Vijana DAR kuundamana kuunga mkono hotuba ya Kikwete

Kweli inchi hii haitaendelea hata siku moja. Hao watu ni wakuwaangalia sana kwa macho mengi maana ndugu zao wanakufa kwa gharama za maisha zinavyoongezeka wao wanaandamana kupinga nini? Mungu awajalie waanadamane vizuri na malengo yao ya kujipatia pesa toka kwa mafisadi yatimie ile ya kubadiri umma unaopata shida yasitimie.
 
Hii ndiyo kazi yako siyo? Unaonekana wewe si binadamu wa kawaida. Mungu akusamehe.
 
Huoni aibu kutofautiana na wenzio wote walio-comment hapo juu.Nina wasi wasi sana na elimu yako,kama sio std 7 itakuwa madrasa na ndio maana mikoa wanayotoka watu wa dizaini ya kwako ni maskini wa kutupwa na mtaendelea kuwa maskini mpaka mwisho wa dunia.Pole sana jitahidi uende shule ukanoe ubongo wako vinginevyo utaishia tu kuvaa t-shirt na kofia za CCM huku ela zote mkimpa Rostam na wenzie

Msomi hana sifa ya kutukana anapopewa hoja.Msomi hutakiwa kujibu hoja. Kaka umesema mimi nimetofautiana na wengine, nadhani hapa kila mmoja anauhuru wa kutoa mawazo yake. Kwahiyo wewe msomi umejibu kwa kuangalizia? nina wasiwasi na elimu yako, inaonekana ulikuwa mzee wa chabo, una degree ya chabo.wasomi kama wewe hamuhitajiki kwani akili yako huishughulishi kivyako unafata mkumbo. Pole sana.
 
Hao vijana watakuwa sio wa kitanzania. Kila kijana wa tanzania sasa ameerevuka na anajua nchi yetu inavyoelekea shimoni. Labda waandamane watoto wao.
 
1. Kuandamana ni haki yao.
2. Kutoa mawazo yao ni haki yao.
3. Wanachozungumzia ni maisha yao.
4. Watakachosema ni maoni yao.
5. Muda na nguvu watakazopoteza ni vya kwao.
6. Aibu na fedheha watakayopata ni za kwao.
7. Hatutawazuia kwa sababu tunajua wapo.

Ni habari njema sana kama wataandamana siku hiyo. Hii itakuwa nafasi ya pekee kuwajua kwa sura na kuwaona. Itakuwa ni kipimo cha hali ya vijana, uelewa wao, utayari wao kuona mabadiliko nk.

Mh. Mrema Augustine kama atashiriki atakuwa amehitimisha kazi yake atakayokuwa ametumwa. Nitamshangaa sana.

Shida za watanzania si za kuambiwa na CHADEMA, ni shida wanazoishi kila siku. Amani na utulivu vimeletwa na wananchi wenyewe sio CCM. Kikwete alipata kura Mil 5 wananchi wako milioni 30+ sasa iweje hao wachache ndio wameleta amani na utulivu? Hao milioni 25+ wameleta nini?

Tutafurahi kuwaona waandamanaji.
 
Hao vijana watakuwa sio wa kitanzania. Kila kijana wa tanzania sasa ameerevuka na anajua nchi yetu inavyoelekea shimoni. Labda waandamane watoto wao.

wewe unafikiri vijana wote wako tayari kutumika na wanasiasa uchwara wanaojiita wapinzani?? kila mtu anao uhuru wa kuchagua upande gani ausopoti,we unafikiri hali ngumu ya maisha itaisha kwa kuandamana?
 
Ushauri Wa bure MAandamano kwa nchi yetu hayana tija tufanye kazi tuache kutembea ovyo

kuna baadhi ya maandamano yanakuwa na tija na mengine hayana tija. Pia kuna mengine viongozi wake wanapoomba idhini ya kuyafanya huwa na kichwa cha habari kizuri lakini wakisha fika viwanjani wanabadilika na kuwa mbogo kwa kuongea maneno ya kuamsha hisia za vurugu, kwahiyo maandamano ya aina hiyo hayana tija.
 
kuna baadhi ya maandamano yanakuwa na tija na mengine hayana tija. Pia kuna mengine viongozi wake wanapoomba idhini ya kuyafanya huwa na kichwa cha habari kizuri lakini wakisha fika viwanjani wanabadilika na kuwa mbogo kwa kuongea maneno ya kuamsha hisia za vurugu, kwahiyo maandamano ya aina hiyo hayana tija.

baambie bana
 
MAANDAMANO ya kuunga mkono hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa mwishoni mwa mwezi uliopita, .......

....Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana wa Tanzania, wapenda amani, Said Mwaipopo alisema, pia maandamano hayo yatahusisha kupinga kauli viongozi wa CHADEMA zinazochochea kutokea kwa vurugu nchini.....

Maandamano hayo yatafanyika kuanzia viwanja vya Mnazi Mmoja mpaka uwanja wa Bakhresa Manzese, na Mwenyekiti wa TLP Augustino Mrema anatarajiwa kuyaongoza.

Sijawahi kuona ama kusikia wanaCCM wamefanya maandamano wakiwa na ajenda inayowahusu wananchi.
Mara nyingi huwa ni kuunga mkono hotuba, kupongeza kuteuliwa, n.k. Siku zote ajenda yao ni ile yenye kujikomba kwa mkuu wa nchi. Natamani katiba mpya ije haraka ili tu-scrap presidential powers ili rais na bunge wawe wanajikomba kwa wananchi na si kinyume chake.
Vinginevyo wasombe vijana kwenye Fuso kutoka Mkoa wa Pwani na Morogoro, sitarajii maandamano hayo kuwa yenye kufana kama Musoma, Mwanza, Shinyanga, Arusha na Karagwe.

Kamati ya Vijana Wapenda Amani (KVWA) hii huteuliwa na nani mbona ndo inasikika leo. Kazi zake ni zipi?? Amani gani wanyoipenda wao??? Mbona vijana walipouawa Arusha hii kamati haikusikiaka??? Inafadhiliwa na nchi gani au na nani??

Na huyu Dr (hc) A.L Mrema bado anatafuta cheo gani maana aliwaomba ubunge wakampa, kaomba M/kiti wa kamati ya bunge wakampa, bado ataka nini zaidi. Wanadhani kwa kuita Kamati ya Vijana featuring Dr. Mrema ndio itaondoa dhana kwamba hao sio CCM??

Mara nyingine mtu hushindwa kuamini kwamba hii CCM with all the resources (human and non human) at their disposal bado hawawezi kushindana kwa hoja. Wao ndio wenye serikali kwa nini wanashindwa kujibu hoja za kina Mbowe???
 
waungwana tunasema umechemka.Vijana waliojiweka tayari kutumika kufanya vurugu ni masela wa chadema na sio wengineo.Kijana mwenye mtindio wa ubongo ulio sawa haiingii akilini kwake kuwa kufanya vurugu kunaweza kubadilisha maisha yake yeye kama yeye, na kama maisha yake yeye kama yeye hayawezi kubadilika basi hakuna haja ya kuendea upuuzi huo. Mfano slaa anachochea hizo kwa vile kashindwa kuing

Another bogus in our country
 
MAANDAMANO ya kuunga mkono hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa mwishoni mwa mwezi uliopita, yanatarajiwa kufanyika Dar es Salaam Machi 16, mwaka huu, yakiwa na ujumbe ‘amani yetu bado tunaipenda’. Akizungumza na waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana wa Tanzania, wapenda amani, Said Mwaipopo alisema, pia maandamano hayo yatahusisha kupinga kauli viongozi wa CHADEMA zinazochochea kutokea kwa vurugu nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti huyo, inaeleza kuwa, vitendo na kauli za viongozi vya chama hicho vina lengo la kupandikiza chuki kwa Watanzania dhidi ya serikali iliyopo madarakani, ambavyo mavuno yake ni umwagikaji wa damu.
Alisema, maandamano yanayofanywa na CHADEMA huvishwa sura ya kupanda kwa gharama za maisha, wakati huohuo yakiwa na lengo la kuipinga na kutaka kuing’oa serikali.
Maandamano hayo yatafanyika kuanzia viwanja vya Mnazi Mmoja mpaka uwanja wa Bakhresa Manzese, na Mwenyekiti wa TLP Augustino Mrema anatarajiwa kuyaongoza.
source: www.uhurupublications.com

Kwani JK ni hotuba ya kwanza kuitoa, wamekosa cha kufanya. Hivyo vipandikizi vya Mafisadi hawana jipya zaidi ya kutapatapa.

Vp dau wanatoa shilingi ngapi? maana siku uhuru juzi walitoa hadi 60,000/= kwa washiriki.
 
Msomi hana sifa ya kutukana anapopewa hoja.Msomi hutakiwa kujibu hoja. Kaka umesema mimi nimetofautiana na wengine, nadhani hapa kila mmoja anauhuru wa kutoa mawazo yake. Kwahiyo wewe msomi umejibu kwa kuangalizia? nina wasiwasi na elimu yako, inaonekana ulikuwa mzee wa chabo, una degree ya chabo.wasomi kama wewe hamuhitajiki kwani akili yako huishughulishi kivyako unafata mkumbo. Pole sana.

we umezidi bwana yaani umetoa post inayo kera, na kwa lazima utakua hauna degree piga ua hata form 6 sidhani, yäani hujafikiria hata kidogo.
 
Back
Top Bottom