Vijana Wa Chadema Kukutana Na “wamachinga”

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
WE MNYIKA ACHANA KUFUKUZANA NA WAMACHINGA, NJOO HAPA JF UJIBU MASWALI YA MWENYEKITI WAKO MBOWE!




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

VIJANA WA CHADEMA KUKUTANA NA “WAMACHINGA” WA MKOA WA DAR ES SALAAM
• Kuzindua ripoti ya uchunguzi kuhusu hali na changamoto za wafanyabiashara ndogo ndogo
• Kutoa zawadi kwa washindi wa kuandika michanganuo ya miradi ya wafanyabiashara ndogo ndogo

Wanachama wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) watafanya mkutano na wafanyabiashara ndogondogo wa jijini Dar es salaam katika maeneo ya Kigogo Sambusa siku ya jumapili tarehe 16 Machi, 2008 kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 9 alasiri. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo ni Ndugu Mhonga Said Ruhanywa, Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA) ambaye pia ni mmoja wa wadhamini wa uchunguzi huo.

Mkutano huo ni mahususi kwa ajili ya kuzindua ripoti ya uchunguzi wa mwenendo wa wafanyabiashara ndogondogo jijini Dar Es Salaam pamoja na kutoa zawadi kwa washindi wa kuandika mchangunuo wa biashara ndogo kwa vijana. Pia mkutano utatoa fursa ya washiriki kujadili masuala ya wafanyabiashara ndogo ndogo na ujasiriamali.

Kadhalika katika mkutano huo washindi wa shindano maalumu la kuandika mchanganuo kwa wafanyabiashara ndogo ndogo wa Kinondoni lililoratibiwa na kurugenzi ya vijana wa CHADEMA watapatiwa zawadi zao.

Itakumbukwa kwamba tangu awamu ya kwanza ya serikali ya CCM kumekuwepo na tatizo kubwa la wafanya biashara ndogondogo kuingia katika mivutano ya mara kwa mara dhidi ya serikali iliyopo madarakani. Aidha kwa upande wake, serikali imekuwa ikiwaondoa wafanya biashara hao kwa madai kuwa wanaharibu mandhari ya jiji na kwamba ni budi ama warudi vijijini, au wafanye biashara katika maeneo ambayo yamepangwa na serikali.

Pamoja na hoja hizo, bado kumekuwepo na hali ya mvutano isiyokwisha baina ya wafanya biashara ndogondogo maarufu kama wamachinga , kiasi cha kupelekea uvunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na mauaji, uharibifu wa mali za wafanyabiashara hao, na mapigano baina ya askari kwa niaba ya serikali dhidi ya wafanya biashara hao. Vijana wa CHADEMA tuliamini kuwa kujirudia kwa mivutano na mapambano haya kila wakati ni kielelezo kuwa kuna tatizo la msingi ambalo serikali ya CCM bado ama haijalichunguza au kama limechunguzwa basi halijawekwa bayana.

Katika muktadha huo CHADEMA ikiwa ni chama mbadala kinachoamini katika misingi ya amani, na ufumbuzi wa matatizo kisayansi hatuoni sababu ya watanzania kuendelea kuvutana kiasi cha kuhatarisha hali ya amani na utengamano kwa mambo ambayo yanaweza kupatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa njia za kistaarabu.

Hivyo tuliamua kufanya uchunguzi wa takribani miezi sita katika kipindi cha mwaka 2007 kwenye maeneo husika ili kubainisha njia mbadala kwa mustakabali mwema wa wafanya biashara ndogondogo ambao wengi ni vijana. Aidha uchunguzi huo ulifanywa na vijana wa CHADEMA kutoka taasisi za elimu ya juu, kwa kushirikiana na wafanya biashara ndogondogo. Kamati maalumu ya uchunguzi ya vijana watano iliundwa kuratibu mchakato huu.

Lengo likiwa ni kupata hoja za kuboresha mazingira ya wafanyabiashara ndogo ndogo kwa kutambua mchango wao katika ongezeko la ajira na kukua kwa uchumi wa taifa.

Uchunguzi huu ulihusisha kutembelea maeneo yaliyotengwa kuangalia hali ya mazingira ilivyo sambamba na kuzungumza na wafanyabiashara ndogondogo. Pia uchunguzi ulihusisha kukutana na baadhi ya viongozi wa serikali kupata taarifa mbalimbali za msingi na kufanya uchambuzi wa mwelekeo wa mipango iliyopo. Mchakato huu ulihusisha pia kuwatembelea wahanga wa bomoa bomoa ya wakati uliopita pamoja baadhi ya maeneo yaliyofanyiwa bomoa bomoa katika hatua ya awali kujua hali ilivyo hadi wakati uchunguzi ulipofanyika. Uchunguzi huu ulihusisha pia kutembelea baadhi ya wadau wengine mathalani mashirika yasiyo ya kiserikali kupata maoni yao kuhusu njia bora za kukukabiliana na changamoto za wamachinga. Kwa upande mwingine mchakato huu ulihusisha pia kupitia nyaraka zilizopo ikiwemo zile zilizoandaliwa na taasisi mbalimbali za utafiti zinazozungumzia changamoto zinahusiana na biashara ndogondogo nchini. Kadhalika uchunguzi ulihusisha kupata uzoefu wa baadhi ya nchi nyingine duniani zinavyoshughulikia suala la wafanyabiashara ndogondogo katika nchi zao.

Tunapenda kusisitiza kuwa: “Tunathamini na kutambua haja ya miji yetu kuwa safi, lakini tunathamini na kutambua zaidi maisha ya watu kabla ya chochote.Tunaamni jumuiya ya wafanya biashara ndogondogo, taasisi za serikali na zisizo za kiserikali za kitaifa na kimataifa zitatuunga mkono matokeo ya uchunguzi huu na kuzifuatulia changamoto ambazo tutazianisha , kwa maslahi ya wafanyabiashara ndogondogo na Taifa kwa ujumla.

Punde baada ya matokeo ya uchunguzi huo kutangazwa, hapo kesho , tutayapeleka kwenye taasisi na wadau wote muhimu ili kujadili na kuanza mchakato wa kuishinikiza serikali juu ya namna bora na ya kistaarabu ya kukabiliana na changamoto za wamachinga Tanzania”

Imetolewa 15/3/2008:



John John Mnyika
Mkurugenzi wa vijana
0754 694 553
mnyika@chadema.net
www.chadema.net
 
Mheshimiwa Mnyika,

Hizo reports hazitasaidia kitu chochote kwa Wamachinga.

Njia ya kuwasaidia Wamachinga ni kwa kushirikiana nao ili waunde
vikundi vyao vya kibiashara na kuwasaidia kuongeza capacity ambayo nayo itasaidia ku add value kwenye vitu wanavyofanya.

Kwa mfano mnaweza kuanzisha vikundi vya wanachama wa CHADEMA na mkawasaidia
kuendesha biashara zao kwa ufanisi na kisha mnatumia mafanikio ya hapo kusaidia vikundi vingine zaidi.

Maneno matupu hayatasaidia katika kubadili hali ya Wamachinga, lazima kuwe na vitendo. Hivyo vitendo lazima vitoke chini kwa kuwashirikisha wamachinga wenyewe.

Ninachokiona katika taarifa yako hiyo sidhani kama kitakuwa na faida yoyote kwa Wamachinga zaidi ya kuwatumia kisiasa. Kinachofanyika hapa, utafikiri ni zile tume za serikali ambazo tunasikia kila siku lakini bila tija kuongezeka.

Mafanikio mema, usikose kutuletea mafanikio yatakayotokea ili na wengine tujifunze.
 
Mheshimiwa Mnyika,

Hizo reports hazitasaidia kitu chochote kwa Wamachinga.

Njia ya kuwasaidia Wamachinga ni kwa kushirikiana nao ili waunde
vikundi vyao vya kibiashara na kuwasaidia kuongeza capacity ambayo nayo itasaidia ku add value kwenye vitu wanavyofanya.


Kwa mfano mnaweza kuanzisha vikundi vya wanachama wa CHADEMA na mkawasaidia
kuendesha biashara zao kwa ufanisi na kisha mnatumia mafanikio ya hapo kusaidia vikundi vingine zaidi.

Maneno matupu hayatasaidia katika kubadili hali ya Wamachinga, lazima kuwe na vitendo. Hivyo vitendo lazima vitoke chini kwa kuwashirikisha wamachinga wenyewe.

Ninachokiona katika taarifa yako hiyo sidhani kama kitakuwa na faida yoyote kwa Wamachinga zaidi ya kuwatumia kisiasa. Kinachofanyika hapa, utafikiri ni zile tume za serikali ambazo tunasikia kila siku lakini bila tija kuongezeka.

Mafanikio mema, usikose kutuletea mafanikio yatakayotokea ili na wengine tujifunze.


Machinga wapo katika makundi mbalimbali kutokana na uwezo wao, wale wanotembeza soksi pea 3, viatu pea 2 nk kuwe na mipango ya kuwashawishi na kuwawezesha kwenda vijijini kulima mfano waende wakalime nyanya Ilula.
 
angalau hao chadema wana nia ya kusaidia japo kuwa njia ya kusaidia yaweza kuwa sio, wakati serikali imewasahau kama na hao wamachinga ni raia wake.
 
Serikali haijawasahau machinga, ila inataka kuwe na utaratibu maalum na unaoeleweka kisheria kwa machinga kufanya shughuli zao, hilo liliwezekana sana under Keenja, lakini alipotoka tu wamekuja wale wale watekelezaji wetu uchwara, wanaishia kuwatisha na kuwadhalilisha tofauti kabisa na agizo la serikali,

Anyways, mkuu JJ angalau mnawakumbuka machinga na heshima mbele kwa hillo, sisi tunafuatilia hilo, na ikibidi tunaweza kuchangia mawazo, lakini barvo mkuu!
 
Serikali haijawasahau machinga, ila inataka kuwe na utaratibu maalum na unaoeleweka kisheria kwa machinga kufanya shughuli zao, hilo liliwezekana sana under Keenja, lakini alipotoka tu wamekuja wale wale watekelezaji wetu uchwara, wanaishia kuwatisha na kuwadhalilisha tofauti kabisa na agizo la serikali,

Anyways, mkuu JJ angalau mnawakumbuka machinga na heshima mbele kwa hillo, sisi tunafuatilia hilo, na ikibidi tunaweza kuchangia mawazo, lakini barvo mkuu!

FMES,

Kama ulivyosema kuna mipango mingi sana ya kusaidia Wamachinga, pia serikali inatoa pesa nyingi kwa lengo hilo (kumbuka mabilioni ya JK), tatizo ni kwamba pesa nyingi haziwafikii walengwa kwasababu mbalimbali.

Kinachotakiwa ni hivyo vikundi kusaidiwa kuongeza capacity. Kama alivyosema mchangiaji hapo juu, hakuna added value yoyote kwenye kuzunguka kuuza chupi tatu au nne. Lengo liwe kwenye vikundi vinavyo create au ku add value kwenye services wanazotoa.

Hapo ndipo penye tatizo maana vikundi vingi havina uwezo. Mashirika kama PRIDE yanasaidia ila wamelenga mno kwenye kukopesha na kukusanya pesa zao kuliko kutoa mafunzo kwa wahusika. Kikawaida hili ni jukumu la serikali lakini kwa Tanzania tukitegemea serikali itatuchukua muda mrefu sana.

Hapo ndio makundi mbalimbali yanapotakiwa kusaidia na kama CHADEMA watalenga kwenye kutoa mafunzo kwa hao vijana, itasaidia zaidi. Muhimu ni kuanza na kundi dogo na ambalo linaweza kufanikiwa kisha kutumia mafanikio hayo kuelemisha makundi mengine.

SIDO walitakiwa wawe one of the main players kwenye hili lakini na wenyewe wanawatumia tu Machinga kuombea pesa, kisha pesa nyingi zinaishia kwenye ulaji.
 
Back
Top Bottom