jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,987
- 22,515
Mkuu,Kwa walio na uraia pacha baada ya kufanya uchunguzi wangu nimeambiwa katika nchi nyingi hawakuambiwa waukane uraia wao wa kuzaliwa. Naambiwa walitangaza uraia wao wa kuzaliwa kwanza kwa kueleza nchi gani wanatoka na kisha kula kiapo cha uraia wa nchi ya kuasiliwa. Baada ya kula kiapo cha uraia wa kuasiliwa hawakunyang'anywa passport zao za nchi ya kuzaliwa licha ya kupewa form ya kuombea passport ya nchi ya kuasiliwa.
Kwa utaratibu huu hawajaukana uraia wa nchi zao za kuzaliwa, ila wametaja uraia wa nchi zao za kuzaliwa na kupokeleka katika nchi ya uraia wa kuasiliwa, vinginevyo passport zao wangenyang'anywa kama wanaponyang'anywa permanent resident card zao wanapoasiliwa uraia wao.
Tatizo haliko kwa wamarekani, wao wanaruhusu multiple citizenship na ndiyo maana hauruhusiwi kuukana.
Tatizo liko kwa bongo kama bado hawana sheria inayoruhusu uraia wa nchi mbili, hii issue mbona tushaijadili humu?