wakimaliza tu, CDM nao waandae ya kwao halafu uone vijana wa Dar wako upande upiMAANDAMANO ya kuunga mkono hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa mwishoni mwa mwezi uliopita, yanatarajiwa kufanyika Dar es Salaam Machi 16, mwaka huu, yakiwa na ujumbe ‘amani yetu bado tunaipenda'. Akizungumza na waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana wa Tanzania, wapenda amani, Said Mwaipopo alisema, pia maandamano hayo yatahusisha kupinga kauli viongozi wa CHADEMA zinazochochea kutokea kwa vurugu nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti huyo, inaeleza kuwa, vitendo na kauli za viongozi vya chama hicho vina lengo la kupandikiza chuki kwa Watanzania dhidi ya serikali iliyopo madarakani, ambavyo mavuno yake ni umwagikaji wa damu.
Alisema, maandamano yanayofanywa na CHADEMA huvishwa sura ya kupanda kwa gharama za maisha, wakati huohuo yakiwa na lengo la kuipinga na kutaka kuing'oa serikali.
Maandamano hayo yatafanyika kuanzia viwanja vya Mnazi Mmoja mpaka uwanja wa Bakhresa Manzese, na Mwenyekiti wa TLP Augustino Mrema anatarajiwa kuyaongoza.
source: www.uhurupublications.com
Tatizo langu si kuandamana waacheni waandamane, wasiwasi wangu ni kwa Mh. Mrema kweli ataweza kutembea toka Mnazi Mmoja hadi uwanja wa Bakhresa Manzese, akiweza nitaamini dawa ya mzee wa Lindo inaponya.Hivi Mh. Mrema (Mb. TLP) ni kijana au ndo mlezi wa hao vijana? Anyway, Maandamano ruksa, maana huwalazimishi watu kupokea ujumbe na kuutafsiri kama ulivyolenga. Watu wanaona wenyewe kama ujumbe unawagusa au ni uzushi. Wajiandae, Tz ya sasa c ya mwaka 1961, watu walikuwa wanaimba uhuru tu, sahivi tunataka kuona vitu vikifanyika sio tutafanya hili na lile.
Mzee mageuzi1992 hata karatasi nyeupe ilitengenezwa kwa magome ya mti ukiicha maktaba kwa miaka mingi itarudia rangi yake.KIpindi cha nyuma baadhiyetu tuliposema Mrema ni SISIEM tulikejeliwa sana.....HAYA SASA ONENI!!!!!
maandamano ya kuunga mkono hotuba ya rais jakaya kikwete aliyoitoa mwishoni mwa mwezi uliopita, yanatarajiwa kufanyika dar es salaam machi 16, mwaka huu, yakiwa na ujumbe amani yetu bado tunaipenda. Akizungumza na waandishi wa habari mjini dar es salaam, mwenyekiti wa kamati ya vijana wa tanzania, wapenda amani, said mwaipopo alisema, pia maandamano hayo yatahusisha kupinga kauli viongozi wa chadema zinazochochea kutokea kwa vurugu nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwenyekiti huyo, inaeleza kuwa, vitendo na kauli za viongozi vya chama hicho vina lengo la kupandikiza chuki kwa watanzania dhidi ya serikali iliyopo madarakani, ambavyo mavuno yake ni umwagikaji wa damu.
Alisema, maandamano yanayofanywa na chadema huvishwa sura ya kupanda kwa gharama za maisha, wakati huohuo yakiwa na lengo la kuipinga na kutaka kuingoa serikali.
maandamano hayo yatafanyika kuanzia viwanja vya mnazi mmoja mpaka uwanja wa bakhresa manzese, na mwenyekiti wa tlp augustino mrema anatarajiwa kuyaongoza.
Source: www.uhurupublications.com
Ukombozi wa Tanzania na watu wake ni ngumu kwa sababu ya baadhi ya aina yako........! Pengine jina lako lilikosewa kuandikwa vema; "Kash_ga"; Penye ____ panahitaji herufi "o".....!hoja zako zimejaa mashiko
Ukombozi wa Tanzania na watu wake ni ngumu kwa sababu ya baadhi ya aina yako........! Pengine jina lako lilikosewa kuandikwa vema; "Kash_ga"; Penye ____ panahitaji herufi "o".....!
Mnaionaje midomo ya Kashoga, Ephraim Kibonde na James Mbatia? kuna similarity fulani !!!!
Naona kama wamekulia Mombasa vile, hawaeleweki eleweki.