa kimwili kiakili na kinguvu,bila serikali kuwajali na kuwaangalia kwa jicho la kuwasaidia,huko mbele ya safari kuna kazi nzito!,wao watakuwa ndio wezi,na ndio vinara wa kuuza madawa ya kulevya,kwenye mikutano ya wanasiasa watatumika kama chambo,kila ahadi watakayopewa na mwanasiasa ya kuboresha maisha yao wataiamini,hata kama kimtazamo tu haitekelezeki,kutokana na mawazo duni na kukosa elimu utotoni kwao!
ni vyema serikali ikajipanga kuwasaidia
 
Dar es salaam tu wapo kama 15,000 wale ambao wako kwenye mitandao maalumu kama vile Posta,kisutu, feri,mchafukoge,Kariako,Moroco,Magomeni,mnazi MMoja,Mchikichini,Tazara,Ubungo,Mwenge,Msasani hivi ndio vijiwe vyao maarufu,ni bomu kubwa ni wagomvi washari wanapigana visu wenyewe na ubabe mwingi wanatumiwa kwa ngono wote wanaume kwa wnawake,wanalazimishwa kutumia dawa za kulevya na kuziuza na mfumo wa ustawi wa jamii ni marehemu haufanyi kazi kabisa,wengi wao huwa wanaumwa na kufa bila ndugu zao kujua.Swala la usatawi wa jamii kwa serikali hii ni ndoto ndio maana wanawake wengi wanauliwa kwa kusingiziwa wachawi hakuna anaye jali ,wakoma kwenye vituo wameachwa wafe nyumba wanazoishi zilijengwa miaka ya mwanzoni mwa uhuru hakuna anayekarabati
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom