Vijana tunaikwamua nchi yetu na sera za mfumo upi? Ujamaa/ubepari

WAZIWAZI

JF-Expert Member
Mar 10, 2014
1,806
1,558
Mwalimu Julius Nyarere aliopoamua kuanzisha mfumo wa kiuchumi wa ujamaa na kujitegemea mara tu baada ya Tanganyika kupata uhuru wake mwaka 1961, jamii kubwa ya watanganyika walipata matumaini mapya kwa kile walichoamini kuwa wakati wa kuondokana na maisha ya matabaka ,unyonge na unyonyaji, ulikuwa umefikia tamati na hivyo kuanza mwanzo mpya.

Mwalimu kama wengi walivyopenda kumuita, wazo la kuanzisha na kutetea sera za ujamaa na kujitegemae hakuzitoa akilini mwake au hewani, kabla ya hapo alikuwa ameshafanya tafiti kutoka falsafa za waasisi ambao ni magwiji wa ujamaa duniani kama akina Adam Smith, David Ricardo, Milton Friedman, Fredrich Hayek, Ayn Rand Robert Owen, Pierre Leroux na Karl Marx.

Kwa upande mwingine wa shilingi, sera za siasa za ujamaa na kujitegemea, zilikuwa zikipingana moja kwa moja na falsafa na mawazo ya kibepari ya kina Stuart Mill, Albert Einstein, George Bernard shaw, Leo Tolstoy na Emma Goldman ambao katika mazingira ya uchumi wanaheshimika.

Mwalimu nyerere alitumia muda, akili, fedha na rasilimali nyingi kuwasilisha na kuwashawishi watanzania kuupokea na kuukubali ujamaa na kujitegemea. Mambo hayakwenda vizuri katika pande mbili.

Mosi, kutokana na hali ya uchumi wa kidunia na nafasi ya ujamaa kwa wakati huo duniani; utekelezaji wa sera za kijamaa ulikuwa ni wa kutoa jasho mmno. Pili watanzania wengi waliupokea ujamaa na kujitegemea kwa shingo upande na wale walioupokea kwa moyo mweupe, inaonekana hawakumuelewa vizuri Mwalimi Nyerere.

Walikuwa na nidhamu ya woga. Upande wa kwanza ni nafasi ya ujamaa duniani wakati mwalimu alipokuwa anauleta ujamaa ulikolezwa na mapambo (Ujamaa na Kujitegemea) hapa Tanzania. Ukweli ni kwamba hadi kufikia miaka ya 1950 Ujamaa ulishakuwa kwenye hali mbaya ya kumalizikia kuanguka.

Hii ina maana kuwa Mwalimu Nyerere anajaribu bahati yake ya kuijenga Tanzania imara kiuchumi kwa kutumia mfumo wa uchumi uliokwishakuwa katikati ya changamoto kali za kushindwa.

Usahidi wa kushindwa kwa ujamaa katika miaka hiyo, tunaupata kutoka kwa mataifa tunayoweza kuyaita waasisi na miamba wa Ujamaa duniani. Gazeti la Urusi liitwalo Pravda la Mei 1988 liliandika habari ya kitafiti kuhusu hali tete ya uchumi wa Umoja wa Urusi kutokana na kufuata sera zaUjamaa.

Katiaka habari hiyo, Pravda ilithibisha kuwa matarajio ya wajamaa yanazidi kuyeyuka kutokana na matokeo mabaya kwenye uchumi. Kwa mfano , ilielezwa kuwa kati ya sekta 170 zilizoainishwa kuboreshawa na ujamaa wao, hakukuwa na hata moja iliyofanikisha malengo walau kiasi cha kuridhisha. Gazeti hili lilihitimisha kwamba mfumo wa ujamaa ni sawa na machafuko yaliyokusudiwa.

Kunako mwaka 1920 wakati wa utawala wa Lennis Bolsheviks kule Urusi, tayari wanauchumi wengi akiwamo wa kiaustralia Ludwig von Mises, walieleza kwa kina kuwa Ujamaa ulishaanguka hata kabla haujaanguka.

Kwenye machapisho yake mawili maarufu aliyowahi kuyachapa "Econonomic Calculation in the Socialism Commonwealth" na " Socialism: An Economic and Socialism Analyisis" mwanazuoni huyo wa uchumi ananukuliwa kusema kuwa . kutokana na tabia, tamaduni, mazoea na asili ya mwanadamu; kufanikisha Ujamaa duniani ni sawa na kuitengeneza sanamu kisha kutaka uipe uhai.

Tunafahamu kuwa vita kubwa ya wafuasi wa Ujamaa na wale wa ubepari chimbuko lake ni mgawanyo wa rasilimali zilizopo katikati ya wanajamii. Ubepari wenyewe una sifa ya kuruhusu watu binafsi kuendesha uchumi kwa watu binafsi kumiliki njia kuu za uzalishaji. Ubepari wenyewe ni kwamba serikali inatakiwa kubaki kama mwangilizi tu na inapaswa kuliacha soko lenyewe kuamua.

Wakati ujamaa ni kitendo cha kuhakikisha kuwa, njia kuu za uchumi ni lazima zimilikiwe kwa pamoja na kwa ushilikiano na serikali iwe na mamlaka kamili ya kuingilia chochote katiaka mwenendo wa kiuchumi. Ujamaa wa Mwalimu , alipoibuka na mfumo wa ujamaa na aliuongezea viungo kwa kuuita "ujamaa na Kujitegemea"
Lengo la Mwalimu ilikuwa ni kuona Tanzania kama Taifa likisimama na kumudu mahitaji yake na watu wake pasipo kutegemea fadhila , kuombaomba ama misaada.

Yakafanyika mambo lakini makubwa mawili ni kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa na kutaifishwa kwa mali binafsi kuwa za Umma. Nia ilikuwa nzuri lakini matokeo ya hatua hizi hayakuwa mazuri pengine kwa sababu wananchi hawakuelewa vema Ujamaa na Kijitegemea. Kutokana na hili, maelfu ya wananchi hasa wale walioamishwa makazi, walipotelewa na mifugo yao, waliotakiwa kuacha mashamba na mazao yao na kwenda kwenye vijiji vya ugenini , waliuchukia Ujamaa na Kujitegemea katika hatua za awali kabisa. Hata ubnafsishaji wa mali binafsi zikiwamo hospitali, shule, viwanda, kampuni, na mashirika ulileta kizaazaa kwa sababu wamiliki wake walikuwa na wafuasi wengi na kama hawakuridhika basi na wafuasi wao waliuchukia Ujamaa na kujitegeea wakati unaanza.

Mwalimu alopoamua kung'atuka madarakani bila watu kutarajia, nchi kwa vyovyote vile ilikuwa haina ujanja zaidi ya kujisalimisha kwenye makucha ya Benki ya Dunia (WB) na shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Ilikuwaje taifa la ujamaa na kujitegemea likashindwa kujitegemea? Jibu ni kwa sababu wananchi wake katika ngazi ya mtu mmjo mmoja walikuwa hawajitegemei. Badala yake walikuwa wakitegemea Sertikali kwa kila kitu.
Mchumi na mwanasaikolojia John Stuart Mill, katika kitabu chake cha "Principle of Political Economy(1848) anasema "ukimlazimisha mwanadamu awe sawa na wengine, afanye kila kitu kwa kuamuliwa na mamlaka, basi atakuwa na hulka zifuatazo:

Atakuwa mtu anayefanya mambo nusunusu (passive), hatafanya mambo makubwa zaidi ya yale wanayofanya wenzie, hata kama ana uwezo na kubwa zaidi hataona umaana wa kujipambanua katika kazi kwa sababu iwe atafanya sana ama atafanya kidogo, masilahi anapata yaleyale"

Kivuli, kovu na woga kuhusu hekaheka za ujamaa bado zinafuata hadi leo ndio maana hapa nchini mtu anapofanikiwa kiuchumi kwa njia moja au nyingine watu hawamwamini na sanasana wakimhurumia watamwita fisadi

Baada ya Mwalimu kung'atuka na mrithi wake Rasi wa awamu ya pili ,Ali Hassan Mwinyi, kushika hatamu yeye naye kama mwanadamu wa kawaida, alikuwa na vidonda vilivyotokana na mkwiji wa ujamaa na kujitegemea.
Kuthibitisha hilo, Julai 2008 alikaririwa akisema, ujamaa ulikuwa hautekelezeki na kwamba, ulikuwa mfumo mzuri lakini ulikuwa unapingana na uasili wa binadamu.

Kwa asili, karibu watu wengi wanapenda kuwa matajiri. Hwataki kuwa masikini kwa maisha yao yote. Msingi mmoja wa UJamaa ulikuwa ni kwamba, kusiwepo pengo kubwa kati ya matajirinna masikini, pengo ambalo hivi sasa linazidi kuongezeka kadri siku zinavyokwenda kwa wachache wakiwa wamejilimbikizia mali na masikini wakiendelea kuogelea katika ufukara wa kutisha.

Wakati huo Mzee Mwinyi maalufu kama Mzee Ruksa aliwahi kusema, Tungeweza kuendelea na sera ile au kufanya mabadiliko?... Ujamaa kweli ulikuwa unafanya kazi 1980? Lakini ukiniuliza kama ujamaa ulikuwa mbaya? Nitakwambia , ni siasa nzuri duniani. Tatizo lake ni kama ndoto ", alikaririwa akisema siku ya uzinduzi wa kitabu chenye maoni ya wakuu 13 wa nchi za Afrika akiwemo yeye mwenyewe na Raisi aliyemfuata Benjamini Mkapa.
Itakumbukwa kwamba, sera na mipango aliyoianzisha Rais Mwinyi , ikafuatwa kwa kasi kubwa na Rais Mkapa aliyefuatia viongozi hawa wawili walijikuta wanalazimishwa na wakati wa uchumi wa dunia kufumba macho na kuua ujamaa na hatimaye kuuzika ingawa ulimgharimu vilivyo Mwalimu.
Mwalimu mwenyewe baada ya mambo kumchachia na akawa hana jinsi, aliwahi kukaririwa na jarida la New Internationalist, toleo la 309 la January-February 1999 (wakati huo akiwa msuluhishi mkuu wa mgogoro wa Burundi) akisema kwamba ujamaa haukushindwa duniani, isipokuwa haukuwahi kujaribiwa, wakati Fulani 1995, mwalimu mwenyewe alisema.......

"siku hizi ukianza kujadili Ujamaa, inabidi uwe na akili kama za mwendawazimu lakini mimi sioni haya kuyazunguimzia mambo haya hasa ya Azimio la Arusha na maana zake"
Korea ni mojawapo ya mataifa ambayo Mwalimu enzi za uhai wake alipata kwenda kuchukua falsafa ya ujamaa na kujitegemea hasa katika maeneo ya kilimo na maendeleo ya viwanda.

Najenga hoja yagu kwa kusema kwa kadri nchi inakoelekea je ni vema tukarudia azimio la Arusha au tusonge mbele na mfumo tulionao sasa ambao kwa asilimia kubwa ni koti la ubepari?... karibuni tujenge hoja hasa vijana ambao ndo tunatakiwa tuchukue nchi yetu mapema kabisa baada ya wazee kutufikisha hapa, sasa watue mzigo wapunzike.

chanzo habari leo 2013
 
Vijana mada ipo mezani karibuni wakati wenyewe ndo sasa.
 
Koo
ukitaka kumficha kitu mwafika basi uandike page ndefu kama hiyo. Alieturoga mh!!

Ujamaa umeshindwa (Eastern Europe etc), lakini hata hao makuwadi wa free market aliowanukuu WAZIWAZI , ambao ndio miamba ya libertarianism, wamefeli vibaya sana kwa mujibu wa mitikisiko ya uchumi ya miaka ya mwanzo ya karne hii.

Kuna njia ya kati inayojumuisha ubepari unaowekewa mipaka na serikali unaoweza kutoa nafasi kwa mifumo ya kijamii yenye sura za kijamaa bila kuathiri biashara huru yenye adili inayoweza kuwa nzuri zaidi.

Nimemsoma von Mises kwenye "Human Action" na vitabu vyake vingine, Hayek, (AdamSmith, Ricardo, Malthus since high school), Friedman mpaka Leonard Reid na jinsi walivyo influence Reaganomics. I went to their black tie affairs parties and hobnobbed with the likes of Vaclav Klauss. I read their almost religiously dogmatic publications. I penetrated their organizations and checked out their greedy motivation far and above any sliver of academic facade. Theirs was as much of a utopia as Bolshevism and Communism.

If these people had their way we would probably be still under slavery, and the UN would have been an academic abstract.

Kabla ya kututukana kwamba hatusomi qualify your statement.

Mmesoma the new Piketty?

Cc WAZIWAZI
 
Last edited by a moderator:
Mkuu WAZIWAZI heri yako kwa uzi mzuri! Kabla ya yote kwanza ningeomba kusema haya mafupi!

Tunaposema MFUMO hasa unaongoza nchi, ni wazi tunazuzungumzia interconnected elements/policies over all aspects of life kwa maana Uchumi, Siasa, na Utamaduni katika eneo mahususi. So, katika kuchagua ama kubuni mfumo wa kufuata hatuna budi kufuata au kubuni ule utakaokuwa na common elements katika nyanja zote, kulingana na Mazingira na Nyakati zetu mahususi kwa eneo letu! Yaani, tusije kuwa na mfumo utakaohimiza uvuvi hali kuwa tunaishi jangwani pasipo na maji!
So, ujamaa ni sahihi na ubepari vilevile, je ni relevant kwetu au copy and paste style?
Pia Ujamaa na Ubepari si mwisho wa mifumo, muhimu ni kuzingatia mazingira na nyakati zetu katika kuchagua au kubuni njia ya kufuata!
Ubunifu haujawahi kufika mwisho, Nguvu yetu ni Umoja na Kuthubutu! Nitarudi Mkuu!
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani! Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
WAZIWAZI umeandika...

Mwalimu kama wengi walivyopenda kumuita, wazo la kuanzisha na kutetea sera za ujamaa na kujitegemae hakuzitoa akilini mwake au hewani, kabla ya hapo alikuwa ameshafanya tafiti kutoka falsafa za waasisi ambao ni magwiji wa ujamaa duniani kama akina Adam Smith, David Ricardo, Milton Friedman, Fredrich Hayek, Ayn Rand Robert Owen, Pierre Leroux na Karl Marx.

Mtu akishaandika sentensi kama hii tu najua hajui ameandika nini, kanukuu sehemu tu na kutafsisri bila kuelewa.

Adam Smith Milton Friedman, Fredrich Hayek, Ayn Rand ni magwiji wa Ujamaa?

Umesoma kazi zao gani zilizokuonyesha hivyo?

Unaujua Ujamaa? Hawa watu umewasoma kweli au ume copy/ translate/paste tu?

Ayn Rand gwiji la Ujamaa? Umesoma "Atlas Shrugged"?

Adam Smith gwiji la Ujamaa? Umesoma "The Wealth of Nations"?

Fredrich Hayek gwiji la Ujamaa? Umesoma "The Road To Serfdom"?

Milton Friedman gwiji la Ujamaa? Umesoma "Capitalism and Freedom"?

Kifimboplayer nani anahitaji kusoma sasa?
 
WAZIWAZI umeandika...



Mtu akishaandika sentensi kama hii tu najua hajui ameandika nini, kanukuu sehemu tu na kutafsisri bila kuelewa.

Adam Smith Milton Friedman, Fredrich Hayek, Ayn Rand ni magwiji wa Ujamaa?

Umesoma kazi zao gani zilizokuonyesha hivyo?

Unaujua Ujamaa? Hawa watu umewasoma kweli au ume copy/ translate/paste tu?

Ayn Rand gwiji la Ujamaa? Umesoma "Atlas Shrugged"?

Adam Smith gwiji la Ujamaa? Umesoma "The Wealth of Nations"?

Fredrich Hayek gwiji la Ujamaa? Umesoma "The Road To Serfdom"?

Milton Friedman gwiji la Ujamaa? Umesoma "Capitalism and Freedom"?

Kifimboplayer nani anahitaji kusoma sasa?

Mkuu mbona unaleta mabishano na kejeli! ok huenda wewe unajua zaidi ya sisi au umesoma vitabu tofauti na tulivyosoma sisi tufundishe ukijikita kwenye mada ya msingi.
The word is like a book if you don't travel you will read only a page. pekua zaidi mkuu usiatamie hayo uliyoyasoma huenda umesoma dondondoo tu ila hongera kwa kupenda kujisomea.
 
Mkuu mbona unaleta mabishano na kejeli! ok huenda wewe unajua zaidi ya sisi au umesoma vitabu tofauti na tulivyosoma sisi tufundishe ukijikita kwenye mada ya msingi.
The word is like a book if you don't travel you will read only a page. pekua zaidi mkuu usiatamie hayo uliyoyasoma huenda umesoma dondondoo tu ila hongera kwa kupenda kujisomea.

Post yangu #4 hapo juu nimejibu hoja kuu.

Tumeambiwa Waafrika hatusomi post ndefu, nikaisoma post ndefu nikaona ina madudu, mtu kajaza mijina tu, na kusema hawa watu ni magwiji wa Ujamaa, bila hata kujua hao watu wameandika nini.

Sasa kwa kuwa mimi nimewasoma hao watu, na nishatukanwa kwamba sisomi, nikaona nikuulize wewe uliyeonekana umesoma ukaleta post ndefu ya copy translate paste hapa, hao watu umewasoma au umetujazia majina tu?

Unajua ulichoandika au umeokoteza mambo tu, ukaweka hasi chanya, chanya hasi, halafu utegemee umeme uwake?

Napata shida kukuchukulia seriously kama unaniambia kwamba hao unaowaita magwiji wa Ujamaa unafikiri kweli ni magwiji wa Ujamaa.

Unanionyesha kwamba hujawasoma, umeokoteza habari tu.

Sipendi watu wanaojitutumua kuonekana wamesoma vitu ambavyo hawajavisoma na wala hawavielewi hata kwa kuanzia tu.

How could you say Adam Smith, Ayn Rand, Hayek, Friedman etc ni "magwiji wa Ujamaa" ?

Utumbo gani huu?

Unaelewa unachoandika au una parrot watu tu?

Some of us actually read these people, we are not just namedropping without understanding like you.

CC: King'asti
 
Last edited by a moderator:
Habari hii ipo word for word hapa

http://habarileo.co.tz/index.php/makala/18600-ujamaa-na-kujitegemea-bado-una-nafasi-katika-jamii

WAZIWAZI wewe ndiye muandishi?

Au ni copy/ paste tu, ndiyo maana hata maswali unashindwa kujibu?

mkuu kwani hata kama nimepata kwenye link hiyo kuna tatizo gani kuileta hapa jukwaani? si ndio kujisomea kwenyewe! pili swali gani nimeshindwa kujibu? pili na link hiyo unabishana nayo kwamba hao sio magwiji wa ujamaa? tatu wewe hivyo vitabu ulivyonukuu uliwasaidia kuandika au ulicopy na kupest?
 
mkuu kwani hata kama nimepata kwenye link hiyo kuna tatizo gani? kuileta hapa jukwaani? si ndio kujisomea kwenyewe! pili swali gani nimeshindwa kujibu? pili na link hiyo unabishana nayo kwamba hao sio magwiji wa ujamaa?

Ukileta makala ya Jenerali Ulimwengu hapa, bila kutuambia kwamba hiyo ni makala ya Jenerali Ulimwengu umetuletea, hiyo ni plagiarism.

Utakuwa unajinadi kwamba wewe ndiye muandishi wakati sivyo.

Sasa tueleze, wewe ndiye muandishi au ume copy paste tu?
 
Ukileta makala ya Jenerali Ulimwengu hapa, bila kutuambia kwamba hiyo ni makala ya Jenerali Ulimwengu umetuletea, hiyo ni plagiarism.

Utakuwa unajinadi kwamba wewe ndiye muandishi wakati sivyo.

Sasa tueleze, wewe ndiye muandishi au ume copy paste tu?
mbona hujibu hiyo link unabishana nayo ya habari leo? ok ngoja nifanye utakavyo umeridhika?
 
mbona hujibu hiyo link unabishana nayo ya habari leo?

Nijibu mara ngapi?

Nishakwambia nishajibu kwenye post #4 hapo juu.

Wewe mbona hunijibu swali langu?

Wewe ndiye muandishi au plagiarist uliye copy/paste bila kutoa credit tu?
 
umeridhika

Umeridhika wewe ambaye umeulizwa swali hujajisumbua hata kujifanya unalijibu.

Wewe ndiye muandishi au plagiarist tu?

Nashindwa hata kuzama zaidi katika ku discuss Austrian Economics bila kujua uwezo wako.

Na kwa habari hizi za kusema Ayn Rand ni gwiji wa Ujamaa, we na huyo muandishi wote ni plagiarists tu.
 
Back
Top Bottom