Vijana wa Arusha na ubwiaji wa NGISUGI...!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
9.jpg


Niko mitaa Tabata Ubaya Ubaya na washkaji wa A Town....
Kinachoendelea katika eneo hili ni nyama choma na bia, lakini hawa masharobaro wa A Town nawaona wakipena kitu kilichofungwa kwenye nailoni kwa umahiri. Awali nilidhani ni ile kitu maarufu kwa jina la CHA ARUSHA, lakini nimeshangaa wanabwia na kisha kutema mate...

Nimeshikwa na udadisi na nilipouliza wakaniambia hiyo kitu inaitwa NGISUGI au UGORO.

Yaani wanaubwia kama hawana akili nzuri, na wameniambia hiyo kitu nimaarufu sana huko A TOWN....

Mimi nilijua hii kitu inatumiwa na wazee tu na vibibi vizee, kumbe hata vijana...!
 
Hebu ngoja na mie nionje nijue ladha yake.....LOL
 
Mkuu!
Onja tu, lakini mi wasiwasi wangu hiyo onja-onja itaishia hapo?
Au haijaanzia hapo? Pengine "cha Arusha" nacho ulishakionja?
Kama bado huoni umejongea mazingirani kuki'test ?
 
Mkuu!
Onja tu, lakini mi wasiwasi wangu hiyo onja-onja itaishia hapo?
Au haijaanzia hapo? Pengine "cha Arusha" nacho ulishakionja?
Kama bado huoni umejongea mazingirani kuki'test ?

Mkuu ni chungu, haifai hata kuweka mdomoni..
hapa ni mwendo wa kutema mate na kusukutua kwa maji kwa kwenda mbali.... duh starehe nyingine bana
 
Umekosea jina mkuu Mtambuzi...wanaiita ngisugii a.k.a ugoro...!!! Unatumiwa sana na vijana huku...Hata mie nilipokuwa Secondary nilishawahi kujaribu kutumia hii kitu lakini niliacha kwa sababu niliona haina maana.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo kitu ni biashara kubwa sana kwa baadhi ya akinamama wa kimasai..maana inatumika sana Arachuga na kwenye wilaya zake.
 
Baba mzazi, hiyo kitu niliiona arusha aisee, its very common. Kuna ndugu yangu mwanae anatumia (we are a
agemates). Niliishia.kumuambia hata bibi yako tu hadi anakufa hajawahi tumia ugoro, alikuwa anaongelea kama vitu vya wazee, wewe na elimu na kuzaliwa mjino unatumia? Ni zombii flani.
 
Siku moja nikafeel harufu nzuri ya kahawa iliyoandaliwa kienyeji na inauzwa maeneo ya soko kuu nikatafuta parking nikaenda kununua kwa wale wauzaji, niliponea kununua ugoro kwani nilichota na kunusa bila kujua, kilichotokea ni chafya na matapishi.
 
vijana wanatafuta kuwa wazee kwa lazima . hii kitu inamumnywa sana A town . ni aina flani ya ulevi wakiduanzi .
 
Ugoro ni kweli umeshamiri sana arusha,na mirungi pia usisahau,wanakoboa kwenda mbele,big G na coca kwenda mbele plus ugolo na bia kazi ipo!kizazi hiki ni hatari tupu
 
ukiishi arusha na usipokuwa makini utaonja kila kitu.unga ndo sijawahi kuuona LIVE mitaani arusha,,,sio bure ndo maana kuna crimes nyingi sana,Piwa,Dadiii,Ngisugii,Boboo,Veve(mirungi),Bange,Gundi,Kiroba oriGINal, na Denge ni vitu common sana...Karibuni Geneva,sio bure rais anapapenda.labda anatumia,,,,teh
 
nimekuwa nafanya kazi na wafanya kazi wezangu wa arusha kwenye kampuni ya mpawa wenyewe wako karibu asilimia 95% katika kampuni karibu asilimia 80 wanakula ugoro vijana ambao ni chini ya miaka 23 nilishangazwa na hili jambo sana yani meno ya mbele yashabadilika rangi kabisa,hamfai hata kuigwa mnakuja kazin mmelewa mnatia aibu yani wanatema mate kama adi kinyaa
 
wenyewe tunaliita dongo wametuzuia kuberi tumehamia kwenye ugoro ni kutema mate kama wamama wajawazito

ugoro nuksi
 
Back
Top Bottom