Vijana na Tanzania ya kesho.

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,118
1,966
Mimi ni mmoja wa vijana wa taifa hili ambaye kwa hakika ndoto yangu ni kuona mabadiliko na demokrasia ya kweli inakuwepo kwenye taarifa hili.

Pengine ninachokiona wengi wakiwemo viongozi hawajakiona au kama wanakiona wanakipuuzia.Ni ukweli kwamba vijana katika taifa hili ndo wengi kuliko kundi lolote.

Tatizo ninaloliona vijana wengi tuna NJAA,njaa ni tatizo kubwa,mlo si wa kuaminika.Ni njaa hii inayotufanya tuwe na demokrasia ya msimu,ni njaa hii inayotufanya kushindwa kulinda kura kwa kupew sahani ya ubwabwa,ni njaa hii inayotufanya kushindwa kutambua haki zetu za msingi kwani akili nzuri na maono huja kwa mtu aliyeshiba.

Kwa wale wabunge ambao wametoka kwenye vyama mbadala anza mkakati wa kuwaandaa vijana waondokane na njaa,ukimwinua kijana akashiba amani na demokrasia itakuwepo.

Tunayo mapori ya kutosha,tunayo mabonde ya kutosha,na mito yenye maji mwaka mzima, nashindwa kuelewa kwanini ubunifu tena wa gharama ndogo viongozi wanaukosa.

Nina imani bila kuwa na mkakati wa maana,tusitegemee mabadiliko ya maana,upo uwezekano mkubwa maneno ya Lowasa kutimia kuwa ukosefu wa ajira ni bomu lililosubiri kulipuka.

Tutaitisha mikutano mingi,maandamano mengi na mikusanyiko ya kila aina.lakini watu wenye kukusanyika, kuandamana ni watu wenye matumaini dhaifu, imani dhaifu na yenye kuyumba. Inawezekana ukawa mtaji wa kisiasa lakini ikawa ni kwa muda mfupi,si ya kudumu.

Shime viongozi vijana na vyama mbadala,CCM ilishshindwa onyesheni njia katika hili.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom