VIJANA na SIASA

jamani mbona tuna vijana wegi tu....watoto wengi wa viongozi wetu wapo kwenye nafasi tofauti tofauti za kisiasa..huenda hawa baadae wakaja pia kuwa viongozi wa juu wa nchi..lakini pia tunao vijana wengine pia wanao-onyesha interest na siasa...ngoja tuone 2010 watakaojitokeza,......
 
jamani mbona tuna vijana wegi tu....watoto wengi wa viongozi wetu wapo kwenye nafasi tofauti tofauti za kisiasa..huenda hawa baadae wakaja pia kuwa viongozi wa juu wa nchi..lakini pia tunao vijana wengine pia wanao-onyesha interest na siasa...ngoja tuone 2010 watakaojitokeza,......
mhhhhh?
 
Hivi kumbe A.Mashariki ina nchi hizi..!

Vijana wanafaa kutumikia taifa lao kwa kaajili ya nguvu walizo nazo zaidi, lakini si kwenye ngazi za juu za maaamuzi, MAANA HUKOWATAKOROGA.

Ni ukweli uliositirika kwamba maamuzi mengi ya vijana yana mwelekeo wa jazba na uharaka usio na maana!

Ukiamua kuingiza vijana kwenye ngazi za maamuzi, lazima wawe na back-up ya nguvu kabisa ya wazee.

Ukiona Mbunge kijana sana ujue kwamba amechaguliwa na kundi la vijana wenye hasira ya maisha, ambao wanadhani kijana mwenzao atawaelewa hatraka na kuwasaidia.

My take-
Vijana wawe groomed kushika nafasi za uongozi, na si kutoka masomoni au uraiani direct na kuwa viongozi. Mifano ni kama ya akina JK, ambao wamekulia kwenye Siasa!

Si kweli!

Vijana wanaweza. Uongozi ni kipaji na wala mtu hapaswi kuwa groomed ndio awe kiongozi bora.

Vijana wenye kuonyesha uwezo wa uongozi hawana budi kugombea ili Taifa liwe na viongozi wengi vijana watakaotoa changamoto ya kweli kwa kuwa na mawazo mapya na nguvu mpya.
 
Si kweli!

Vijana wanaweza. Uongozi ni kipaji na wala mtu hapaswi kuwa groomed ndio awe kiongozi bora.

Vijana wenye kuonyesha uwezo wa uongozi hawana budi kugombea ili Taifa liwe na viongozi wengi vijana watakaotoa changamoto ya kweli kwa kuwa na mawazo mapya na nguvu mpya.
Boramaisha,
Hoja yako ina ukweli sana.
Kujitokeza kugombea ni muhimu badala ya kukatatamaa.
 
Mimi si kijana naheshimu sana michango yenu na Taifa linawahitaji mtafanikiwa mkitambua Siasa ni sanaa sio kila mmoja anaweza kupiga gitaa au kuimba. Siasa sio laptop na internet mkadhani utafanya siasa kwa kuandika nadharia mkijua siri ni kwenda kuishi na watu na kujua shida zao na wewe ukawa sehemu yao wakakuamini, ukawa jasiri kuwasemea matatizo yao watakupa nafasi ya kuwa kiongozi wao vinginevyo mtabakia kuwa watazamaji siku zote
 
Sio realistic kuwa vijana kati ya miaka 20 hadi 30 waingie kwenye siasa na kuwa viongozi wakubwa katika nchi. Hiyo miaka ni miaka ambayo kijana bado anashughulikia mambo mengine muhimu kama kusoma na kujenga familia ( kuoa au kuolewa).
Maana kuingia kwenye siasa bila misingi hiyo mara nyingi ni matatizo. Nakubaliana na Adolf Hitler ambaye katika kitabu chake "Mein Kempf" au My struggle, ameshauri kuwa mtu aingie kwenye siasa angalau akifikia miaka 30 , maana kabla ya hapo mafanikio huwa ni madogo na inahitaji kipaji cha hali ya juu, na sio wote wanaweza kuwa na vipaji kama hivyo. Wengi wanaojitosa bila kutafakari huishia kwenye matatizo makubwa ikiwa na pamoja na kuuawa, maana hawajajua mchezo huu...POLITICS..!
Hivyo basi, is just Ok, kuona kuwa vijana wachache sana wanaingia kwenye siasa katika umri mdogo..!
 
Hao wazee unaowaona katika siasa sasa hivi, walianza wakiwa vijana. Nadhani issue hapa si kwamba vijana hawahusishwi, pengine vijana wengi wa umri huo sasa hivi hawajihusishi na siasa.

FM;
Unajua siku zile vijana hao walikuwa na mtizamo wa ukombozi wa Bara la Africa na hata baada ya ukombozi , vijana wengi waliendelea kupigania mataifa yao katika kuyakomboa na umaskini.

FM; mgogoro ulianza pale tu baadhi ya wale vijana wa zamani(wazee) walipoanza kujilimbikizia mali na hapo ndipo waluianza kuziba mianya ya vijana wa sasa(leo) na ndipo waliposema kijana hana nafasi tena katika uongozi wa Taifa hili.

FM; nadhani kuna kila sababu kutoa elimu kwa wazee wetu na pia kuwaelimisha vijana kuhusu suala zima la uongozi wa Taifa lao na sio vinginevyo.
 
..tatizo wote mnataka kujiunga na CCM.

..NCCR,TLP,UDP,CCJ, etc wapo wanawasubiri mjiunge nao.
 
Hata vijana wanakuwa wagumu sana kushiriki katika siasa, yaani hawana mkakati wao wa kuwezesha kuingia kwenye siasa
 
mfumo ndio unakuza viongozi, si kweli kua viongozi wanazaliwa ivyo, ni system ndio inawakuza, wale vijana wa enzi za mwalimu aliwajenga ndio wakawa viongozi wazuri, kwa sasa vijana wako bize na facebook,twitters, bongo fleva nk ni wachache sana wenye mtazamo wa kuangalia dunia inaendaje na awe mzalendo, wengi ni machewk bob tu wakipewa uongozi wanataka iwe ndio tiketi ya kutafutia wasichana!
wachache ambao wana uwezo kuingia kwenye mfumo wanabaniwa na wazee wachache wenye umoja kwa sababu vijana hawana umoja na vision kuwapiku ni ngumu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom