Mwanajamii
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 7,063
- 68
Nchi yetu ina vijana wengi sana Wasomi , wengine wanaendelea kusoma, vijana wenye nguvu za kufanyakazi za ujenzi wa Taifa la Tanzania. Jambo la kushangaza ni kwamba elimu yote tuliyo nayo kama vijana, nguvu zote tulizonazo pamoja na fursa nyingine nyingi kama vijana , vyote hivyo vimeingiliwa na watu ambao aidha wanaonekana wana uelewa zaidi kuliko sisi vijana ama wanafanya makusudi ili mradi tu malengo yao yaweze kutimia. Vijana tumekuwa msatari wa mbele kuhamasishwa kutumia nguvu zetu, elimu tuliyo nao kufanya mambo ambayo kwa namna moja au nyingine ni wachache watakaonufaika nayo. Tumekuwa mstari wa mbele kujihusisha katika migomo ambayo siyo ya lazima, maandamano yasiyo ya lazima na hata kufikia hatua ya kutoa lugha chafu kwa Wazazi wetu, wakubwa zetu, viongozi wetu wa dini na hata wa Serikali. Je Mwisho wa siku tutamlaumu nani? ni mara ngapi tumetumia elimu na nguvu tulizonazo kushiriki kwenye makongamano, shughuli za uzalishaji mali, ushauri , ili nafasi yetu kama vijana iweze kuonekana katika jamii? Tutafakari hili vijana wenzangu ili nafasi yetu katika jamii iwe chachu ya maendeleo, amani na utulivu katika Taifa letu la Tanzania. Tutambue kuwa itikadi za kidini, kisiasa hupata msukumo wa nje kwenda kwa watu maarufu lakini kupitia kwa vijana kama ngazi ili mradi tu hawa watu wa nje pamoja na wafuasi wao watimize haja zao huku wakiacha kundi hili likiangamia.