Vijana nao wamtolea uvivu Mzee Moyo; Alisherehekea vifo vya K. Hanga na O. Sherrif!

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Wanasema kuwa Mzee Moyo:

  • Sio Mwana-mapinduzi wa kweli na hakuyajua Mapinduzi ya 1964
  • Mwezi mmoja kabla ya Mapinduzi ya 1964 alikipiga pande chama cha ASP
  • Alisherehekea kifo cha Wazanzibari Wana-mapinduzi cha akina Hanga na Othman Sherrif

moyo.png


Pichani: Mzee Moyo akiwataka Vijana kuendelea na harakati za ukombozi wa nchi ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar

Zanzibar, Tanzania | Na Geofrey Kimbitikiri | Zanzibar Yetu


Katika mgeuko wa maneno vijana wa kizanzibari katika tovuti lao la Mzalendo.net wakitoa maoni yao chini ya mada – "Muungano waibua mpasuko CCM Zanzibar" iliyotoka kwenye gazeti la NIPASHE, wamemshambulia vikali kikongwe wa CCM Bw. Moyo kwa kile walichokiita kuwa Bw. Moyo ni mwenye siasa ya kurukaruka.

"Ni kweli tumshukuru Mzee Moyo kwa kutuunga mkono katika hii vita yetu ya ukombozi, lakini tusimuamini sana huyu Mzee, kwani huu ndio mtindo wake. Kila akiona jahazi karibu ya kuzama huwa anarukaruka. 1964 alifanya haya haya dhidi ya ASP na tukiwauliza wazee wa mitaani watatueleza zaidi."

Muandishi wa maoni haya anasema kuwa anashangazwa kuwa leo Mzee Moyo anataka Muungano wa Mkataba, kwani hataki Zanzibar igubikwe na Bara. Huo ndio ulikuwa msimamo wa akina Hanga na Othman Sherrif. Walipomuona Karume anazidi kuelekea Bara wakataka kumsimamisha na hapa ndipo walipokutwa na vifo vyao.


"Zaidi kinachonishangaza mimi ni kuwa haya haya anayoyaunga mkono yeye leo ndio akina Hanga na Othman Sherrif wakiyapigania", anafafanua muandishi chini ya jina la kipiganaji (nom de guerre) la Saidi Sudi – ambalo ni jina la mwarabu maarufu wa zamani aliekuwa akiitikisha Unguja enzi zilizopita.


Muandishi anaendelea kuandika kuwa Bw. Moyo alishiriki katika mauaji ya Wana-mapinduzi hawa wawili, yaani Bw. Abdallah Kassim Hanga na Othman Sherrif na siku ya mauaji hayo Bw. Moyo alivalia nguo za kijeshi akiwa na bastola kiunoni. Siku hio kama inavyojulikanwa kulikuwa na curfew Unguja nzima.


"Eh Mzee Moyo we, kaa kimya mzee wetu upate kusitirika!", alimalizia maoni yake muandishi huyo.
 
Nilivyosoma historia ni kuwa Mzee Karuma alitaka Mzee Hassan Moyo awe naye lakini wengi Wanamapinduzi wakati Ule

Ambao walikuwa ni Waafrika Hakumpenda...
 
Mwandishi Saidi sudi anajulikana wala si jina bandia. Ni jina lake na ni mwana CCM kigogo eti na yeye anasema pia.?.
 
Huyu Mzee kweli mwacheni apumzike na mwambieni achutame ili asiadhirike wakati watakapomvua nguo, Mzee huyu kaka Dodoma miaka ya 1978-1985 na mke wake alikuwa Mwl wa shule ya Msingi Amani, kafaidika na wamefaidika sana enzi hizo huku bara leo hataki wapemba nao wafaidi, basi vunjeni ila ajiandae kuwapokea na aliowaacha huku
 
Kutoka CIA fact book:-

Although Zanzibar's union with Tanganyika was in​
his interests-ind as much as it got Babu off the island--Karume apparently was not initially enthusiastic about the idea; certainly, he was not as strongly infavor of the union as Hanga, who claims that he and Kambona agreed when they werestudents together in London that Tanganyika and Zanzibar should be united one day, The idea of as a union was not a new one.

Nyerere probably
had
it in the back of his mind when he first became involved in Zanzibar politics, beginning around 1956. For years he had looked forward to the time when an African government would.come to power in Zanzibar, at which time he planned tomerge the two countries . His feeling of urgency about the union in March and April 1964 was probably a reflection of his concern that Babu was well on his way to consolidatinghis position in Zanzibar and his beleif that only decisive action taken in time could save Zanzibar's African revolution from Arab control ..,
 
Back
Top Bottom